Wafanyakazi wa Hoteli ya Kitalii ya Palma iliyoko Pwani Mchangani Mkoa Kaskazini Unguja wamepongeza kwa juhudi zao za kutoa huduma bora kwa wageni wanaotembelea Zanzibar Kiutalii.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Tafrija Maalum iliyoandaliwa na Uongozi wa Hoteli hiyo kwa Wafanyakazi wake ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2012.
Balozi Seif alikabidhi zawadi ya Printer ya rangi kwa Mshindi wa shindano Maalum Ndugu Goria Agostina Mtemi la kusherehekea mwaka mpya kwa Wafanyakazi hao lililopewa jina la Rafol
Alisema Watalii na Wageni wengi wamekuwa wakifurahia huduma nzuri zinazoendelea kutolewa kwenye mahotelini mbali mbali hapa Zanzibar.
Balozi Seif alisema ukarimu uliopo miongoni mwa wafanyakazi wa sekta hiyo ya Mahoteli unaashiria kuimarisha kwa sekta ya Utalii Nchini.
Tafrija hiyo Maalum iliyoandaliwa na Uongozi wa Hoteli ya Palm ya pwani Mchangani ilitoa fursa kwa wafanyakazi hao kula , kunywa na kufurahia pamoja mwaka mpya wa 2012.
Othman Khamis Ame
Ofisi yha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top