Busara Promotions waandaaji wa tamsaha maarufu la muziki Africa, Sauti za Busara, wanaadaa onyesho maalumu jijini Dar es salaam, litakalofanyika Trinity Bar Oyster Bay tarehe 29 Novemba, onyesho hilo litapambwa na Hoko Roro, Seven Survivor na Msafiri Zawose ambae atazindua albam yake mpya.

Lengo la onyesho ni kupata fursa ya kuwa pamoja na wasanii wa Tanzania, lakini pia kutangaza/ kuzungumzia tamasha la 11 la Sauti za Busara litakalofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe,Mji Mkongwe Zanzibar, kuanzia tarehe 13-16 February 2014. 

Katika onyesho hilo kutakuwa na uuzaji wa tiketi kwa punguzo maalum la asilimia 20 kwa wale watakaonunua kwa malipo ya moja kwa moja, au kwa malipo katika mtandao. Tunawaomba wapenda muziki kununua tiketi zao mapema.

Pia kutakuwa na bahati na sibu yenye zawadi za kuvutia kwa washindi.Mlango utafunguliwa saa mbili na shoo itaanza saa tatu kamili usiku, baada ya kumalizika kwa muziki wa moja kwa moja, kutakuwa na disko kabambe litakaloporomoshwa na DJ Davey mpaka majogoo.
Kiingilio ni shilling 15,000

0 comments:

 
Top