Sauti za Busara inaleta watu pamoja, licha ya kwamba kuna tamaduni tofauti, siasa na dini, lakini kupitia muziki unaondosha mipaka iliyopo.
 
Mkurugenzi wa Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud amesema kwamba muziki ndio njia pekee ya kujenga au kuleta amani. “Nafikiri umoja kwa Waafrika ni lazima, na kujenga umoja kwa Afrika ni kitu cha lazima, lakini ni rahisi katika kiwango cha mtu na mtu, kuliko katika tasnia ya siasa”. Alisema Mahmoud. Aidha Bwana Mahmoud anaamini kwamba hali hiyo imepelekea kusaidia Busara Promotion kuandaa ratiba ya kuonesha filamu ambazo zitafikisha ujumbe wa umoja na mshikamano kwa Waafrika kwa sauti na kueleweka. “Kwa kuwaleta watu pamoja kusheherekea katika tukio linaloheshimu mchanganyiko wa tamaduni na uhuru kwa kujieleza, lakini pia Sauti za Busara inasaidia kuleta demokrasia na uwazi,.kwa lengo la kuinua jamii. Naamini kwamba tamasha la Suti za Busara lina jukumu la kulinda au kuendeleza amani na umoja Zanzibar, kukuza uelewa wa muingiliano wa tamaduni na kuuheshimu”. Alisema Mahmoud.
Mwaka huu tamasha la Sauti za Busara linaleta watu pamoja kwa muda wa siku tatu katika kufurahia filamu ndefu zinazohusiana na muziki wa Afrika. Filamu hizo ni ‘Omar Sosa's Souvenirs from Africa’, ‘Benda Bilili!’, and ‘United States of Africa: Beyond Hip Hop’. Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions Bi. Rebecca Corey amesema filamu zote tatu zinatoa nafasi nyingine kwa watazamaji kuona thamani ya utajiri na mchanganyiko wa muziki wa Afrika, na kuchangia kuwapo kwa mabadiliko chanya katika jamii ambayo ni urithi katika muziki. “ Filamu tatu za mafunzo zilizochaguliwa mwaka huu zinahusu aina tofauti za muziki, ikiwemo Jazz, Rumba ya Congo na Hip hop, lakini zote kwa pamoja zina maudhui yanayofanana. Ambapo ujumbe katika muziki unaodosha mipaka, unajenga amani na mazungumzo, na unasisitiza utu wa mtu”. Alisema Corey.

Nae Mkurugenzi wa tamasha Ndugu Mahmoud, amesema kwamba wamekuwa wakifanyakazi kwa upana na kuangalia mahitaji ya watu, huku wakiendeleza muziki, pia kuheshimu dini na tamaduni. Amesema atahakikisha kwamba muziki haupigwi wakati wa sala, na wasanii wote wamesaini mikataba ambayo inawataka kuvaa vivazi vya heshima na kutokwenda kinyume na maadili ya wazanzibar. Kwa upande mwingine alipatwa na mshangao anapofikiri hali aliyoiona nchini Mali, kumekuwa na kutoheshimu wanamuziki kwa muda mrefu. Mahmoud amesema anajisikia vibaya kuona msanii kama Khaira Arby, ambae atafanya onesho katika tamasha la mwaka huu akiwa anasumbuliwa na kutothaminiwa nchuni mwake.


Mahmoud amesema Busara Promotions imekuwa akikumbana na changamoto katika masuala ya udhibiti, kutokana na baadhi ya viongozi wa siasa wakiwa hawafurahii baadhi ya maonesho ya wasanii kama Comrade Fasto kutoka Zimbabwe na Didier Awadi kutoka Senegal. Wasanii hawa wamekuwa wakizungumzia masuala ya rushwa katika siasa na kutokuwepo kwa haki. Sauti za Burasa maana yake Sound of Wisdom, kwa hiyo tunaona ni jukumu letu kuandaa jukwaa kwa wasanii kama hawa ambao wanatoa ujumbe muhimu unaogusa na kuingia katika mioyo ya watu, na ni tofauti na siasa.


0 comments:

 
Top