Kufuatia vurugu zinazodaiwa kufanywa na vijana wa UAMSHO kwenye kisiwa cha Unguja, jumla ya watu arubaini na tisa (49) na wanane (8) kati ya hao tayari wameshafikishwa mahkamani kwa ajili ya kusikiliza mashataka yao.
Hayo yameelezwa na Kamisha wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, wakati akiongoea na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Polisi hapa visiwani.
Aidha Kamishana Mussa alieleza kwamba mara abaada ya kupokea taarifa za kupotea kwa Sheikh Faridi Hadi, jeshi la polisi limefanya juhudi kuwamba za kutafuta taarifa za habari ya kupokea kwa kiongozi huyo wa Mwamsho, ikiwa ni pamoja na kufika kwenye sehemu ya makaburi ambayo yalikuwa nje kidogo ya mji wa Zanzibar kwenye kijiji cha Bumbwini.
Kamishina Mussa alifahamisha kwamba katika hali isyo ya kawaida mnamo tarehe 19.10.2012 majira ya usiku Sheikh Faridi alizuka ghafla na kuoneka akiwa katika eneo hilo hilo la Mazizini ambapo ndipo  alipopotelea na sasa yupo katika hali nzuri kiafya.
Hata hivyo,Kamishana Mussa alisema
“ Jeshi la Polisi sasa hivi linawahoji Sheikh Farid na viongozi wenzake wa jumuiya ya UAMSHO ili kufahamu wapi alipokuwa na kuthibitisha kama kweli alitekwa ama la” alisema Kamishana.
Sambamba na hilo kama kwenye mahojiano hayo yanaweza kuonyesha dalili au ishara yoyote ya vitendo vya jinai ambavyo vimefanywa na makundi ya vijana ya kuharibu mali za ummah Sheikh Faridi na viongozi wenzake wa UAMSHO watakuwa na kesi ya kujibu.
Kamishina Mussa alifahamisha kwamba vyomba vyote vya Ulinzi na Usalama pamoja na Jeshi la Polisi havikuhusika katika suala zima la utekeji wa Sheikh Farid na kuahidi kwamba jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kiwana juu ya suala hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limepelekea uvunjifu wa amani kwenye kisiwa cha Unguja.
“ Tunazo taarifa za uhakika kuwa wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO wamepanga kuvamia kambi za Polisi, Jeshi pamoja na Afisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kama kiongozi wao huyo ataendelea kukamatwa, natoa onyo kali kwa wananchi wote kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, Jeshi la Polisi na Vikosi vyote vya ulinzi na Usalama tumejipanga madhubuti kukabiliana na mtu yoyote ama kikundi chochote kitakachothubutu kuanzisha ama kuendeleza vurugu za aina yoyote kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani nchini” alisema Kamishina Mussa.
Akifafanua kuhusu vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-20 ambapo wamekuwa wakijihusisha na makundi ambayo kwa kiasi kikubwa ndio wanaochangia vurugu, alisema
“tutapambana kwa nguvu zetu na kwa gharama zozote ili kuhakisha kwamba amani na utulivu vinalindwa ipasvya, nawaombeni wananchi wema waonyeni watoto wenu, ndugu zenu na hata jamaa zenu wasishiriki kwa njia yoyote ile katika vitendo vya uvunifu wa amani: alisema Kamishana Mussa.
Wakati huo huo Kamisha Mussa alieleza kwamba kufuatia vurumai hizo ambazo zilipelekea kuuwawa kwa askari CPL Said Abdulrahaman mwnye namba F.2105 jumla ya watu sita wamekamatwa katika mazingira tofauti ambapo watu watatu (3) walikamatwa Tanga ambapo likimbilia huko, mmoja (1) alikamatwa kisiwa cha Unguja kwenye mazingira ya kawaida, wa pili (2) alikamatwa kisiwa cha Tumbatu na wa tatu (3)  alikamatwa kwenye afisi za Uhamiaji Unguja.

0 comments:

 
Top