Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kimataifa ya Lagema iliyoko katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ulikuwa na burdani ya aina yake kufuatia Kikundi cha Muziki wa Taarab cha Wanawake cha { Tausi Women Taarab } kutumbuiza wakati wa Tafrija Maalum aliyoandaliwa Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Hui Liangyu na Ujumbe wake.
Bwana Hui na Ujumbe wake akiwa sambamba na mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwepo Zanzibar kwa ziara ya kiserikali ya Siku mbili.
Ule utamaduni na silka ya Waswahili ya kutoa tunza kwa mtu au kikundi kinapofanya vizuri au kufurahisha ilianikiza ndani ya Ukumbi huo wa Lagema.
Naibu waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Hui Liangyu na mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  walishindwa kukaa kwenye viti vyao wakati Kikudi hicho kikiendelea kutoa burdani hiyo.
Balozi Mdogo wa China aliyepo hapa Zanzibar Bibi Chen Qiman aliwa sambamba na Msanii Sharifa wa Kikundi hicho cha Tausi walionekana kuanikiza ukumbini hapo huku wageni na wenyeji walioshuhudia wakifurahia utamu huo wa aina ya pekee.
Nyimbo mchanganyiko za Kiswahili na zile za Kichina ziliimbwa zikizoongozwa na Bwana Han Xu wa Wizara ya Mifugo ya China aliyekuwemo kwenye Ujumbe huo akionyesha umahiri wake wa kuimba licha ya kwamba yeye ni mwana mifugo.
Furaha hiyo ya aina yake ya Chakula cha usiku imekuja kufuatia Ujumbe huo wa China Ukioongozwa na Naibu Waziri Mkuu wake Bwana  Hui Liangyu kumaliza ulitaji saini mashirikiano na Zanzibar katika masuala ya  Uchumi na Ufundi.
Mkataba huo umeleta faraja kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kupatiwa jumla ya RMB Milioni Sitini sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 14.8.
Feha hizo zinatarajiwa kutumika katika Miradi ya Utengenezaji mkubwa wa Jengo la Hospitali ya Abdulla Mzee iliyoko Mkoani Pemba, Ujenzi wa Majengo mengine pamoja na Vifaa vyake katika Hospitali hiyo.
Pia Ujenzi wa Skuli katika eneo na Mwanakwerekwe ambayo tayari Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauzindua ujenzi wake pamoja na utiaji wa Taa za bara barani zinazotumia nishati ya jua katika bara bara kuu za Mjini Zanzibar.
Fedha hizo halkadhalika zitatumika pia katika utoaji wa mafunzo  mafupi na marefu katika fani tofauti ambazo zitapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo pia uchimbaji wa Visima vya maji na maeneo mengine  ambayo yatakubalika kwa pande hizo mbili.
Kikundi hicho cha Tausi Women Taarab chenye mvuto wa aina yake unaopelekea kupata mialiko katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya visiwa vya Zanzibar kinaogozwa na Gwiji la Habari Nchini Bibi Maryam Hamdan.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top