Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amepongeza maandalizi mazuri yaliyofikiwa katika zoezi zima la Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufikia kilele chake alhamis tarehe 12 januari 2012.
Baloz Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Mapambo Taifa amesema hayo alipokutana na Wajumbe wa Kamati hiyo hapo VIP Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
Amesema Kutokana na Maandalizi hayo ama matumaini kwamba Wananchi na Jamii yote Zanzibar na Tanzania kwa ujumla itaendelea kufurahia sherehe hizo zilizoanza rasmi Tarehe 5 Mwezi huu katika maeneo tofauti Nchini kwa Usafi wa Mazingira.
“ Nategemea kesho mambo yatakuwa mazuri mbele ya wageni wetu ingawa inawezekana zikawepo hitilafu ndogo ndogo lakini hizo tutazijuwa wakati wa kikao cha Tathmini ya Sherehe nzima ”. Alifafanua Balozi Seif.
Balozi seif aliwaagiza Wajumbe wa Kamati zote ndogo ndogo zilizoteuliwa kusimamia mambo mbali mbali kuhakikisha kwamba mapungufu yaliyomo ndani ya uwezo wao yanakamilika kama ilivyopangwa.
Mapemba Balozi Seif na Wajumbe wa Kamati yake waliangalia Mazoezi ya Maandalizi ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama vinavyotarajiwa kunogesha Kilele cha sherehe za Mapinduzi hapo uwanja wa Amani.
Gwaride hilo lililojumuisha Vikosi vya Jwtz, Polisi, Mafunzo, KMKM, JKU, Valantia, na Zima moto vilipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya kamati hiyo ambayo imeridhika na kiwango kilichofikiwa na Vikosi hivyo katika Kuchapa gwaride.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini misri Balozi Mohd Haji Hamza aliyefika kumuaga hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo yake Balozi Seif alimuasa Balozi Hamza kwamba katika uteuzi wake huo atapambana na changamoto ya Mageuzi ya Kisiasa Nchini Misri ambayo atapata fursa ya kujifunza siasa za Kiarabu.
Balozi Seif alisema hata hivyo uhusiano wa Misri na Tanzania bado ni mzuri licha ya mabadiliko hayo na akamuomba atumie busara zake katika kuona ule ushirikiano wa sekta muhimu wa pande hizo mbili unadumishwa.
Naye Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohd Haji Hamza alimuhakikishia Balozi Seif kusimamia vyema majukumu yake aliyopangiwa na Taifa.
Balozi Hamza alisema tayari ameshafanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ambazo zina ukaribu wa uhusiano wa kiutendaji na Misri ili kuona yale yaliyopangwa yanatekelezwa kwa pande zote mbili.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top