Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE linatarajia
kufanyika kuanzia tarehe 18 – 20 ya mwezi wa kumi 2012 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam.
TWENDE imekuwa ikifanyika
kila mwaka kwa mwaka watatu sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010, lengo
likiwa ni kuwaleta pamoja wanawake wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale
wanaochipukia ili kupata fursa ya kuuza, kuonesha na kujadili masuala ya
biashara kwa ujumla.
Sambamba
na hilo. TWENDE inalenga kusaidiana na serikali katika kutimiza malengo ya
milenia likiwemo lengo namba moja ambalo linalenga kuondoa umasikini, namba tatu
kutetea haki na fursa sawa kwa wanawake, lengo namba tano kuhamasisha afya ya
uzazi na lengo namba nane, ambayo ni kuendeleza uhusiano wa kudumu kwa ajili ya
maendeleo ya jamii. Pia TWENDE inalenga Kukuza uzalishaji kwa wanawake
wafanyabiashara na kukuza mgawanyiko wa masoko sambamba na muonekano wa
wafanyabiashara wanawake katika jamii.
Kwa upande wa mwaka huu TWENDE inatarajia kuwashirikisha wanawake
wajasiriamali wengi zaidi ambao wamekuwa wakifanya biashasha tofauti ili kuweza
kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi zaidi kibiashara.
Sambamba na semina bora zitakazotolewa kwa wanawake wote ambao watapata elimu
itakayotolewa wataalamu wa fani mbalimbali
Kwa miaka mitatu mfululizo TWENDE imekuwa ikitoa fursa
kwa wanawake wajasiriamali kukutana pamoja na kujadili mafanikio na changamoto
ambazo zimekuwa ni kikwazo cha wanawake wajasiriamali kutofikia malengo yao
kibiashara.
“Licha ya kwamba wanawake wengi wamejikita katika sekta
hii ya ujasiriamali, lakini bado wamekuwa wakikabiliawa na changamoto
mbalimbali zinazokwamisha kufikia malengo yao, ikiwemo elimu ya ujasiriamli na
upatikanaji wa mikopo, kwa hiyo ipo haja kwa wanawake kujijengea utaratibu wa
kushiriki katika fursa kama hizi zinazowajengea uwezo”. Alisema Saphia Ngalapi
Meneja Mradi wa TWENDE.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali Wanawake 100 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatarajai kushiriki katika
TWENDE mwaka huu, ampabo maonesho hayo yanakwenda sambamba na semina zitakazo
tolewa kwa wanawake wote bure, kwa wale watakaoshiriki katika maonesho, na hata
wale ambo watakuwa hawakupata frusa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao.
KUHUSU TWENDE
Tanzania Women Entrepreneurs
& Networking Development Exposition (TWENDE) inapanga kuleta maendeleo kwa
wanawake wajasiriamali kwa kuandaa jukwaa ambalo litakua mahususi kuweza
kukutana zaidi ya wanawake wafanyabiashara 100 wadogo, wakati na wakubwa kutoka
viwanda vikubwa na vidogo, taasisi za serikali na mashirika yasio ya kiserikali
(NGO).
Tanzania Women Entrepreneurs
& Networking Development Exposition (TWENDE) pia inalenga kuyapa fursa
makampuni kukutana yakikidhi malengo ya wahudhuriaji. Ni sehemu ya kuuza na
kuonyesha bidhaa na huduma za kampuni mbalimbali kwa wafanya maamuzi. Maonyesho
haya yataenda sambamba na mkutano wa siku tatu utakaotoa elimu bora kwa
washiriki. Kwa habari zaidi tembelea www.twende.info
0 comments:
Post a Comment