Makamu wa apili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Kiongozi wa Wakristo wa madhehebu ya Optic Nchini Misri Pope Shenouda 111 hapo Ubalozi mdogo wa Misri uliopo Vuga Mjini Zanzibar.
 Waumini wa Dini ya Kikristo wa Madhehebu wa Coptic Orthodox Church Nchini Misri wanaendelea na Maombolezo kufuatia kifo cha Kiongozi wao Pope Shenouda  wa tatu.
Pope Shenouda amefariki Dunia usiku wa Jumamosi ya Tarehe 17 Mach mwaka huu Nchini Misri Taifa lenye Waumini wa Dhehebu hilo la Coptic wapatao Milioni nane.
Hapa Zanzibar Viongozi na  makundi ya Waumini wa madhehebu tofauti wamekuwa wakiweka saini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Misri uliopo Vuga Mjini Zanzibar kufuatia kifo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alikuwa miongozi mwa watu mbali mbali walioweka saini kitabu hicho cha Maombolezo ya Popa Shenouda 111 Nchini Misri.
Akitoa salamu zake ya rambi rambi kufuatia  kifo hicho Balozi Seif  alimuomba Balozi Mdogo wa Misri aliyepo Zanzibar Bw. Walid Ismail pamoja na Waumini wa Dini hiyo Nchini Misri kuwa na moyo wa subra  kutoklana na msiba huo mzito.
Naye Balozi Mdogo wa Misri aliyepo hapa Zanzibar Bwana Walid Ismail  alieleza faraja yake kutokana na Wananchi wa Zanzibar kuguswa kwao na msiba huo.
Pope Shenouda 111 amezaliwa tarehe 3 Agosti mwaka 1923 katika Mji wa Alexadria Nchini Misri na kupata elimu ya msingi, Sekondari hadi chuo Kikuu katika fani ya Historia.
Ametumikia wadhifa huo wa pope  Wa Alexadria  tokea Tarehe 14 Novemba mwaka 1971 hadi  kufariki kwake  akijihusisha pia  katika masuala ya Uandishi, Ualimu pamoja na kuhamasisha suala la amani miongoni mwa waumini.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top