Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amepokea mchango wa pole shilingi milioni 20,000,000/- kutoka kwa Uongozi wa Serikali Mkoa wa Mara ili kusaidia Mfuko wa Maafa Zanzibar kufuatia ajali ya Meli ya M.V. Spice Islanders mwezi Septemba mwaka Jana.
Mchango huo amekabidhiwa Balozi Seif na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. John Gabriel Tuppa hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mh. Gabriel alisema Wananchi wa Mkoa wa Mara wamepokea taarifa ya Janga la kuzama kwa meli ya M.V. Spice Islanders katika hali ya mshtuko mkubwa.
Alisema katika kuungana na Wananchi wenzao wa Zanzibar kwenye janga hilo wamefikia maamuzi ya kuchangia kwa lengo la kuwafariji wenzao.
MH. Gabriel ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyochukuwa kwa kupelekea kuokoa idadi kubw ya Wasafiri waliokuwemo kwenye Meli hiyo.
Akiupokea mchango huo wa Maafa Kutoka Mkoa wa Mara Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliushukuru Uongozi wa Mkoa huo kwa haua yao ya kuchangia Mfuko wa Maafa Zanzibar.
Balozi Seif alisem kitendo chao hicho kimeashiria kuguswa kwao na tukio hilo ambalo ni la kihitoria kuwahi kutokea katika Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pia alipokea mchango wa maafa kutoka kwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida.
Mchango huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Singida Nd. Joran Sinid mara baada ya chakula cha Mchana alipokula nao huko katika Hoteli ya Palm Pwani Mchangani Mkoa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif ameelezea furaha yake kutokana na ukaribu uliopo kati ya Wananchi wa Zanzibar na Singida.
Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Singida ulikuwepo Zanzibar kuhudhuria shehere za Mapinduzi ya Zanzibar kutimiamiaka 48 zilizofikia kilele chake katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar kwa mualiko wa Balozi Seif Ali Iddi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment