Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema sifa sahihi watakayoendelea kupewa Wazazi popote pale itapatikana endapo jukumu la kuwalea Watoto wao watalipa kipaumbele kinachostahiki.
Balozi Seif ambaye pia ni Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba mfumo wa utandawazi wa Dunia uliopo hivi sasa umechangia kuathiri malezi bora ya Vijana ndani ya Jamii licha ya kwamba upande mmoja unaelimisha.
Akiufungua
Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja hapo ukumbi
wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope Balozi Seif alisema Jumuiya hiyo hivi sasa ina kazi nzito ya malezi ya Vijana kutokana na mfumo huo wa Utandawazi.
Balozi
Seif alionya kwamba baadhi ya Wazazi Nchini wanahusika katika janga la
upotofu wa maadili kwa Vijana kutokana na kuwaridhia Watoto wao
kupindukia na matokeo yake Watoto hao kukosa Heshima kwa kiwango cha
kutisha.
“
Utandawazi kwa kiasi kikubwa umeharibu mfumo wa malezi na kupelekea
baadhi ya watoto kuwaita Baba zao Madingi wakati Mama wakiwaita Mom.
Sasa tunakwenaa wapi?”. Aliuliza Balozi Seif Ali Iddi.
“
U dot. Com wao walioubeba Vijana hvivi sasa unawaharibia maadili yao.
Sasa watoto wetu Heshima zao zimepungua kutokana na utandawazi
ulituharibia mfumo wetu wa malezi”. Alieleza Balozi Seif Ali Iddi.
Alisema
Wanajumuiya hiyo ya Wazazi lazima wawadhihirishie Wananchi, CCM na
Vijana wote kwamba Jumuiya hiyo ina nguvu kwa vile inabeba watu wa rika
zote katika Jamii inayowazunguuka.
Balozi
Seif amewashauri Viongozi wapya watakaochaguliwa katika Mkutano huo
kukubali kubeba dhamana ya kuwa Waaminifu, Waadilifu na upendo ili
kuisaidia Serikali Kuu kwa wao ndio walezi katika kutoa Elimu kwa
Watoto.
“ Chagua Kiongozi unaeamini
kwamba ni mahiri na madhubuti ambaye atakuwa na nguvu na ubunifu katika
kuiwezesha Jumuiya bau Jamii kupata mapato yake bila ya kutegemea mwega
mwengine”. Alisisitiza Balozi Seif.
Akizungumzia
suala la amani Balozi Seif aliitaka Jamii kupiga vita dalili zote
zinazoashiria kuvurugika kwa Amani ambayo ikitoweka hakutakuwa na wakati
wa kujenga Uchumi wa Taifa.
Aliwakumbusha Viongozi wa Jumuiya hiyo ya Wazazi pamoja na Wana CCM kuendelea kuisimamia Amani iliyopo Nchini kama Ilani ya Chama hicho Ibara ya 168 ilivyoelekeza kusimia amani ya Nchi.
“
Kuna watu wanataka kutuondoshea amani yetu tuliyonayo kwa karne kadhaa
zilizopita. Hili ni jukumu letu. Hivyo tunapaswa kupambana na wote
wanaotaka kutuvurugia amani yetu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliwakumbusha
Wana CCM wote kuendelea kutetea sera na Ilani za Chama chao kwa wazi
bila ya kificho kwa vile wanaziamini na walishiriki katika
kuzitengeneza.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM liwapongeza
Viongozi wote waliochanguliwa kuanzia ngazi ya shina hadi Wilaya na
kuridhika na chaguzi hizo zilizokwenda kwa amani na utulivu.
Mapema Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Nd. Mussa Ame
Silima alisema Jumuiya ya Wazazi inaendelea kufanya chaguzi zake katika
ngazi mbali mbali sambamba na Jumuiya nyengine kutokana na mabadiliko ya
ngazi za juu ya CCM.
Ndugu
Mussa alisema Jumuiya ya wazazi sasa italazimika kufanya chaguzi zake
katika kipindi cha kila baada ya miaka mitano badala ya miaka mine
iliyokuwa ikifanya hapo kabla.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment