Kikosi cha zima moto na uokozi kimefanikiwa kuuzima moto uliotokea katika jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii liliopo Kilimani Mjini Zanzibar.
Chanzo cha Moto huo kimesababishwa na hitilafu za umeme uuliotokea majira ya saa nne na nusu za asubuhi .
Mmoja wa wafanyakazi wa usafishaji wa Jengo hilo nd. Vuai Haji aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hitilafui hiyo imetokea katika Chumba cha iliyokuwa afisi ya bodi ya mapato Zanzibar ZRB cha mtandao wa Kompyuta.
Usafishaji huo umekuja kufutia watendaji wa bodi hiyo kuhama na kujitayarisha kukabidhi ofisi hiyo kwa uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hapo kesho.
Msaidizi Kamishna wa Kikosi cha zima moto na uokozi Kamanda Simai Ame Simai amesema watedaji wake wamelazimika kuvunja vioo vya dirisha la Ofisi hiyo kwa lengo la kuzima moto ili kunusuru kuzagaa kwa maafa zaidi.
Kamanda Simai ametoa wito kwa jamii kutoa Taarifa za haraka pale yanapotokezea matukio kama hayo ili waweze kupata huduma za haraka na uhakika.  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika eneo hilo kujionea hali halisi ya tukio hilo.
Akizungumza na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Balozi Seif ameagiza kutolewa kwa Elimu ya Huduma za mwanzo ya kukabiliana na maafa kwa wafanyakazi wa Ofisi na Taasisi za Umma.
Balozi Seif alisisitiza pia kufuata utaratibu wa kuzimwa kwa mashine zote za umeme wakati wanapomaliza shughuli zao za kikazi. Hadi sasa bado haijajuilikana hasara iliyopatikana kutokana na moto huo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu w Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top