Zanzibar
itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba kutokana na
Historia ya muda mrefu kati ya Mataifa hayo mawili rafiki tokea
Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa
kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Watu
wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Ernesto Gomez Diaz aliyefika Nyumbani
kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kumuaga baada ya kumalizika muda wake wa utumishi hapa Tanzania.
Balozi
Seif alisema Wananchi wa Zanzibar kwa muda mrefu wameshuhudia juhudi
kubwa za Cuba katika kuunga mkono Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa
Wananchi wa Zanzibar .
Aliitaja
Sekta ya Afya Zanzibar kuwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopata fursa ya
kuimarika Kitaalamu na utendaji kufuatia Mpango wa Wataalamu Mabingwa wa
Afya wa Cuba kuwafundisha Madaktari wazalendo hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi wa Cuba kwamba Mpango huo unaonyesha ishara njema ya kupata Wataalamu Wazalendo wanaotarajiwa kutoa huduma za Afya mara wamalizapo mafunzo yao.
“
Kwa muda mrefu tulikuwa tukishuhudia Vijana wetu wengi wanaopata fursa
za masomo ya Juu nje ya Nchi hutoweka mara wamalizapo masomo yao bila ya
kujali kuwa wanaitia hasara Nchi yao kwa tamaa ya maisha mazuri zaidi”. Alifafanua Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Balozi Ernesto Gomez Diaz kwa
juhudi zake za kuendelea kuunganisha nguvu ya uhusiano uliopo kati ya
Zanzibar na Cuba.
Balozi
Seif alimuahidi Bwana Ernesto Gomez kwamba Wazanzibari watahakikisha
wanaendeleza mazuri yote aliyoyaacha Balozi huyo kwa kuyafanyia kazi.
Aidha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuomba Bwana Ernesto kuwa Balozi
mpya wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla atakaporejea nyumbani kwa kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo Nchini ili Wawekezaji wa Cuba wapate fursa ya kuweka Vitega Uchumi vyao hapa Nchini.
Mapema
Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba aliyemaliza muda wake Nchini
Tanzania Bwana Ernesto Gomez Diaz alielezea matumaini yake kwamba Mpango
wa kufundisha Madaktari Wazalendo chini ya usimamizi wa Madaktari
Mabingwa wa Cuba utasaidia kupunguza uhaba wa Madaktari Zanzibar.
Bwana
Ernesto alisema katika kuimarisha uhusiano wa pande hizo mbili Cuba
inakusudia kuongeza fursa za masomo kwa Vijana wa Kitanzania hatua
ambayo hata Zanzibar itafaidika na Mpango huo.
Halkadhalika
Balozi Ernesto alisema Zanzibar bado ina fursa kubwa ya kujifunza
kutoka Cuba katika Nyanja za Uvuvi, Utalii na Biashara kwa vile nchi
hiyo tayari imeshapiga hatua kubwa za Kimaendeleo katika sekta hizo zilizoinyanyua Kiuchumi Nchi hiyo.
Aliupongeza ukarimu wa Watanzania uliomsaidia kumuwezesha kutekeleza majukumu yake hapa Tanzania kwa ufanisi zaidi .
Bwana Ernesto Gomez Diaz amemaliza muda wake wa utumishi wa
Kidiplomasia Nchini Tanzania na anarejea Nyumbani Oktoba Mbili mwaka
huu wa 2012 kwenda kupangiwa majukumu mengine katika Taifa lake.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment