Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambae pia ni Rais wa Jamuhuri Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wamewaasa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kujishirikisha zaidi katika masuala ya kujenga Nchi ili kuleta faida iliyokusudiwa ndani ya Jamii ya Watanzania.

Dr. Kikwete ametoa nasaha hizo wakati akiifunguwa Semina Maalum ya Wajumbe wa Halmashauru Kuu ya Taifa ya CCM ambao baadae wanakutana katika kikao chao cha Pili tokea kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Hicho mwisho mwa mwaka jana.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa aliwaambia Wajumbe hao wa NEC hapo Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma kwamba tabia ya baadhi ya Viongozi ndani ya Chama kuendeleza Makundi waelewe kuwa wanasimamia kujenga migogoro baina yao pamoja na wale wanaowaongoza.

Dr. Kikwete alifahamisha kwamba Ilani ya CCM ndio iliyokubalika kwa wananachi walio wengi na kupata ridhaa ya kuunda Serikali. Hivyo Viongozi wa Chama hicho hasa Wajumbe wa Nec wafahamu kwamba wana jumuku la kusimamia itekelezaji wa Ilani ya CCM Katika maeneo yao.

Alitahadharia kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi kuwa na mawazo ya kuendeleza makundi kwa maslahi yao binafsi ambayo kama haikudhibitiwa inaweza kuleta athari hapo baadaye.

“ Unapompendekeza mtu achaguliwe kuwa Kiongozi lakini bahati mbaya akakosa fursa hiyo inakuwa ndio mwanzo wa muelekeo wa magenge ndani ya Chama”. Alitahadharisha Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa Dr. Kikwete.

Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliwakumbusha Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kwamba kuelewa kwamba wao ndio wasimamizi wakuu katika kutanzua matatizo yanayowakumba Wananachi na Wanachama katika maeneo yao.

Alihafamisha kwamba Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika utekelezaji wake ndani ya Serikali zote mbili usimamizi itafikiwa iwapo Wajumbe wa NEC watakuwa makini katika usimamizi huo.

Semina hiyo ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imejumuisha mada nne ambazo ni Nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu katika Uongozi pamoja na Maadili ya Viongozi.

Nyengine ni mjadala wa Maazimio ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita pamoja na mkakati wa kukuza ajira Nchini ambalo limo ndani ya ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Othman Khamis Ame


Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top