Mwandishi maalum, UAE.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na uongozi wa shirika la misaada la mwezi mwekundu kuzungumzia masuala mbali mbali yakiwemo ya kuipatia misaada Zanzibar.
Viongozi hao ambao wamekutana mjini Abudhabi katika falme za nchi za kiarabu UAE, wameahidi kuendeleza ushirikiano  na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na UAE.
Katibu Mkuu  wa shirika hilo Dr. Mohd Ateeq Al Falahi, amemuahidi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kuwa Shirika hilo la kimataifa la Red Crescent, litaendeleza misaada yake kwa Zanzibar na nchi nyengine duniani.
Shirika hilo limekuwa likijishughulisha na utoaji wa misaada kwa nchi mbali mbali dunia ikiwemo misaada katika sekta za elimu na afya.
Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa kurejea nchini kesho baada ya kumaliza ziara yake ya wiki mbili nchini Marekani na Uingereza.

0 comments:

 
Top