Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM
Balozi Seif Ali Iddi amewaomba Wanachama wa Chama hicho ambao tayari
wameshaamua kwenda tofauti na sera za chama hicho katika mfumo wa muundo wa
Muungano ni vyema wakakiacha chama hicho kwa heshima na Taadhima.
Balozi Seif akiwa pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope
ametoa ombi hilo wakati akiufungua mkutano Mkuu wa uchaguzi wa CCM Jimbo
la Kitope uliofanyika katika Ofisi ya
Jimbo hilo iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini B.
Balozi seifg alisema
wakati umefika kwa wanachama wa CCM wasiozikubali sera za chama hicho
ambazo zimepata ridhaa ya Wananchi waliowengi kuongoza Nchi hii itapendeza kama watarejesha kadi za chama hicho mara moja.
Aliwataka Wanachama wa chama cha Mapinduzi kujizatiti
katika kuhakikisha Nchi inaendelea kubakia kuwa ya amani na salama muda wote.
“ Wale wanaotaka kutuvurugia chama chetu na Muungano
wetu waturejeshee kadi zetu. Kwa nini wanachama haio wanasubiri mpaka
wajadiliwe kwenye Vikao vya chama au
vile vikao vya maadili? Ya nini kutuvurugia chama chetu wakati nafasi za
kung’atuka ipo wazi? Aliuliza Balozi Seif.
Alisema Taifa hivi sasa klinapita katika kipindi
kigumu kutokana na baadhi ya vikundi kujaribu kushawushi wananchi na hasa
Vijana kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani.
Aidha alieleza kwamba Wanachama hao hawana budi
kufikiria kupanga safu makini itakayoendeleza na kusimamia vyema uendeshaji wa
chama pamoja na taifa kwa ujumla.
Balozi Seif alitahadharisha kwamba hivi sasa jamii
inashuhudia matusi ya nguoni yanayoendelezwa na baadhi ya maundi ya watu dhidi
ya Viongozi wa Serikali na Chama hali ambayo kama
Jamii hiyo haitakuwa makini Taifa linaweza kutumbukia katika fujo na hatimae
maangamizi.
“ Tunakotoka kubaya sote ni mashahidi, kwa sababu
familia na hata ndugu wa karibu walikuwa hawaulizani hali na hata maziko
hawaendeani. Kwa kweli tusifikie tabia hii kuiruhusu irejee tena”. Alifafanua
Balozi Seif.
Alisisitiza kwamba Chama cha Mapinduzi kitaendelea
kuunga mkono mfumo wa uongozi wa Serikali mbili nchini Tnaznia na kuamini
kwamba Mwanachama ye yote wa chama hicho
anayejiamini ataunga mkono mfumo huo.
Akizungumzia ujenzi na uimarishaji wa majengo ya
Matawi ya chama Balozi Seif alieleza kuwa mkazo utaendelea kuwekwa ili
kukamilisha matawi matatu yaliyobakia ndani ya Jimbo hilo kati ya matawi yote 20.
Alisema hatua hiyo imelenga kwenda sambamba na mfumo
wa chama cha Mapinduzi ya kuwa na Ofisi zenye hadhi inayokubalika.
Akitoa Taarifa
ya utekelezaji wa chama katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Katibu
wa CCM Jimbo la Kitope Nd. Khamis Khamis alisema uongozi wa chama hicho
umejipangia kuongeza idadi ya wanachama watatu kwa kila shina.
Nd. Khamis alisema hatua hiyo inalenga zaidi
kuimarisha nguvu na uhai wa chama katika utekelezaji wa sera na ilani zake.
Katika mkutano huo wajumbe hao wamemchagua Ndugu Zamir
Makame kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jimbo la Kitope, Katibu ni Nd. Khami Khamis,
Katibu Mwenezi ni Nd.Hamisa Yussuf na Uchumi na Fedha ni Nd.Juma Fadhil.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ni Ndugu
Hilika Fadhil, Nd. Asha Suleiman,Maryam Haji naMwinyi Mahfoudh. Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Mkoa ni Nd. Ali Ameir, Ali Khamis na Nd.Juma Makame.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya n Nd. Abdulla Seif,
Nd, Maryam Haji, Nd.Christina Benjamin, Nd. Ali Haji na Nd. AbdullaVuai.
Wajumbe wa Halmashauri ya Jimbo ni Nd. Asha Suleiman,
Nd. Hilika Fadhil, Nd. Hamisa Taufiq, Nd. Mwinyi Mahfoudh na Nd. Maryam Haji.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment