Muanzilishi wa Mradi wa Taa
zinazotumia mwanga wa Jua kutoka Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi Bwanan
Maurits Groen akimkabidhi Taa inayotumia mwanga wa jua mmoja wa wananchi kadhaa
wa Vijiji vya Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo la Kitope
Kampuni inayojishughulisha na mradi
wa Umeme unaotumia Jua {Solar Energy } yenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi
ya Wakawaka imetoa msaada wa Taa Mia Nne zinazotumia nguvu za mwanga wa jua kwa
Vijiji viwili vya Matetema na Kichungwani vilivyomo ndani ya Jimbo la Kitope
Wilaya ya Kaskazini B.
Halfa ya ugawaji wa
Taa hizo imesimamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya
Wakawaka Bwana Bill Carney ambapo jumla ya Nyumba 86 za Kijiji cha Matetema na
160 za Kijiji cha Kichungwani zilipata mgao wa Taa moja kwa kila nyumba.
Jumla ya shilingi Milioni 25,000,000/-
zimetumika kutengenezea Taa hizo
mia Nne zitakazosaidia kupunguza matumizi makubwa ya Taa za Vibatari zinazotumia Mafuta ambapo
kila taa moja ina Thamani ya Shilingi
Sitini elfu {60,000/- }.
Akizungumza
na Wananchi wa Vijiji hivyo vya Matetema na Kichungwani kwa nyakati tofauti Muanzilishi wa Mradi huo wa
Taa zinazotumia mwanga wa Jua kutoka Kampuni ya Wakawaka Bwana Maurits Groen
alisema Kampuni yao imeamua kuanzisha mradi huo kwa lengo la kusaidia Jamii
yenye kipato cha Chini katika Mataifa mbali mbali Duniani.Bwana Maurits alisema Jamii kubwa hasa katika Mataifa maskini zimekuwa
zikitumia gharama kubwa kwa ununuzi wa mafuta kwa ajili ya matumizi ya Taa
jambo ambalo linawaongezea mgizo wa matumizi wakati kipato chao ni hafifu.
Alisema pia yapo matatizo ya
uchafuzi wa mazingira pamoja na ajali za mara kwa mara za moto zinazosababishwa
na matumizi makubwa ya Taa za Vibatari ambazo huleta athari na wakati mwengine
maafa kutuokana na Taa hizo. Naye Mbunge wa
Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Mampuni hiyo ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi kwa uamuzi
wake wa kusaidia Wananchi wa Jimbo la Kitope katika kujipatia huduma za Taa zinazotumia
mwanga wa Jua.
Balozi Seif
ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Taa hizo kwa kiasi
kikubwa zitaweza kusaidia matumizi mbali mbali majumbani likiwemo lile muhimu
la wanafunzi kupata wasaa wa kudurumu
masomo yao.Alisema kwa
Vile Tanzania na Zanzibar kwa ujumla zimebahatika kuwa na kipindi kirefu cha Jua
ndani ya mzunguuko wa mwaka wa miongo yake Taa hizo zitakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa kadri
ya lengo lililokusudiwa la kuanzishwa
kwa mradi huo.
“ Haya ni maendeleo ya kuachana na Taa za Vibatari kwa vile tayari
tumeshakuwa na Taa isiyohitaji mafuta ambayo ni gharama na yanachafua
mazingira”. Alisema Balozi Seif.
Mradi huo wa
Kampuni ya Wakawaka wa Taa zinazotumia
mwanga wa Jua ni wa mwanzo kuingia ndani ya Bara la Afrika ukiwa
ni wa majaribio.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Kitope akiambatana na Ujumbe wa Uongozi wa Kampuni
hiyo ya Wakawaka inayosimamia mradi wa Taa zinazotumia mwanga wa Jua walipata
fursa ya Kuangaliwa Umeme unaotumia jua kwa baadhi ya Nyumba na Msikiti uliopo
katika Kijiji hicho cha Kichungwani.
Muanzilishi wa Mradi wa Taa
hizo Bwana Maurits Groen alimueleza Balozi Seif kwamba Kampuni yake ina uwezo
wa kila hali kutengeneza Vifaa vya Umeme unaotumia mwanga wa jua.
Othman Khamis Ame
Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment