Tuesday, 29 May 2012

Mambo hayo

haya ni mabaki ya baadhi ya risasi ambayo yalionekana baadhi ya mitaa ya mji wa Unguja kufuatia vuru zilizojitokeza hivi karibuni

Saturday, 26 May 2012

THE UN SECRETARY-GENERAL MESSAGE ON AFRICA DAY

Each year, Africa Day provides an opportunity to acknowledge the achievements of the peoples and governments of Africa and to reaffirm the support of the United Nations for their efforts to build a better future.
The United Nations commends Africa’s recent efforts to consolidate its peace and security architecture, and to reject unconstitutional changes of power. We will continue to work with Africa in building durable peace, ending armed conflicts, boosting democracy, and promoting respect for fundamental human rights, especially the rights of women and youth.
Africa is a dynamic continent undergoing fundamental transformation. Even during the world economic crisis, Africa’s economies continued to expand, and growth forecasts remain positive. However, the benefits are not reaching all Africans. Poverty, hunger, and disparities in health, education, and participation in society, are preventing hundreds of millions of Africans from fully realizing their potential. Greater effort is needed by all to achieve the Millennium Development Goals by 2015.
The growing number of success stories across Africa indicates that broader social and economic progress is realistically attainable for most Africans. I have personally seen the dividends of investing in women’s and children’s health and sustainable agriculture. I have spent many hours with African leaders who are committed to peace, human rights, democracy and good governance.
The challenge is to extend these advances and ensure they reach all Africans, especially the continent’s poorest and most vulnerable people. In particular, we must address the spectre of hunger – from the highly visible periodic food emergencies to the hidden disgrace of stunting that is affecting a new generation of African children.
Many of these issues are on the table at the UN Conference on Sustainable Development next month in Brazil. Rio+20 is a once-in-a-generation opportunity to mould the future we want – a future where climate change and desertification are no longer threats; where devastating maternal and child mortality, and diseases such as TB and HIV/AIDS, are consigned to the past; where all people have access to safe drinking water and adequate sanitation.
From renewable energy to thriving oceans, from empowered women to productive partnerships between governments, civil society and business, Rio+20 is our chance to deliver for all, particularly Africa. On this observance of Africa Day, as the world tries to forge a renewed global partnership for sustainable development, I pledge to work with Africa’s leaders and people to implement an agenda that addresses Africa’s needs – an agenda that will set the continent on the path to the future we all want: dynamic, equitable and sustainable growth that benefits all Africans.

Wednesday, 23 May 2012

Vitambulisho vya Taifa

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)
Kumekuwepo taarifa kwenye baadhi ya mikoa nchini, kwamba fomu za usajili na utambuzi wa watu zenye lengo la kuchukua taarifa za wananchi na hatimaye kuwapatia Kitambulisho cha Taifa, kuanza kuuzwa kinyume na taratibu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ndugu Dickson E. Maimu, vitendo hivyo vimebainika kufuatia taarifa toka kwa wasamaria wema walioshuhudia fomu hizo zikiuzwa kwa wananchi.
Amesema vitendo hivi vinalenga kuwahadaa wananchi na hivyo kuwataka wawe waangalifu na kuwafichua wale wote wanaojihusha na uuzaji huu, ambao ni kinyume cha taratibu, kanuni na Sheria ya Usajili.
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), haijaanza kutoa fomu zozote za usajili kwa wananchi wa mikoani, zaidi ya mazoezi ya usajili kwa watumishi wa Umma kwa Dar-as-salaam, na Zanzibar, na zoezi la majaribio wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro lililofanyika mwezi Machi mwaka huu. Usajili rasmi wa wananchi kwa jumla unakusudiwa kuanza mapema mwezi Juni mwaka huu, kwa kuanzia na mkoa wa Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa taratibu zilizoko, Mamlaka ya Vitambulisho inasisitiza Fomu za Utambuzi na Usajili wa Watu ni BURE na HAZIUZWI, aidha kitambulisho pia kitatolewa bure kwa Wananchi, hivyo wananchi wasikubali kununua fomu mtaani. Utaratibu wa ugawaji fomu utatangazwa kwa wananchi hicho wakati utakapowadia kupitia vyombo vya habari.
Wananchi mnaombwa yeyote atakaye baini au kuwa na taarifa ya vitendo hivi kutoa taarifa kwenye kituo chochote cha polisi kilichoko karibu.
Mamlaka inawasihi wananchi mikoani kuwa watulivu kipindi hiki wakisubiri kuanza kwa usajili katika mikoa yao na kwamba NIDA itakuwa ikitoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi ili kujiandaa na usajili katika maeneo yao husika.

Jain Irrigation to Invest $375 Million in African Countries, PTI

Jain Irrigation Systems will invest $375 million (about Rs 2,000 crore) over the next few years to improve income of small and marginal farmers in African countries, including Nigeria, Kenya and Rwanda. JISL makes drip and sprinkler irrigation systems and components, piping systems, plastic sheets and agro processed products, among other farm products. It has presence in 120 countries and is one the largest drip irrigation companies in the world. JISL will partner and collaborate with the governments of Kenya, Rwanda, Ethiopia, Mozambique, Tanzania, Ghana, Cote d'lvoire, Burkina Faso, Nigeria and others. The company is launching significant African expansion programme which aims to provide an integrated set of irrigation and infrastructure solutions for small-holder and commercial farmers. It would also invest in creation of storage, handling, supply chain and processing infrastructure in the African countries.

Tuesday, 22 May 2012

Waandishi wa masuala ya kinsia

Ni baadhi ya washiriki wa mafunzo yahusuyo mambo ya Jinsi yanaliyoanyika katika hotel ye Peacock Dar-es-salam

Monday, 14 May 2012

JOB OPPORTUNITY


CHIEF EXECUTIVE OFFICER

The Zanzibar Stone Town Heritage Society (ZSTHS) was officially registered in 2002, and presently has over two hundred members. The aim of the Society is to work for the preservation and conservation of the Stone Town Heritage, and to promote environmental and social welfare of its inhabitants by conducting public talks, seminars and workshops, etc. Beside training and awareness, the Society is also engaged in advocacy, networking and research and oversees the operations of the Zanzibar Conservation Centre.

The Chief Executive Officer’s key role would be:
  • Manage the organisation in guidance with its constitution, objectives, strategic plan and policies
  • Responsible for the administration, management of the Society
  • Implementation of project activities
  • Project / proposal write-ups, fundraising initiatives, and report writing
  • Networking and advocacy in national, regional and international settings

Qualifications:
  • Relevant Bachelor / Master Degree in administration, management or other relevant field of education
  • Five to ten years experience in a management position( preferable in civil societies) added
  • Excellent computer skills
  • Fluent in Kiswahili and English is a must, other languages an added advantage
  • The CEO would be chief accounting officer of the society

The applicant should have a genuine interest in conservation and preservation matters and committed to community work. Self-motivation, an analytical mind and organisational skills are a must.

Written Application with CV and copies of transcripts must be delivered/mailed to the address latest by June  20, 2012.


Chairperson
Zanzibar Stone Town Heritage Society
CEO Application
P.O. Box 3892
Zanzibar
                                                             Tanzania
Email:info@zanzibarstonetown.org

Sunday, 13 May 2012

Picha mchanganyiko za Makamo wa Pili wa Rais

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Taasisi ya Kimataifa ya Mtandao wa Kibiashara unaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Bibi Yichen Mao. Bibi Yicheni ni wa pili kutoka kulia aliyevaa Kanzu ya Chui
 Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Maendleo ya Utalii jimboni Calirfonia Nchini Marekani Bwana Richard Soyomba akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Bw.Richard amekuja Nchini kufuatia ziara ya Balozi Seif aliyoifanya Nchini Marekani Mwishoni mwa Mwaka jana kuitangaza Zanzibar kwa Wawekezaji wa Marekani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bibi Sheen Limun kufuatia Nchi yake kuendelea kuiunga Mkono Zanzibar katika harakati zake za maendeleo.

Saturday, 12 May 2012

Mv Sea Gull yaharibika ikiwa safarini

Ni mara nyengine tana Mv Sea Gull ilyokuwa ikifanya safari zake kutoka katika kisiwa cha Pemba na Ugunja imeshindwa kufika kwa wakati, hii ni kutokana na kuharibika katika bahari ya Zanzibar inasemekana ilikiwa katika bahari ya Nungwi.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana zilisema kwamba boto hiyo ambayo mara baada ya kuharibika ilichukuwa na upepo na kufikia karibu na mwambao wa bahari ya Tanga, wakati huo huo abiri wengine walikuwepo katika bandari ya Unguja wakiisubiri boti hiyo kwa ajili ya safari za kwenda Dar

Friday, 11 May 2012

Msaada wa madawati kwa skuli za Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kupokea msaada wa Vikalio kwa ajili ya Wanafunzi wa Skuli za Zanzibar ndani ya kipindi cha Miezi sita ijayo. Msaada huo unaogharimu jumla ya shilingi milioni mia tatu na ishirini {320,000,000/- } umetolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Kampuni ya Nain Jin Tax ya Jimboni Sichuan.
Balozi Mdogo wa China Hapa Zanzibar Bibi Sheen Limun alieleza hayo wakati akizuungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Bibi Sheen alisema Msaada huo umekuja kufuatia Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyoifanya katika Jimbo la Sichuan Nchini China ambapo Kampuni hiyo iliahidi kutoa msaada huo mwezi Oktoba mwaka jana.
Katika Ziara hiyo Balozi Seif alimuakilisha Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda kwenye Tamasha la 12 la Maonyesho ya Biashara Jimboni Sichuan yaitwayo { Western China Expo }.
Balozi Sheen alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Msaada huo umeelekezwa kwenye Vikalio kuzingatia Skuli nyingi za Zanzibar zinakabiliwa na uhaba wa Vikalio.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa jitihada zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar. Balozi Seif alisema msaada huo kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza tatizo la vikalio kwa wanafunzi walio wengi hapa Nchini.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo ya Utalii katika Jimbo la Calirfonia Nchini Marekani Bwana Richard Soyomba.
Katika mazungumzo yao Bwana Soyomba ambaye amekuja Nchini kufuatia ziara ya Balozi Seif aliyoifanya nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana ameelezea kufurahishwa kwake na hali ya mazingira iliyopo hapa Zanzibar.
Bwana Soyomba ameahidi kwamba Taasisi yake itajaribu kuyashawishi Makampuni mbali mbali Nchini Marekani kuja kuwekeza hapa Zanzibar katika Sekta za Nyumba, Utalii na Umeme. Alitoa mfano wa Mradi za umeme unaotumia Jua ni muwafaka kwa mazingira ya Zanzibar kwa vile unaweza kuendeshwa na Wahandisi wazalendo wenyewe baada ya kupatiwa mafunzo. Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimueleza Bwana Soyomba kwamba Serikali itakuwa tayari kushirikiana na Makampuni au Taasisi zozote zilizoamuwa kuekeza Nchini kwa lengo la kustawisha Maisha ya Jamii.
Alisema Mipango maalum itaandaliwa na Taasisi husika zinazosimamia miradi tofauti Nchini ili kuona Makampuni ya Marekani yanaweza kuwekeza miradi yao Nchini.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Mtandao wa Kibiashara { Global Trade 2020 Limited } Bibi Yichen Mao alisema Zanzibar inaweza kupiga hatua kubwa zaidi ya Maendeleo endapo itakuwa na Miundo mbinu makini ya Umeme.
Bibi Yichen na Ujumbe wake alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhusiana na Mradi wa Umeme wa jua unaosimamia na kuendeshwa na Taasisi hiyo katika sehemu tofauti Duniani.
Alisema Taasisi yake imelenga kuelekeza nguvu zake za uzalishaji wa kiwango kikubwa cha umeme katika ukanda wa Mashariki mwa Bara la Afrika.
Akiushukuru Uongozi wa Taasisi hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushauri Uongozi huo kukaa pamoja na Watendaji wa Taasisi husika Nchini ili kuona jinsi gani wanaweza kupata mwanga wa kuujadili vyema mradi huo muhimu.
Balozi Seif alisema Zanzibar hivi sasa ina kianzio kimoja tu cha umeme jambo ambalo huleta usumbufu wakati inapotokezea hitilafu ya kiufundi. Taasisi ya Kimataifa ya Mtandao wa Kibiashara tayari imeshawekeza miradi ya umeme inayotumia nguvu ya jua katika Mataifa ya Spain, Italy, Bulgari kwa ulaya na Angola na Ghana kwa Afrika.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Late CHAIBA KOMBO [1966-2012]

It is with deep sadness that I received the news of Chaiba Kombo’s passing. Having known her for many years, there is no doubt that she was a dedicated writer who was very committed to developing her craft. In Tanzania today, where there is so much hype and excitement about a film industry, it is probably worth reflecting on why an individual like Chaiba, dedicated to education and professional development in her chosen field, found so little opportunity or support for her work.
Chaiba Kombo was born in Kigoma in the western region of Tanzania on 31st August 1966. She grew up in Mombasa, Kenya with her father who was a surveyor and a game warden. There, particularly during the school holidays between 1970 and 1985, she learned much about the forest and wildlife in the Shimba Hills and Tsavo National Park. She attended school at Kinango Full Primary [1974-1980] and Matuga Girls High School [1981-1982].
Chaiba’s talent for performing arts and writing emerged in 1981. As a participant in the national competition her play became the second award winner of that year. Following high school, she took secretarial studies at the Institute of Sales Promotion and was awarded certificates in English, Telephone Operating and typing in 1983. She later worked as a secretary and a telephone operator at the Flamingo Trading Company [1983 – 1986], and the Vatican City Hotel [1987-1989].
Between 1990 and 1993, while working with an American PhD candidate as the research assistant for her work on the history of Kigoma, Chaiiba began writing a novel ‘about my history’. She also began writing for newspapers including Nipashe and Lete Raha. In 1998 she joined the CTN Cable Vision as a producer of a TV play Mahari. This also opened new opportunities to become involved with filmmaking. These included participating in workshops at ZIFF in Zanzibar which she attended regularly, and other similar events across East Africa.
Since then, and inspired by the ZIFF programmes, Chaiba has produced radio plays, including the popular Angalia for Radio Tanzania, funded by DFID and Care International; and a ten-minute TV play Youth and AIDS in 1999 which won a UNAID Award in 2000. Chaiba was also a regular participant in Tanzania Screenwriters Forum and a member of Tanzania Independent Producers Association [TAIPA].
She produced a new version of Mahari in 2001 for DTV and continued to write stories and develop screenplays. Two of her original stories were produced for the African Tales short film series: The Prisoner became Siku ya Kustaafu/Retirement Day [2008] directed by James Gayo; and The Will became Wosia [2005] directed by Neema Kambona. She also co-wrote the screenplay for another film in the series, Mawazo [2008] directed by Nina Mnaya; and was an Assistant Director on Beatrix Mugishagwe’s award winning feature film Tumaini [2005].
Chaiba Kombo was not necessarily concerned with ‘red carpets’ or making newspaper headlines. She wanted to be a writer of the highest professional standard. She also wanted to tell her ‘Kigoma story’. She always said that the passion which drove her to write was her belief that Tanzania had too many untold stories and a rich history that was unknown to most of the population. She wanted to tell those stories and to see them in the cinema.
On behalf of Tanzania Independent Producers Association [TAIPA]
Imruh Bakari

Saturday, 5 May 2012

Balozi Seif aenda Cuba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anaondoka Nchini leo kuelekea Nchini Cuba Kupitia Nchini Israel kwa ziara ya wiki mbili ya Kiserikali.
Balozi Seif katika ziara hiyo anafuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad kwa upande wa Israel wakati ziara ya Cuba ataambatana na Waziri wa Afya Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dr. Malik Abdulla Juma. Akipitia Nchini Israel Balozi Seif anatarajiwa kukutana na Uongozi wa Taasisi zinazosimamia na kushughulikia masuala ya Maafa, Uokozi pamoja na majanga ya Matetemeko.
Hatua ya ziara hiyo imelenga kuimarisha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha kwamba inakuwa na uwezo zaidi wa kukabiliana na Maafa na Majanga kwa haraka wakati yanapotokea.
Akiwa Nchini Cuba Balozi Seif na Ujumbe wake anatarajiwa kukutana na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Nchi hiyo katika suala zima la Kuimarisha Uhusiano uliopo wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili.
Uhusiano huo utalenga zaidi katika masuala makubwa ya Sekta ya Afya ambapo Cuba imekuwa mshirika mkubwa wa Zanzibar katika kusaidia huduma za Afya katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Zanzibar hivi sasa inaendelea kufaidika na huduma za Madaktari Bingwa wa Cuba wanaoendelea kutoa huduma za Afya pamoja na Mafunzo kwa Madaktari 50 Wazalendo wanaotarajiwa kuhudumia Hospitali mbali mbali za Unguja na Pemba mara baada ya kumaliza mafunzo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atamaliza ziara yake Tarehe 19 Mei na kupitia Rasil Heyma kwa mualiko wa Mfalme wa Nchi hiyo Bwana Saoud Bin Qasimi.
Viongozi hao wawili watapata fursa ya kuzungumzia Miradi kadhaa ya Nchi hiyo inayokusudiwa kuwekezwa hapa Zanzibar ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anatarajiwa kurejea nyumbani Tarehe 22 Mei mwaka huu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Monday, 30 April 2012

Mhe.Fatma akifafanuwa kitu wakati alipokutana na waandishi wa habari afisini kwake Migombani-Zanzibar

Wasanii watakiwa waache majivuno

Wasanii Nchini wameaswa kuacha tabia ya kujisikia kupindukia mkapa wakati wanapokuwa tayari wameshakubalika kutokana na kuwasilisha fani yao kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akikabidhi Mchango wa Shilingi Milioni moja {1,000,000/- } kwa Kikundi cha Muziki wa Taarab cha Zanzibar One Taarab hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mchango huo aliomkabidhi Mkurugenzi wa Kikundi cha Zanzibar One Taarab Abdulla Ali { Du } unafuatia ahadi aliyoitoa Balozi Seif wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kutimia Miaka Mitano tokea kuanzishwa kwa Kikundi hicho zilizofanyika Katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar Tarehe 21 Aprili 2012.
Balozi Seif alisema kumekuwa na tabia inayoanza kutoa sura mbaya kwa wapenzi wa Sanaa na Hata Michezo mengine ya kuwalalamikia Wasanii na Wachezaji ambao hufanya kiburi baada ya kujiona wanatajika ndani ya Jamii.
“ Mastaa wetu hasa wale wanaojulikana zaidi na Jamii baadhi yao wamekuwa na tabia ya maringo jambo ambalo halipendezi kwa wapenzi wao. Wanajisahau kwamba wao ni kioo cha Jamii wanatakiwa kuwa mfano bora wa matendo yao ya kila siku” Alisisitiza Balozi Seif.
“ Kwa wenzetu walioendelea hasa Nchi za Ulaya na Bara la Asia Tabia hii imekuwa ni ya kawaida tu, lakini kwa sisi Nchi Maskini na changa tunaochipukia hatujafikia kuwa na hulka hii”. Aliendelea kufafanua zaidi Balozi Seif. Alikemea tabia hiyo kupigwa vita mara moja au vyenginevyo Wasanii na Wanamichezo hao Maarufu wanaweza kujikuta wakitengwa na Wapenza wao.
Balozi Seif aliendelea Kukipongeza Kikundi cha Zanzibar One Taarab kwa juhudi zake za Kutoa Burdani na hata Taaluma kwa Wapenzi na Wananchi kupitia Sanaa hiyo ya Taarab.
Aliwataka Wasanii hao kuendeleza Umoja na kushikamana miongoni mwao wakitambua kwamba bado wana dhamana na wajibu wa kutoa huduma kwa Jamii kupitia fani yao. Akipokea Mchango huo Mkurugenzi wa Kikundi cha Zanzibar One Taarab Ustadhi Abdulla Ali { Du } kwa niaba ya wana Kikundi wenzake alimshukuru Balozi Seif kwa kutekeleza ahadi yake ndani ya kipindi kifupi.
Mkurugenzi Du alisema Mchango wa Balozi Seif hasa wakati huu kwa kiasi kikubwa umekuwa chachu ya kukisogeza Kikundi chao katika hatua ya mafanikio zaidi. Abdulla Ali Alimuhakikishia Balozi Sei kwamba mchango huo uliokuja kwa wakati muwafaka utatumiwa kwa lengo la kukinufaisha zaidi Kikundi na Wasanii wake wote.
Kikundi cha Zanzibar One Taarabu kilichoanzishwa Mwaka 2007 hapa Zanzibar chini ya Mlezi wake Ustaadhi Mohd Ahmed kikiwa na Wasanii 18 miongoni mwao wanane ni wanawake kimelenga kutoa burdani kwa njia ya Taarab ya Kisasa. { Modern Taarab }.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

African music

Crossroads of African music, Dakar hosts of 3 to 5 May 2012 the Salam Music Expo, the show of African music. For 3 days, the exhibition brings together hundreds of professional musicians from Senegal, Africa and Europe. Program at a music market with exhibition stands, twenty concerts, professional meetings and workshops. Salam The Music Expo will be accompanied by a promotional compilation that brings together a dozen unreleased tracks by artists from the continent.
The Salam Music Expo represents a showcase for music professionals. All the actors in the music industry has the opportunity to present its activities, sell its products, meet professionals, to meet the public, make new collaborations, access to information, promote artists, discover new talents , exchange with government and civil society. The objective of Salam Music Expo is to promote African music, to highlight the economic potential of music to make it competitive African market.
- The professional meetings around the theme "music as a vehicle for development" held at the French Institute of Dakar Thursday, May 3 from 10 to 18 and Friday, May 4 from 10am to 13pm.
- The music market is held Saturday, May 5 from 10h to 19h at the House of Culture Douta Seck. It is open to producers, managers, talent agents, publishers, programmers, recording studios, festivals, concert venues, media, artists, artisans, instrument makers, audiovisual skills, sound business, professional organizations, any actor in connection with the world of music.
- The concerts are open to the public: French Institute Thursday, May 3 at night, House of Culture Douta Seck Friday, May 4th evening and Saturday, May 5 during the day, then a mega concert on driveways Centennial Saturday, May 5 evening with Omar Pene as sponsor of the event

Tuesday, 24 April 2012

Ni vyema kutunza mazingira ya bahari na kuwa safi

ni baadhi ya mabaki ya chomba ambacho kilizama na kuibuliwa katika bahari ya Zanzibar, inawezekana kabisa ni miongoni wa boti ambazo hazikuweza kutambulika kwa mara moja

Sanaa ni ajira siyo uhuni

Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Aya Yolu Jijini Dar es salaam kikitoa burdani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Sera ya Maji Barani Afrika unaoendelea kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach Jijini Dar es salaam

Mataifa ya Afrika yatakiwa kushirikiana kikamilifu

Mataifa ya Bara la Afrika yanapaswa kushirikiana katika kuhakikisha matatizo ya upatikanaji wa huduma za mazji safi na salama kwa ajili ya Jamii za Mataifa hayo yanatanzuka.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni wakati akiufungua Mkutano wa nne wa Siku tano wa Sera ya Maji Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kunduchi Beach Jijini Dar es salaam.
Dr. Sheni katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema yapop matatizo mengi yanayochangia ukosefu wa upatikanaji wa maji hali inayoendelea kusumbua Wananchi walio wengi hasa wale wa Vijijini.
Alisema ongezeko la Watu, harakati za Kilimo likiwemo lie la Mabadiliko ya hali ya hewa yanapelekea Mataifa mengi kushindwa kudhibiti matumizi bora ya huduma za maji.
Alifahamisha kwamba Viongozi, Taasisi za Kijamii , zile za Kiraia pamoja na Wananchi wanapaswa kuungana pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya Maji katika maeneo yao.
Alisisitiza kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 iwe imeshapiga hatua kubwa ya kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji safi.
Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni ameyapongeza Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni { Unesco } na ile Taasisi ya Utafiti wa Maji ya Kimataifa { IHP } kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Mataifa ya Afrika katika kukabiliana na tatizo la Maji.
Alisema Mataifa mengi ya Bara la Afrika bado yanakabiliwa na ukosefu wa fedha pamoja na ufinyu wa Teknolojia ya Kisasa hali ambayo inafaa iondoke kwa kuungwa mkono na Mashirika hayo.
Akimkaribisha Balozi Seif WEaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Tanzania Mh. Shukuru Kayambwa alisema utafiti unaendelea kufanywa na Wataalamu katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji unalenga kuwa na matumizi bora ya maji. Mh. Kayambwa alifahamisha kwamba huduma ya maji bado inaendelea kuwa muhimu kwa uhai wa Viumbe wakiongozwa na Mwanaadamu.
Mapema Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa { Unesco } kanda ya Afrika Profesa Joeoh massaquoi alisema Umoja wa Mataifa umeshaanza utafiti katika sekta ya Maji tokea mwaka 1975 ukiwa katika awamu sita.
Aliwapongeza Viongozi wa Bara l;a Afrika kwa uamuzi wao wa wa kutafuta mbinu za kukabiliana na tatizo hilo na kupanga mikakati ya kulinda rasilmali zilizomo barani humo ikiwemo ile muhimu wa Maji.
Mkutano huo wa nne unaofanyika Tanzania umeshirikisha wajumbe zaidi ya mia moja kutoka Nchi Tisa za Afrika wakiwemo pia Wataalamu wa Taasisi na Mashirika Hisani .Mikutano ya mwanzo ya Mataifa hayo imefanyika Nigeria mwaka 2006, Afrika Kusini mwaka 2008 na Nepal mwaka 2010.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Monday, 23 April 2012

Wasanii watakiwa wafanya kazi zao kibiashara zaidi


Wakati umefika kwa Vikundi vya Sanaa Nchini kuendelea kufanya kazi zao katika misingi ya Kibiashara ili kuwa na uwezo wa kujijengea mazingira ya kujitegema. 
Kazi ya sanaa si ya kuipuuza  wakati huu kwa vile  tayari imeshaonyesha muelekeo mpana wa kutoa ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana  katika sehemu mbali mbali Duniani. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo katika sherehe Maalum ya kutimia Miaka Mitano tokea kuasisiwa kwa Kikundi cha Taarab ya Kisasa Zanzibar { Zanzibar One Taarab } zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. 
Sherehe hizo za aina yake zilizobeba wapenzi mashuhuri wa Muziki wa Taarab ya Kisasa { Modern Taarab } zilipambwa na wimbo mzito wa Mapenzi yangu pokea ulioghaniwa na Msanii Gwiji wa Sanaa ya Taarab Zanzibar ambae pia ni Mlezi wa Kikundi cha Zanzibar One Taarab Ustaadhi Mohd Ahmed. 
Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  aliwapongeza Wasanii wa Kikundi hicho kwa juhudi zao za kutoa Burdani na kuwaomba waendelee kudumu na kuwa mahiri  zaidi.Alisema Vikundi vingi vya Sanaa huanzishwa vyema lakini hatma yake hufifia kutokana na migogoro lakini inapendeza kuona Zanzibar One Taarab bado inanawiri na kutamba. 
“ Kikundi chenu kina Wasani wazuri kama kungekuwa na tunzo naamini Kikundi hichi kingetokea mshindi. Kwa niaba yangu na Familia yangu nawapa  hongera kwa kutimia miaka mitano. Happy Birthday”. Balozi Seif alikifyagilia Kikundi hicho. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwa vile Sanaa ni ajira mfano wa Wasanii wa Ulaya ipo haja kwa Washirika wa Fani hii kuendelea kuunga mkono Kikundi kama hicho ili Vijana hao wawe na uwezo kamili wa kuendesha Maisha yao. 
Katika kuunga mkono juhudi za kikundi cha Zanzibar One Taarab Balozi Seif ameahidi kukizawadia Shilingi 1,000,000/- Kikundi hicho ili zisaidia kutunisha mfuko wake. 
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wasanii wenzake Mkurugenzi wa Kikundi hicho cha Zanzibar One Taarab Ustaadhi Abdulla Ali maarufu { Du  }  alisema lengo la kuanzishwa kwa Kikundi chao ni kutoa Burdani kwa Jamii kupitia Sanaa hiyo ya Taarab. 
Mkurugenzi Abdulla Du amewapongeza Viongozi na Washirika  wao wote walioamua  kujitolea kukisaidia Kikundi chao ambacho hivi sasa kiko katika muelekeo mzuri. 
Kikunci cha Zanzibar One Taarab kimeanzishwa Mwaka 2007 hivi sasa kikiwa na umri wa Mikaka Mitano. 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Saturday, 21 April 2012

Zanzibar yaipongeza CUBA kwa misaada yao kwenye sekta ya afya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Serikali ya Cuba kwa uwamuzi wake wa kuendelea kusaidia kuiunga mkono Zanzibar katika masuala ya Huduma za Afya.
Pongezi hizo amezitoa hapo nyumbani kwake Mazizini wakati akizungumza na Madaktari Bingwa wa Cuba wanaotoa huduma za Afya Nchini baada ya kumaliza nao chakula cha pamoja cha usiku.
Balozi Seif Alisema Zanzibar hivi sasa imepiga hatua kubwa ya Maendeleo katika huduma za Afya ambapo Cuba ina mchango mkubwa na wa muda mrefu wa Utaalamu katika fani hiyo.
Alisema Afya ni miongoni mwa sekta ziliyopewa msukumo mkubwa na Serikali katika Sera ya kuwa na Kituo cha Afya kwa kila masafa ya Kilomita Tano Unguja na Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba sera hiyo inatarajiwa kwenda sambamba na mpango wa Wizara ya Afya wa Kuwapatia Taaluma Madaktari wazalendo 50 Chini ya Wataalamu wa Cuba.
“ Kundi hili la Madaktari 50 Wazalendo wanaofunzwa na Walimu wa Cuba litasaidia kupunguza uhaba wa Madaktari liliopo hapa Zanzibar”. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Aliowaomba Madaktari hao kujihisi kwamba huduma wanazozitoa zinafanana na zile walizokuwa wakizitoa Nchini kwao na Serikali itakuwa tayari kushirikiana nao ili lile lengo lao la kuwepo Zanzibar liweze kufanikiwa .
Naye Kiongozi wa Madaktari hao 16 Kutoka Nchini Cuba Dr. Freddy Fagindo alisema yeye na Timu yake wameelezea furaha yao kutokana na ukarimu mkubwa wanaoupata kutoka kwa Wananchi wa Zanzibar.
Dr. Freddy alimuhakikishai Balozi Seif kwamba Taaluma pamoja na huduma wanayoitoa itawafikia Walengwa ambao ni Wananchi walio wengi.
Kiongozi huyo wa Timu ya Madaktari wa Cuba ambae kituo chake kipo Mjini Dar es salaam alieleza kwamba Sera za Cuba ni kuona Taaluma iliyomo ndani ya Nchi hiyo inasambaa katika maeneo inayohitajia popote pale Duniani.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Friday, 20 April 2012

HOTUBA YA MHE. MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, BALOZI SEIF ALI IDDI ALIYOITOA KATIKA UFUNGAJI WA MKUTANO WA SABA WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR TAREHE 20 APRIL, 2012

1.0 Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehma zake za kutukutanisha hapa tukiwa wazima na afya njema na pia kwa kutuwezesha kufanikisha Mkutano huu wa Saba wa Baraza letu Tukufu. Shukurani zangu za dhati na Wajumbe wenzangu zikufikie wewe Mheshimiwa Spika pamoja na timu yako yote kwa kuendesha vikao vyetu kwa umahiri na umakini mkubwa. Pia, nawashukuru wale wote waliofanikisha mkutano huu wa saba kwa njia moja au nyengine; wakiwemo ndugu zetu mafundi mitambo pamoja na waandishi wa habari ambao muda wote wamekuwa nasi kufikisha majadiliano yetu ndani ya ukumbi huu, kwa wananchi wenzetu.
2.0 Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii adhimu kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein kwa mashirikiano mazuri ambayo yalipelekea Rais Kikwete kuteua Tume ya Taifa ya Kuratibu Maoni na Mapendekezo ya Wananchi ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye wajumbe sawia kutoka pande mbili za Muungano; wajumbe 15 kutoka Zanzibar na wajumbe 15 kutoka Tanzania Bara. Wajumbe hawa 30 wameteuliwa kutoka tabaka mbali mbali za jamii yetu, wamo kutoka Vyama Vya Siasa, Jamii za Kiraia, Walemavu, Waandishi wa Habari na kadhalika. Kuteuliwa kwa Tume hii yenye Wajumbe wazito kumekidhi haja na matarajio ya wananchi wengi wanaosubiri kwa hamu kutoa maoni yao. Naomba uniruhusu niwapongeze kwa dhati kabisa wajumbe wote wa Tume hiyo na ninawatakia kazi njema yenye ufanisi ya majukumu iliyopewa.
Sisi Wawakilishi jukumu letu kwa sasa ni kuwaelimisha wananchi wetu kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwa uhuru bila ya woga wakati utakapowadia. Lakini ikumbukwe kuwa wakati huu ni muhimu sana kuvumiliana na kufuata taratibu zilizowekwa ili kutoa nafasi nzuri kwa kika mwananchi kuheshimu mawazo ya mwenzake na huu ndio msingi mzuri wa Demokrasia.
Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Mohammed Raza Hassan Dharamsi kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Ni mategemeo ya wananchi wa Jimbo hilo kuvuna matunda bora baada ya kupanda mbegu bora. Mhe. Raza ni chuma cha pua, ni dhahiri sasa wananchi wa Uzini watapata maendeleo kwa haraka zaidi.
Aidha, napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa wafuatao kwa kuteuliwa kushika nyadhifa mpya. Nampongeza Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mheshimiwa Ramadhan Abdallah Shaaban kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Maji, Makaazi na Nishati, Mheshimiwa Abdillahi Jihad Hassan kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Suleiman Othman Nyanga kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mheshimiwa Said Ali Mbarouk kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Mheshimiwa Mansour Yussuf Himid kwa kuteuliwa kuwa Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum. Nawaombea kwa Mwenezi Mungu awajaalie hekima na mafanikio makubwa katika nafasi zao. Wenzetu hawa wanamaliza Mkutano wa Saba wakiwa na nyadhifa tofauti na zile walizoanzia mkutano huu. Hongereni sana.
3.0 Mheshimiwa Spika, tumeanza mkutano huu wa saba bila ya mwenzetu, ambaye ametangulia mbele ya haki, Mheshimiwa Salum Amour Mtondoo, Mwakilishi wa Jimbo la Bububu kwa tiketi ya CCM. Mwenzetu huyu tutamkumbuka kwa uchapaji kazi wake bora. Alifuatilia kwa karibu matatizo ya Jimbo lake na alipenda sana kushirikiana na wenzake katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Kwa mara nyingine tena kwa niaba yangu na kwa niaba ya wajumbe wote wa Baraza lako tukufu napenda kutoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu na sote kwa pamoja tumuombee mwenzetu makaazi mema peponi. Amin.
4.0 Mheshimiwa Spika, mkutano wetu huu wa saba umepata baraka ya kupokea na kujadili kwa kina Miswaada saba ya Sheria na hatimaye Waheshimiwa Wajumbe kwa busara zao wameipitisha miswaada hiyo. Miswaada hiyo ni kama ifuatayo:-
(i) Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Ulipaji Mafao ya Viongozi wa Kitaifa Na. 4 ya Mwaka 1988 na Sheria ya Viongozi wa Kisiasa Nam. 6 ya Mwaka 1999 na kutunga Sheria Mpya ya Maslahi ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa baada ya Kustaafu Pamoja na Mambo Mengine yanayohusiana na Hayo.
(ii) Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Tume ya Mipango Nam. 5 ya 1989 na Kutunga Sheria Mpya kwa ajili ya Uendeshaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Kazi zake, Uwezo wake na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(iii) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(iv) Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Utumishi wa Umma na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
(v) Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Baraza la Mitihani la Zanzibar na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(vi) Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Utalii Nam. 6 ya 2009.
(vii) Mswada wa Sheria wa Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
5.0 Mheshimiwa Spika, kutokana na kupitishwa kwa Sheria ya Tume ya Mipango, muundo wa tume hiyo unaendelea kutayarishwa kwa kuziunganisha Idara zote za Mipango, Sera na Utafiti kuwa chini ya usimamizi wa Tume ya Mipango. Aidha, Tume imo katika mchakato wa kuzifanyia mapitio kamati za mipango za mawizara mbali mbali ili kuhakikisha mipango ya Serikali inaenda sambamba kwa Serikali nzima.
6.0 Mheshimiwa Spika, Mswada wa Kamisheni ya Utalii ulipita kwa taabu kidogo hasa pale Wajumbe walipotofautiana kuhusu suala la ajira liwe kwa Mtanzania au Mzanzibari. Hii ndiyo demokrasia ilioonekana ndani ya Baraza letu ingawa hatimaye, Wajumbe waliotaka neno Mtanzania litumike ndani ya mswaada huu badala ya Mzanzibari wameshinda. Sina nia ya kurejesha mjadala huu lakini napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Wajumbe wote waliosema ndio na wale waliosema hapana kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia. Aidha, napenda kusema kuwa kuukubali Utanzania sio dhambi na wala sio usaliti wa Uzanzibari na kuukubali Uzanzibari sio dhambi na wala sio usaliti wa Utanzania. Naomba sana tusinyoosheane vidole kwa mambo haya. Tupimane uzalendo wetu kwa nchi yetu kwa vitendo vyetu. Tujiulize naisaidiaje nchi yangu kuendelea mbele? Nalipa kodi? Najiepusha na rushwa? Natumia madaraka yangu kwa maslahi ya nchi au kwa maslahi yangu? Nina hakika sote tunaipenda nchi yetu na tungependa kuona inaendelea vyema kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru sana Wajumbe wote wa Baraza lako tukufu, kwa kuipitisha Miswaada yote ambayo Serikali iliiwasilisha mbele yao. Naelewa wamefanya hivyo kwa lengo la kuipa nafasi Serikali yao kutekeleza mipango inayojipangia kwa ufanisi zaidi ili hatimaye tupige hatua ya maendeleo. Sasa kazi iliyo mbele yetu tushirikiane kwa pamoja katika kusimamia sheria hizi tulizozipitisha ili kukidhi matarajio ya wananchi wetu. Sheria isiyosimamiwa vizuri haiwezi ikatufikisha pale tunapotaka kufika. Zaidi ya hayo, tutakuwa tunakaribisha pole pole bila ya kujifahamu utawala wa mwenye nguvu mpishe badala ya utawala bora ambao msingi wake mkubwa ni watu wote ni sawa mbele ya sheria.
7.0 Mheshimiwa Spika, katika mkutano wetu huu wa saba mbali na Miswaada tuliyoijadili na kuipitisha, Baraza lako Tukufu pia lilipokea na kujadili Ripoti mbali mbali za Kamati za kudumu zikiwemo:
1. Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii;
2. Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari;
3. Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi;
4. Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
5. Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo;
6. Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa;
7. Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC); na
8. Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi.
Napenda kuwashukuru na kuwapongeza Wenyeviti wa Kamati hizi pamoja na Wajumbe wao kwa kuandaa ripoti hizo nzuri zilizochunguza kwa kina mienendo ya Mawizara mbali mbali na Taasisi zao. Ripoti hizo zimesaidia sana kuitanabahisha Serikali katika mapungufu mbali mbali yaliyogundulika. Serikali itayazingatia kwa makini mapungufu yote yaliyogundulika kuchukuliwa hatua zifaazo kuyarekebisha au kuyaondoa kabisa mapungufu hayo. Na kwa kupitia Baraza hili Mhe. Spika nawaagiza Mawaziri wote kuzisimamia vyema wizara zao pamoja na Taasisi zilizo chini yao ili mapungufu hayo yasitokee tena.
8.0 Mheshimiwa Spika, Wajumbe wako pia walipata nafasi ya kupata Taarifa ya Hoja ya Eneo la Bahari la Ukanda wa Kiuchumi iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu; Taarifa ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na Taarifa ya Hoja ya Ripoti ya Baraza la Manispaa ya Mji wa Zanzibar iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Aidha, Baraza lako Tukufu limepitisha marekebisho na mapendekezo ya kanuni za Baraza la Wawakilishi pamoja na kujadili hoja binafsi ya Mheshimiwa Hija Hassan Hija, Mwakilishi wa Kiwani kuhusu Ripoti ya Manispaa, Baraza imeona vyema liunde Kamati Teule yake ili ikafanye uchunguzi wake badala ya kujadili ripoti ambayo siyo yake. Kuhusu hoja binafsi ya Mhe. Hija, Baraza limeamua kuwa Kamati ya PAC ikafanye uchunguzi huo.
9.0 Mheshimiwa Spika, wakati wa kufunga Mkutano wa Sita wa Baraza lako Tukufu, nilizungumza kuhusu fedha zilizochangwa na wahisani na wananchi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi walioathirika kutokana na ajali ya meli M.V Spice Islander 1. Nilisema Serikali itazigawa mara moja fedha zilizopatikana kwa wananchi walioathirika na ajali hiyo baada ya kumalizika zoezi la uhakiki wa majina ya wale wote wanaostahiki kulipwa na wale wananchi wenzetu waliofariki na wale waliookolewa wakiwa hai. Napenda kuliarifu Baraza lako tukufu na wananchi wote kuwa Serikali tayari imeshaanza ugawaji wa fedha hizo kwa kisiwa cha Unguja na linaendelea vizuri. Hadi kufikia tarehe 17 April, 2012 kati ya watu 457 waliofariki watu 256 sawa na asilimia 57 tayari wameshapatiwa fedha zao. Aidha jumla ya watu 122 waliookolewa sawa na asilimia 63 wameshalipwa fedha zao kati ya watu 193. Nawale ambao walihusika katika ajali ile na majina yao hayajajitokeza katika orodha ya malipo Serikali itayafanyia tathmini na wale wote waliohusika Serikali itawapatia haki zao. Baada ya kumalizika kwa zoezi hili hapa Unguja, zoezi litaanza rasmi kwa upande wa Pemba, nalo litafanyika baada ya muda si mrefu.
Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena, nachukua fursa hii adhim kuwapongeza sana wananchi kwa ustahamilivu na uvumilivu wao ambao umetusaidia sana kuendesha zoezi hili la uhakiki wa majina hadi kufikia hatua ambayo sasa tunalipa fedha tulizoahidi kwenye Baraza hili. Tunatoa wito pia kwa wananchi wote kufika katika vituo walivyopangiwa kwa kufuata utaratibu unaoendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari hasa Shirika la Utangazaji la Zanzibar kupitia radio yake.
10.0 Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha mwezi Julai hadi Febuari 2011/2012 ni wa kuridhisha ingawa bado tumeendelea kuwa na changamoto katika upatikanaji wa rasilimali kutoka nje kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo. Katika kipindi hicho jumla ya Shilingi 340,969 milioni zimekusanywa sawa na asilimia 55.6 ya makadirio ya mwaka ya Tsh. 613,076 milioni. Aidha jumla ya matumizi katika kipindi hicho yamefikia Tsh. 296,766 milioni sawa na asilimia 69 ya makadirio ya mwaka.
11.0 Mheshimiwa Spika, zao la karafuu ni zao mama hapa kwetu Visiwani na litaendelea kuwa tegemeo la uchumi wetu kwa miaka mingi ijayo. Kwa bahati mbaya zao hili linakabiliwa na tatizo la ukongwe wa mikarafuu unaopelekea uzalishaji mdogo wa zao hili. Katika kutimiza azma ya kuimarisha zao la karafuu ili kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza kipato cha wananchi na Taifa kwa jumla, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inaendelea na kampeni ya upandaji mikarafuu katika maeneo yote husika ili kuutumia vyema msimu wa mvua zinazoendelea. Wizara ya Kilimo na Maliasili kupitia Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka imejiandaa kuhakikisha miche ya kutosha inapatikana katika vitalu vyake na kwamba wakulima wote nchini watapatiwa miche hiyo bila ya malipo. Nawaomba Waheshimiwa Wawakilishi wenzangu wanaotoka maeneo yanayolimwa karafuu kuichangamkia miche inayotolewa kwa kuwahamasisha wananchi katika majimbo yao kuipanda miche hiyo kwa wingi. Tunawaomba wakulima na wananchi wote kwa jumla kuitumia fursa hii adhimu kuzingatia maelekezo na masharti ya msingi yanayotolewa na wataalamu ikiwemo utayarishaji wa mashamba kabla ya kupatiwa miche hiyo.
12.0 Mheshimiwa Spika, kilimo cha Mpunga nacho kinaendelea vizuri msimu huu ikilinganishwa na msimu uliopita licha ya matatizo yaliyojitokeza ambayo yametokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Takwimu zilizokusanywa na Wizara ya Kilimo na Maliasili zinaonyesha kwamba jumla ya eka 28,400 sawa na asilimia themanini na mbili (82%) ya lengo lililowekwa zimelimwa Unguja na Pemba hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2012 na kazi bado inaendelea. Hata hivyo, upatikanaji wa ruzuku ya pembejeo na huduma za utayarishaji wa mashamba haukuweza kuwafikia wakulima wote kama tulivyotarajia kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wakulima waliohamasika na kujitokeza kutumia huduma hizo kulinganisha na uwezo uliokuwepo. Serikali itaendelea kufikisha huduma hizo kwa wakulima wengi kadri itakavyowezekana katika misimu ijayo ili waweze kuongeza uzalishaji na hatimae kujiongezea chakula na kipato chao na Taifa kwa jumla. Aidha, Serikali inawaomba wakulima kuzingatia ushauri unaotolewa mara kwa mara na wataalamu wetu wa kilimo kupitia vyombo vya habari, ikiwemo matumizi ya mbegu bora na kulima kwa kuzingatia mabadiliko ya miongo ya mvua ili waweze kuepuka hasara zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo msimu uliopita.
13.0 Mheshimiwa Spika, sekta ya mawasiliano ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu. Mipango ya Serikali yetu ya kuunganisha miji na vijiji kwa mtandao wa barabara itaendelea kutekelezwa kwa kasi zaidi Unguja na Pemba. Katika kikao kilichopita cha Baraza letu nilizungumzia barabara ya Mfenesini – Bumbwini yenye urefu wa kilomita 13.2 kuwa iko katika hatua za kukamilika. Napenda kulijulisha Baraza lako Tukufu kuwa barabara hii imekamilika sasa pamoja na madaraja ya Mwanakombo, Tingatinga na Mto wa Maji. Kukamilika kwa barabara hii pamoja na madaraja niliyoyataja kunategemewa kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo usafirishaji wa bidhaa kwenda kwenye masoko kwa urahisi zaidi pamoja na kufungua maeneo yetu kwa wawekezaji wa ndani na nje. Nawaomba wananchi wanaoishi sehemu ambazo madaraja hayo yamejengwa kuwa walinzi dhidi ya uharibifu wa aina yoyote ile ili yaendelee kutuhudumia kwa miaka mingi ijayo kama tulivyokusudia. Aidha, nawaomba madereva wanaotumia madaraja haya kuwa waangalifu kwani uzoefu wetu unaonyesha kuwa ajali nyingi za barabarani Mkoa wa Kaskazini hutokea mara kwa mara sehemu zenye madaraja. Nawaomba sana wadereva hao waepuke ajali hizo kwa kufuata sheria za barabarani.
14.0 Mheshimiwa Spika, Serikali yetu kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo hivi karibuni imekarabati mtambo wa mawimbi mafupi (short waves) uliopo Dole kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Mtambo huo umekabidhiwa kwa Serikali tarehe 9 Machi, 2012. Kukarabatiwa kwa mtambo huo kunafanya matangazo ya redio ya Shirika la Utangazaji (ZBC) kusikika hadi nchi za Mashariki ya Kati.
Wizara pia inaendelea na ujenzi wa studio na ofisi katika eneo la Bungi pamoja na nyumba mbili za kisasa za wafanyakazi zinazojengwa kwa lengo la kuimarisha utendaji mzuri wa kazi. Studio imehamishiwa Bungi kutoka Chumbuni kwa sababu za usalama wa ndege uliokuwa ukihatarishwa na mnara uliokuwepo huko.
15.0 Mheshimiwa Spika, sekta ya Utalii itaendelea kuwa tegemeo la uchumi wa nchi yetu na ndio maana Serikali yetu kila inapoona kuna haja ya kujenga mazingira mazuri kwa lengo la kuimarisha sekta hiyo huwa inafanya hivyo. Marekebisho ya Sheria namba 6 ya Mwaka 2009 na Mswaada wake kupitishwa na Wajumbe wa Baraza lako Tukufu katika mkutano huu ni hatua muhimu kuelekea kwenye utalii utakaosaidia juhudi zetu za kujenga maisha mazuri kwa wananchi wetu. Kamisheni yetu ya Utalii katika jitihada zake za kuimarisha Utalii nchini kwa njia ya kuitangaza Zanzibar katika nchi mbali mbali duniani imepata mafanikio mazuri. Hivi karibuni Zanzibar imepata tunzo ijulikanayo “The Annual Russian Tourism Award” kwa kuwa kituo bora cha utalii barani Afrika. Tunaipongeza Kamisheni yetu ya Utalii kwa mafanikio haya makubwa na tunawaomba waendelee na jitihada zao za kuitangaza Zanzibar duniani kote. Hata hivyo, ni vyema ikaeleweka kuwa kazi ya kuitangaza Zanzibar ni kazi yetu sote. Wengi wetu Barazani hapa tunapata fursa ya kutembelea nchi tofauti duniani. Tutumie basi fursa kama hizo kuitangaza nchi yetu kwa watu tunaokutana nao.
16.0 Mheshimiwa Spika, Taifa letu linatambua haki za walemavu. Watu wenye ulemavu wana haki na fursa sawa kwa wote. Si vyema kwa jamii yetu kuendelea na tabia ya kuwanyanyasa na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu. Taasisi nyingi za Serikali hivi sasa zinajenga majengo mapya. Natoa wito kwa wale wote wanaojenga majengo kwa ajili ya kutoa huduma za umma, kuhakikisha kwamba majengo hayo yanakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu. Kuwa rafiki maana yake mlemavu aweze kutumia jengo hilo kama watu wengine, kwa kuwekewa miundombinu ambayo itamrahisishia kuingia ndani ya jengo hilo na kutumia fursa zilizomo ndani yake. Kwa mfano, majengo hayo yanatakiwa kuweka vyoo maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu katika ghorofa zote za jengo na pia mlemavu apate fursa ya kwenda ofisi yoyote ndani ya jengo hilo bila ya vikwazo. Suala la ajira kwa watu wenye ulemavu wenye sifa na uwezo ni la umuhimu pia. Waajiri wasiwanyime fursa watu hawa kwa sababu tu ya ulemavu wao, ni muhimu kuangalia sifa na uwezo wao na kuwapa vipaumbele. Ubaguzi mzuri (Positive discrimination) wakati mwengine inafaa kutumika katika jamii kwa lengo la kuwanyanyua wale walioachwa nyuma. Kwa hivyo suala la kuwapa vipaumbele walemavu wakati wa ajira ni muhimu sana.
17.0 Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetayarisha Sera ya Mifugo ambayo imeweka mazingira mazuri na mikakati endelevu ya kuendeleza sekta ya mifugo. Sera ya sasa imezingatia mambo muhimu ya kuiendeleza sekta hiyo ambayo hayakuwemo katika sera iliyokuwepo. Mambo yaliyokuwemo katika sera ya sasa ni pamoja na mambo ya utafiti, ustawi wa wanyama, uzalishaji na utumiaji wa nishati itokanayo na samadi, kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo, kuendeleza uzalishaji wa ndani na upatikanaji mitaji ya fedha kwa wajasiriamali. Sera hii tunategemea itakuwa kichocheo cha ufugaji bora nchini.
18.0 Mheshimiwa Spika, nchi yetu ilikumbwa na uhaba wa mchele wiki za mwanzo wa mwezi wa Machi, 2012, hali ambayo ilisababisha bei ya mchele kupanda kutoka shilingi 50,000/= kwa kipolo cha kilo 50 mpaka shilingi 57,000/=. Hali hii ilisababishwa na kuchelewa kufika kwa mchele ulioagizwa mwishoni mwa mwezi wa Machi, 2012. Hata hivyo, tayari mchele umeanza kuingia kutoka nje ambapo kiasi cha tani 12,251 zimeingia mapema mwezi huu. Mchele huo unatarajiwa kutumika kwa miezi miwili, matumizi kwa mwezi yanakisiwa kuwa ni tani 6,000. Kwa upande wa bei hivi sasa imeshuka na mchele unapatikana kwa shilingi 52,000/= kwa kipolo cha kilo 50. Tunawasihi wafanya biashara kuacha tabia ya kuutorosha mchele wetu kimagendo kwa sababu ya kushuka kwake kwa bei.
19.0 Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kuanzisha kampeni ya Kitaifa ya kutoa dawa za Kichocho na Minyoo kwa Wananchi kuanzia tarehe 28 mwezi huu wa Aprili. Madhumuni ya kampeni hii ni kupambana na maradhi ya Kichocho na Minyoo ambayo yamekuwa yakisumbua Wananchi wengi hasa watoto katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu maradhi ya kichocho yameenea kwa asilimia 15 kwa kisiwa cha Pemba na asilimia 8 kwa kisiwa cha Unguja. Hii ina maana maradhi ya kichocho yapo katika Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba. Na kwa Unguja maradhi yamesambaa zaidi katika Mkoa wa Kaskazini. Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukuwa jitihada mbali mbali kutokomeza kichocho na minyoo ambapo kampeni hii ni mojawapo ya juhudi hizo.
Mheshimiwa Spika, dawa hizi ni za kuzuia wadudu wa kichocho na kuua minyoo iliyokuwemo mwilini, Dawa hizi hazina matatizo kwa afya ya binaadamu na Serikali imeamua kuzitoa dawa hizi bure. Hivyo natoa wito kwa wananchi wote kutokua na hofu juu ya madhara ya dawa hizi. Nawaomba Wawakilishi wenzangu kushajiisha na kuwaelimisha wananchi kula dawa. Narejea tena dawa hizi hazina matatizo kwa afya ya binaadamu tuzitumieni ili lengo la Serikali yetu la kutokomeza kabisa kichocho nchini ifikapo 2015 lifanikiwe.
20.0 Mheshimiwa Spika, kama tujuavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimo katika maandalizi ya Sensa ya Watu na Makaazi ambayo imepangwa kufanyika nchini kote kuanzia Jumapili ya tarehe 26 Agosti mwaka huu, Taarifa zitakazokusanywa katika Sensa ya mwaka 2012 zitatumika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2020 kwa Zanzibar, Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umaskini Zanzibar – MKUZA. Takwimu hizo zitatumika pia kutathmini utekelezaji wa malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2015.
Mheshimiwa Spika, kauli mbiu ya Sensa ya safari hii ni “Sensa kwa Maendeleo ya Taifa: Jiandae kuhesabiwa”. Kauli mbiu hii tuifanyie kazi sote kwa pamoja, Viongozi na wananchi tunaowaongoza katika kufanikisha sensa ya safari hii. Maelezo mengi yametolewa kuhusu umuhimu wa sensa kwa maendeleo yetu. Kwa kifupi sensa inatueleza sisi ni nani na kwa namna gani tumebadilika kwa kipindi kilichopita. Takwimu za sensa zinasaidia sana Serikali kupanga mipango yake kwa kuelewa vyema mahitaji ya wananchi wake. Takwimu hizi pia zitatusaidia katika kushajiisha uwekezaji katika nchi yetu. Takwimu sahihi za idadi ya watu, hali ya uchumi wa nchi kwa jumla ni miongoni mwa taarifa muhimu kwa muwekezaji. Kwa rafiki zangu wafanyabiashara, takwimu za sensa zitawasaidia wapi katika nchi wafungue biashara zao. Sisi Wanasiasa pia takwimu hizi za sensa zitatusaidia kuelewa wapiga kura wengi tutawapata vijiji vipi! Takwimu za sensa tutakazozipata baada ya sensa hii ni mali kwa kila mwananchi, inategemea tutazitumia vipi. Maelezo mengi kuhusu Sensa hii tumeshayapata kupitia Semina mbili tulizofanyiwa na Wataalamu wetu wa Sensa. Ni matumaini yangu kwamba yale yote tuliyoelezwa katika semina hizo tutayafanyia kazi ipasavyo.
21.0 Mheshimiwa Spika, jukumu la kila Kiongozi kuanzia chini hadi juu kuelekeza uongozi wake wa busara katika kufanikisha sensa ya mwaka huu na jukumu la mwananchi kuanzia sasa kuhakikisha kuwa siku ya Sensa inapowadia anakuwa mstari wa mbele katika kuhesabiwa. Natoa wito kwa Makampuni mbali mbali nchini yajitokeze kusaidia kuhamasisha sensa ya mwaka huu. Milango iko wazi Makampuni hayo kushirikiana na Kamati ya Taifa ya Sensa katika kuhamasisha wananchi kwa vipeperushi au hata kuchapisha fulana na mambo kama hayo.
22.0 Mheshimiwa Spika, sote ni mashahidi nchi yetu iko katika hali ya kupigiwa mfano wa Amani na Utulivu na hasa baada ya Kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi yenye Mfumo wa Umoja wa Kitaifa. Matumaini ya wananchi wetu, hali hii itabakia na itaendelea kwa kizazi kilichopo na kijacho. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa upande wake imedhamiria kwa dhati kudumisha hali hii ya amani na utulivu Visiwani mwetu. Kurasa zetu za historia ambazo zilijaa migogoro ya kisiasa, uhasama na hali ya kutoaminiana, tumezitia moto; kurasa tulizonazo tunaandikia historia yetu mpya, kichwa chake cha habari kinasomeka; Umoja, Amani na Utulivu. Ndani ya kurasa hizo habari tunazozinakili na ambazo zimetawala ni maendeleo kwa wote; haki kwa wote; maji safi kwa wote; elimu bora kwa wote, afya njema kwa wote na kadhalika. Hakuna mwenye ubavu kubadilisha kichwa hiki cha habari kwani wenyewe tupo macho. Pia hakuna mwenye ubavu kubadilisha yale tunayoyanakili kwenye kurasa hizi kwani wenyewe tupo, kuangalia.
23.0 Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumetokea kikundi cha wenzetu wachache kinachoendesha makongamano na mihadhara inayotishia hali yetu ya amani na utulivu niliyoielezea. Kikundi hiki mbali na kuhamasisha kwa nguvu watu kuukataa Muungano pia kinatukana kwa nguvu Viongozi wetu na wale wanaounga mkono Muungano.
Mheshimiwa Spika, Serikali haikatazi kikundi chochote kuendesha mihadhara au makongamano nchini na ndio maana tumevumilia tukidhani kuwa nia ya mihadhara hiyo ni kuelimisha jamii, lakini mihadhara hiyo imebadilika sura na badala ya kuelimisha imekuwa ni uwanja wa kashfa, kejeli na matusi tena matusi mengine ni ya nguoni kwa Viongozi wetu, jambo ambalo ni kinyume kabisa na utamaduni wa mzanzibari na misingi ya kidemokrasia.
Mheshimiwa Spika, napenda ieleweke wazi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitakivumilia kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi wetu. Hatuko tayari kurudishwa kule tulikotoka ambako tukiishi kwa chuki na uhasama mkubwa. Hatutasita kukizuwia kikundi chochote kile kuendesha mihadhara au makongamano tutakayobaini yanahatarisha usalama wa nchi yetu. Kwa hili hatutokuwa na muhali na mtu yoyote yule.
Mheshimiwa Spika, ninawaomba sana Wtanzania wenzangu kuwa fursa iliyotolewa na Serikali zetu kwa kuleta mchakato wa katiba mpya ni jambo la kihistoria na linaloonesha kukuwa kwa demokrasia katika nchi yetu. Hivyo litakuwa ni jambo la busara sana kutumia fursa hii kwa mustakabali wa nchi yetu badala ya baadhi ya wenzetu kujitokeza kuharibu dhamira njema ya Serikali.
24.0 Mwisho, Mheshimiwa Spika, kwa mara nyengine tena napenda kukushukuru wewe binafsi na kwa kupitia kwako kwa Naibu Spika na Wenyeviti wetu wa Baraza la Wawakilishi kwa namna mlivyouendesha mkutano huu kwa busara na utulivu mkubwa. Mkutano huu ulijaa hekima, maarifa na uvumilivu mkubwa. Hivyo, napenda niwapongeze Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza kwa michango yao mizuri iliyokuwa ya faida kubwa kwa Serikali. Hii imeonyesha uwezo wao wa kuisimamia na kuielekeza Serikali vizuri. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeithamini sana michango hiyo na naahidi Serikali itachukua hatua kwa yale yote ambayo Wajumbe wameyaelekeza.
25.0 Mheshimiwa Spika, kuhusu taarifa ya Kamati Teule ambayo imewasilishwa katika Baraza lako Tukufu na kuchangiwa na Waheshimiwa Wajumbe kadhaa wa Baraza lako tukufu. Kwa niaba ya Serikali nachukua fursa hii kuipongeza sana kazi iliyofanywa na Kamati hiyo pamoja na michango yote iliyotolewa kuhusiana na ripoti hii.Ripoti ya Kamati Teule imetupa nafasi nyengine kama Serikali kuona namna ambavyo Baraza la Wawakilishi katika Awamu ya Saba ya Serikali ya Zanzibar imejipanga kuona kuwa Serikali inabadilika katika utendaji wake na uwajibikaji wake.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi hizi za Baraza la Wawakilishi kwa sababu zimeunga mkono kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Saba kuwa tunaachana na utendaji wa kimazoea (Business as usual).
Mheshimiwa Spika, mara zote Mhe. Rais wa Zanzibar anakuwa akisema “Tushirikiane kupambana na rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma kwa lengo la kujenga Taifa lenye kufuata Utawala Bora, usawa na Haki za Binadamu”. Lazima sote ndani ya Serikali tuuheshimu msemo huu wa Rais wetu.
Mheshimiwa Spika, Serikali inachukulia taarifa ya Kamati Teule (miongoni mwa Kamati nyengine za Baraza) kuwa ni mchango thabiti wa Baraza katika kuunga mkono juhudi na mwelekeo wa Serikali ya Zanzibar ya Awamu hii. Serikali kuu imetoa mwelekeo, Baraza la Wawakilishi limetoa mfano mzuri juu ya mwelekeo huo. Sasa nijukumu la Watendaji wa Serikali katika ngazi zote kufuata nyayo, na tunakiri kuwa ni jukumu la Uongzi wa juu wa Serikali kulisimamia jambo hili.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeyasikia vizuri maelezo yaliyomo kwenye taarifa ya Kamati pamoja na michango mizuri ya Wajumbe wa Baraza. Nataka kulihakikishia Baraza lako Tukufu kwamba Serikali nayo itakuwa makini sana katika kuifanyia kazi kwa vitendo Taarifa ya Kamati Teule.
26.0 Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa nawatakia Wajumbe wote safari njema ya kurejea Majimboni kwao ili wakaungane na wananchi wao kuendeleza harakati zao za kuyaletea Majimbo yao maendeleo.
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba kutoa hoja ya  kuliahirisha Baraza lako Tukufu hadi Jumatano tarehe 13 Juni, 2012 saa 3.00 asubuhi.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja

Tuesday, 17 April 2012

Sauti za Busara yatangaza tarehe ya tamasha la mwaka 2013

Busara Promotions inatoa taarifa ya tarehe ya tamasha la 10 la sauti za busara ambalo liataanza tarehe 14 – 17 februari 2013 katika ukumbi wa kihistoria wa ngome kongwe, Zanzibar.
Sauti za busara ni tukio la muziki la kila mwaka ndani ya afrika mashariki na kufahamika zaidi kama ‘tamasha rafiki katika sayari’. Katika toleo la mwakani litawaletea wanamuziki 200: zaidi ya vikundi 20 kutoka afrika mashariki na kwingineko vitafanya maonyesho yao ya moja kwa moja (live)
Ngome kongwe patafanyika maonyesho ya muziki kwa siku tatu mfululizo, ratiba kuu itaendelea  mpaka jumapili kwa maonyesho kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 7 usiku.
Tamasha litaonyesha filamu za muziki wa kiafrika: Makala, video za muziki na matamasha, yote haya katika kuangazia uendeleza wa utajiri na mchanganyiko wa muziki wa afrika.
Sauti za Busara litaendelea na uendeshaji wa kongamano lijulikanalo kama Movers and Shaker kwa ajili ya wenyeji na wageni wataalam wa sanaa. Kongamano hili linatoa nafasi ya majadiliano, kubadilishana mawazo na uendelezaji wa mawazo ya ubunifu katika ukanda wa afrika mashariki na kwingineko.
Si tu tamasha linafanya uandaaji maonyesho, jamii inahimizwa kuandaa matukio ya ziada ya busara. Hayo yakiwemo Ngoma za kiutamaduni, Maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa na maonyesho ya vikundi vikongwe vya taarab ambayo yanaandaliwa na wenyeji.
Ni miaka tisa sasa tangu tamasha lianzishwe rasmi mwaka 2004, Tamasha limefanikiwa kuwapandisha jukwaani wasanii mbalimbali akiwemo Samba Mapangala & Orchestra Virunga, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate, Jagwa Music, Tumi & The Volume, Freddy Masamba, Thandiswa, Mlimani Pack Orchestra, Culture Music Club, Orchestra Poly Rythmo na wengineo wengi. Tamasha linafanya muziki wa moja kwa moja (Live).
Kuanzia mwezi wa nne wasanii wanaweza kufanya maombi ya moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya Sauti za Busara. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/7/2012. Tamasha linatafuta wasanii wanaochipukia na wakongwe ili mushiriki katika tamasha. Kitu cha muhimu ni maonyesho kufanyika moja kwa moja kwa asilimia mia (100% live) na hakika inaunganisha afrika.
Msanii anayetaka kutuma maombi kupitia tovuti yetu inabidi atembelee tovuti yetu ya www.busaramusic.org
Mwisho wa kupokea maombi ni 31/7/2012.
na akamilishe ujazaji wa fomu au kwa kupitia sanduku letu la posta kama ifuatavyo Busara Promotions, P O Box 3635, Stone Town, Zanzibar, Tanzania.

Saturday, 14 April 2012

Wawakilishi watakiwa kusimamia vyema utekelezaji wa sensa

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameombwa Kushirikiana na Viongozi wengine katika kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za Sensa katika Wilaya sambamba na kuhakikisha kuwa Elimu kwa Wananchi inatolewa ipasavyo.
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Semina ya Wajumbe wa Baraza hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Balozi Seif ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Taifa ya Sensa Tanzania alisema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni Miongoni mwa Wajumbe wa Kamati za Sensa za Wilaya.
Alisema ni vyema wakatumia nafasi zao kama Wawakilishi wa Wananchi kuhamasisha na kuelimisha Umma kuhusu umuhimu wa kushirikiana na Makarani wa Sensa wakati wa kipindi cha kuhesabu kwa kutoa Takwimu sahihi.
Alifahamisha kwamba hatua hiyo itasaidia kupata Taarifa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo. Balozi Seif alieleza kwamba Serikali hutumia Takwimu zitokanazo na Sensa katika kutunga Sera, kufanya maamuzi juu ya Utawala wa Umma kwa kuzingatia mahitaji halisi pamoja na vigezo vya umri na Jinsia.
“ Sensa ya Mwaka huu wa 2012 ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa Taarifa zitakazokusanywa zitatumika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa dira za Taifa za Maendeleo za Mwaka 2025 Upande wa Bara na Mwaka 2020 kwa Upande wa Zanzibar”. Alisisitiza Balozi Seif.
Mwenyekiti huyo Mwensa wa Kamati ya Tifa ya Sensa Tanzania aliongeza kuwa Takwimu hizo zitatumika pia kutathmini Utekelezaji wa Malengo ya Milenia ifikapo Mwaka 2015 na Ule Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa Mwaka 2011/12 hadi 2015/16.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mh. Omar Yussuf Mzee alisema Wajumbe wa Baraza hilo ambao watakuwa wajumbe wa Kamati za Sensa katika maeneo yao wataendelea kupata muendelezo wa Semina za mara kwa mara kwa kuhusiana na Masuala ya Sensa ya Watu na Makazi.
Mh. Omar alifahamisha kwamba nia ya kutolewa kwa Taaluma hiyo mara kwa mara kwa Wajumbe hao imelenga kuhakikisha kila mwana Jamii anaelewa na kutambua jukumu lake katika kuhakikisha Sensa ijayo inafanikiwa vyema.
Akizuingumzia Madodoso yaliyotayarishwa Waziri Omar alieleza kwamba Serikali imeamuwa kuwa na Dodoso la Jamii ambalo litafanyiwa kazi kwa mara ya kwanza ndani ya zoezi hilo la Sensa.
Alisema mapango unakusudiwa kufanywa kwa tathmini ya hali ya mazingira katika maeneo mbali mbali hapa nchini. Masuala 62 yanatarajiwa kuulizwa katika Dodoso refu wakati lile Dodoso fupi litakuwa na Maswali 37.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Friday, 13 April 2012

Sekta ya michezo yaimarika Zanzibar

Zanzibar inaendelea kufaidika na sekta ya Michezo kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Amani miaka michache iliyopita uliojengwa na Serikali ya Jamuhuri ya watu wa china.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Mpya wa China Nchini
Tanzania Bwana Lu Youqing aliyefika Zanzibar kujitambulisha rasmi. Mazungumzo ya Viongozi hao wawili yalifanyika kwenye Ofisi ya Balozi Seif iliyoko katika Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema Uwanja wa amani umezidi kuwa na hadhi zaidi ya kuchezewa kwa mechi za kimataifa na kukifanya kuwa miongoni mwa Viwanja muhimu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.
Aliipongeza Jamuhuri ya watu wa china kwa Makampuni yake kuendelea kutoa huduma hapa Nchini na kuelezea matumaini yake ya Zanzibar kuwa na kiwanja chengine cha Kimataifa hapo baadaye.
Alieleza kuwa uwanja huo uliopewa jina la Kiongozi wa China Mao Tse tung unatarajiwa kujengwa upya ili kukidhi mahitaji ya wana michezo nchini. Balozi Seif alisema uwanja huo utakapomalizika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutoa huduma nying za michezo pamoja na shughuli za Kitaifa ikiwemo ile maarufu ya gharide katika sherehe mbali mbali.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar


Thursday, 12 April 2012

Umuhimu wa kazi kazi kwa pamoja katika kukuza jamii bora

Ushirikiano wa pamoja kati ya Viongozi wa Serikali, Siasa pamoja na Taasisi za Kijamii ndio utakaowezesha ubora wa maandalizi hadi kufikia kukamilika kwa zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi hapa Nchini. Akikifungua Kikao cha Wakuu wa Mikoa , Wilaya pamoja na Maafisa Tawala wa Zanzibar hapo Ukumbi wa Jumba la Wananchi Forodhani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hakuna Kiongozi asiyeelewa umuhimu wa Sensa kwa Maendeleo ya Taifa. Balozi Seif alieleza kwamba Takwimu za Sensa wakati wote husaidia Serikali katika kufuatia utendaji wake hasa Dira ya Taifa ya Mwaka 2020 pamoja na Mpango wa kupunguza Umaskini Zanzibar { Mkuza }. Alisema Viongozi hao wana jukumu kubwa la kuhakikisha Taratibu nzima za Maandalizi ya Sensa katika kutoa Elimu ni vyema yanawafikia kwa wakati walengwa ambao ni Wananchi. “ Wakati muda unazidi kukaribia kinachohitajika zaidi hivi sasa ni uhamasishaji wa karibu kwa Jamii”. Alisisitiza Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi. Balozi Seif aliwaeleza Wakuu hao wa Mikoa, Wilaya ya Maafisa Tawala wao kwamba utayarishaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu hapa Zanzibar umeshakamilika likiwemo pia suala la Dodoso linalokadiriwa kuchukuwa takriban dakika 50 kila Kaya kwa lile Dodoso kubwa. Akitoa Taarifa juu ya Matayarisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Nd. Mohd Hafidh alisema zoezi la Sensa hasa katika Bara la Afrika limekuwa likikabiliwa na ufahamu finyu wa umri kwa Baadhi ya Watu ndani ya Jamii. Nd. Mohd Hafidh alisema tatizo hilo kwa kiasi Fulani limekuwa likiviza Mipango ya Kiuchumi na Maendeleo kwa Mataifa hayo ya Bara la Afrika. Alisisitiza kwamba kadri kasi ya uhamasishaji itakavyoendelea kuwa kubwa ndivyo Changamoto zilizopo kwenye uhamasishaji huo zinaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka. Nd. Mohd alieleza kuwa zoezi la Sensa halihitaji kuzuia shughuli za Wananchi lakini cha msingi ni kuhakikisha muhusika Mkuu wa Kaya anawajibika kuwa na kumbu kumbu na vielelezo vyote vya Familia anayoishi nayo. Hata hivyo Mtakwimu Mkuu huyo wa Serikali aliwaomba Wakuu hao wa Mikoa, Wilaya na Maafisa Tawala wao kuangalia vibali vya Shughuli zote zinazokusanyisha Watu kwa usiku wa kuamkia siku ya zoezi la Sensa vinazuiliwa kwa muda. Wakichangia Taarifa hiyo kuhusu Matayarisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 baadhi ya Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wameitahadharisha Serikali kuwa makini na baadhi ya Vikundi vinavyojihusisha na uhamasishaji ndani ya Jamii ambao uko nje ya Maadili ya malengo ya Taasisi zao. Wamesema uhamasishaji huo tayari umeanza kutoa cheche za muelekeo wa shari, Vurugu na uvunjifu wa Amani katika maeneo mbali mbali hapa Zanzibar. “ Ukwel lazima tuuseme. Wapo Vigogo waliojificha nyuma ya Vikundi hivyo wakichochea wimbi hilo lenye ishara mbaya ya kulipeleka Taifa katika Migogo isiyotambulika hatma yake”. Walitahadharisha baadhi ya washiriki wa kikao hicho. Sensa ya Watu na Makazi inayokadiriwa kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 27 za Kitanzania inatarajiwa kufanyika Usiku wa Jumapili wa Tarehe 26 Mwezi wa Nane mwaka 2012.
 Othman Khamis Ame
 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar