Zanzibar International Film Festival (ZIFF) imeandaa MINI ZIFF RED CARPET katika ukumbi wa New Maisha Club siku ya Jumapili tarehe 22 Januari 2012. Wasanii mbali mbali maarufu wa filamu za Kitanzania (Bongo Movies), wasanii maarufu wa Bongo Fleva na wadau mbali mbali wa sanaa nchini wataalikwa kupita katika Red Carpet.
Wasanii wote maarufu wa Bongo Movies na Bongo Fleva watahudhuria katika RED CARPET jumapili hii New Maisha Club na baada ya hapo kutakua na onesho maalum ambapo kwa mara ya kwanza ZIFF imeweza kuwaweka wasanii AT na Offside Trick katika jukwaa moja.
MINI ZIFF RED CARPET inaandaliwa kufungua kampeni ya “ Nunua kazi halisi ya msanii wa nyumbani ili kukuza tasnia ya sanaa nchini/Buy Original Product of our Artists to support the Development of Arts in Tanzania". ZIFF imeona umuhimu wa kuanzisha kampeni hii ili kusaidia kusambaza ujumbe huu na uwafikie watanzania wote ambao wengi wao wamekua wakinunua kazi zisizo halisi (Pirated Copies) na hivyo kuwanyima mapato wasanii ambao wamekua wakijitahidi katika kujikwamua kimaisha na kukuza tasnia nzima ya sanaa hapa nchini.
Katika Red Carpet ZIFF itatoa tuzo maalum (Nishani- Medal) kwa Kampuni bora iliyotoa mchango mkubwa kwa sanaa ya filamu Tanzania kwa mwaka 2011, Muigizaji bora wa kiume kwa 2011, mwigizaji Bora wa kike kwa 2011, filamu bora kwa mwaka 2011 na muugizaji bora anayechipukia. Tuzo hizi zitatolewa katika RED CARPET siku hiyo baada ya Kamati maalum (Panel) ya watu kumi watakaoteuliwa kufanya zoezi maalum la kuchagua watakopata tuzo hizo kutokana na kufanya kazi zao vizuri. Kamati (Panel) hiyo itaundwa na wadau wa karibu wa Bongo movies na watatoka katika vitengo au mashirika mbali mbali.
AidhaMINI ZIFF itaendelea Ngome Kongwe Zanzibar tarehe 27 na 28 Januari, 2012, tutaonesha filamu za Kiswahili (Bongo Movies) sita katika screen kubwa ya Amphitheatre kuanzia saa moja usiku na filamu zitakazo oneshwa ni Mr.President ya Steve Nyerere, Big Daddy ya Kanumba, Pamoja ya Pastor Myamba, Dj Ben ya J.B, na filamu mpya toka CL& CY production.
Filamu zitaoneshwa bure siku ya Ijumaa ya tarehe 27, tarehe 28 Jumamosi itaoneshwa filamu moja na kufuatiwa na maonesho ya mavazi kutoka kwa Lucky Creation na Mgece Makory baada ya hapo tamasha hili dogo litafungwa na burudani kutoka kwa AT na Offside Trick kwa kiingilio cha shilingi 3,000/= tu.

0 comments:

 
Top