Akizindua Mpango wa Mikopo kwa Vijana Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozoi Seif Ali Iddi alisema Vijana wanalazimika kufahamu sula hili na ni vyema wakajiandaa kukabiliana nalo.
Balozi Seif alisema suala la kupambana na umaskini ni la kila mtu hivyo hapana budi kujituma kwa bidii huku ikizingatia kwamba sekta Binafsi ndie muajiri Mkuu.
Makamu wa Pili wa Rais aliwashauri Vijana popote walipo waamue kujiajiri kwa vile yapo maeneo mengi ya ajira katika sekta za Kilimo, Utalii, Biashara za Wajasiri amali.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri ya Sekta Binafsi ili watakaoamua kujiajiri waweze kupata Elimu na Utaalamu kupitia Vyuo vyuo vya Waajasiri amali vilivyopo na vitakavyoanzishwa.
Aliwakumbusha Vijana kujiandaa vizuri na kuwa waaminifu katika kukopa na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili mfuko wao uwe madhubuti na Vijana wengine waweze kufaidika nao.
“ Sera ya Mpango huu ni ukopeshaji na sio ugawaji wa sadaka ukiwa na lengo la kuwasaidia Vijana wasio na ajira ila wako tayari ”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiomba Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto kuwa makini katika usimamizi na uendeshaji wa mpango huo kwa kuzingatia misingi iliyowekwa.
Balozi Seif alisema Serikali iotaendelea na juhudi za kutafuta Washirika wa Maendeleo wa ndani na nje ili kuiunga mkono katika juhudi zake na kusaidia Mipango yake.
Akizungumzia kuhusu suala la Ukimwi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kuchukuliwa kwa kwa hatua madhubuti za kukinga maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Alisema ukimwi bado upona unaendelea kuathiri maisha ya wtu wengi hasa Vijana na matokeo ake Taifa linapoteza nguvu kazi muhimu kutokana na maradhi hayo yaliyokosa dawa hadi hivi sasa.
Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo Vijijini CRDB Tanzania ambae pia ni Meneja Uendeshaji wa Benki hiyo Bwana Samson Kenja alisema bado ipo changa moto kubwa katika utoaji wa huduma za Mikopo kwa Wananchi hasa kundi kubwa la Vijana.
Bwana Kenja amesema Uongozi wa Benki ya CRDB umeahidi kutoa Mafunzo kwa Vijana waliokuwa wameshajikusanya ili kuwajengea uwezo wa kujiwezesha Kiuchumi.
Alisisitiza kwamba mahitaji ya Vijana bado ni makubwa, hivyo Uongozi wa Benki yake utaendelea kujikita katika utoaji wa Mikopo kwa lengo la kuwajengea uwezo Vijana waliojikusanya katika Makundi ya Saccos.
Katika Risala yao iliyosomwa na Aziza Abeid Vijana hao wameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuajengea uwezo Vijana katika mfumo wa Kujiwezesha Kiuchumi na kukabiliana na hali ngumu ya Uchumi.
Vijana hao wametoa wito kwa Vijana wanaopata mikopo kufuata taratibu zilizopo hasa za urejeshaji wa mikopo kwa lengo la kuwpa fursa Vijana wengine kutumia fursa hiyo.
Mapema Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mh. Zainab Mohammed ameyapongeza Mashirika,Wahisani na Taasisi tofauti za Ndani na Nje zilizo kubali kusaidia harakati za Vijana katika kujiwezesha Kiuhumi.
Mh. Zainab amesema juhudi hizo zimewezesha kupunguza wimbi la Vijana wasiokuwa na ajira katika maeneo mbli mbali hapa Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment