Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameondoka nchini leo kuelekea nchini Marekani na Uingereza kwa ziara ya kikazi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,
Maalim Seif ataanza ziara yake mjini North Caroline Marekani, ambako
atahudhuria mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na taasisi ya National
Democratic Institute, inayoshughulikia masuala ya kukuza demorasia
ulimwenguni.
Makamu
wa Kwanza wa Rais amekuwa na uhusiano wa muda mrefu na taasisi hiyo,
akiwa katika jitihada za kupigania demokrasia nchini Tanzania na
ulimwenguni kwa ujumla, katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili
iliyopita.
Katika ziara hiyo Maalim Seif anatarajiwa
kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa serikali za
Marekani na Uingereza, pamoja na viongozi wa taasisi zinazoshughulikia
sera za mahusiano ya kimataifa.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais
ameagwa na viongozi na watendaji mbali mbali wa serikali wakiwemo Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib
Fereji, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillahi Jihadi Hassan na Waziri
wa Afya Mhe. Juma Duni Haji.
Hassan Hamad (OMKR).
0 comments:
Post a Comment