Kampuni ya usafiri wa anga.. Ethiopian airlines imejitokeza kudhamini Tamasha la 16 la filamu Tanzania, ZIFF linalotazamiwa kufanyika Zanzibar, June 29 hadi July 7, 2013. Meneja na Mkurugenzi msaidizi wa Tamasha hilo Daniel Nyalusi maarufu kwa kifupisho cha Dean alisema wanajisikia furaha sana kushirikiana na Kampuni hiyo, na kwamba anatarajia ushirikiano huo utafungua njia kwa makampuni mengine.
Aidha Dean alisema Ethiopian Airlines ndio wamekuwa wadhamini rasmi wa usafirishaji wa watengenezaji filamu na wageni wote wa ZIFF kimataifa na kuongeza kuwa Tamasha la ZIFF 2013 linatarajiwa kufana zaidi kutokana na maandalizi yake na udhamini huu mkubwa wa Ethiopian Airline.
Pamoja na Ethiopian Airlines kampuni nyingine iliyojitosa kwenye udhamini wa Tamasha hilo ni ZUKU TV, hii itakuwa mara ya pili kampuni hii kushiriki katika kuunga mkono Tamasha hilo, ambalo kwa miaka 16 iliyopita limesherehekea kazi za sanaa nchini na kuwezesha uzalishaji wa filamu hapa Tanzania na duniani kote. Akizungumziaa ushirikiano huo, Meneja wa ZIFF, Daniel Nyalusi alisema “ ZUKU inadhamini dola laki moja kila mwaka kwa miaka 10 kuanzia mwaka jana na itaangalia jinsi ya kupanua udhamini wake kadri muda unavyoendela” Dean alisema “Tunakaribisha wadhamini wengine kushirikiana na ZIFF na matumaini yetu ni kwamba wadhamini wataweza kufaidika kutokana na ushirikiano huu kwani ni nguzo ya masoko ya ubunifu kwa ajili ya wawekezaji na wafanyabiashara ambao wana maono kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na ajira katika sekta zote, hasa utalii na burudani. Kwa kazi ya kukuza sekta ya burudani, ZIFF na Makampuni shiriki yatasaidia kujenga ajira kwa watengenezaji wa filamu, wazalishaji na watendaji katika kanda nzima.” Tamasha la ZIFF hupokea wageni zaidi ya 6000 toka nje kila mwaka na zaidi ya watu 45,000 wakati likiendelea Zanzibar.

0 comments:
Post a Comment