Wananchi wa Kijiji cha Tumbe kiliyomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba wametakiwa kuwa na subra katika kipindi hichi kigumu kufuatia watu wananewa Kijiji hicho kufariki baada ya kula nyama ya Kasa hapo majuzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa nasaha hizo baada ya kufanya ziara fupi ya kuzifariji na kutoa mkono wa pole kwa Familia mbili zilizopatwa na masiba huo.
Balozi Seif alisema alipata habari hizo za kusikitisha ambazo familia moja pekee imepoteza watu saba kati ya wanane waliofariki kutokana na tukio hilo.
Alisema hiyo ni kudra ya Mwenyezi Muungu na wala hakuna mkono wa mtu.
“ Nyinyi mnawapenda sana jamaa zenu. Lakini tuelewe kwamba Mwenyezi Muunga anawapenda zaidi watu hao ”. Alitanabahishwa Balozi Seif.
Hivyo aliwataka wafiwa hao kundelea kuwa na moyo wa subira kwani hiyo ni njia ambayo kila kiumbe kitapita.
Wakitoa shukrani zao Mmoja wa wana Familia hizo Bwana Ali Mohd Bakari wameelezea faraja yao kutokana na ujio wa Kiongozi huyo ambao unaendelea kutatinda Mapenzi kati yao na Wananchi.
Wamesema kitendo hicho kimewajengea imani na kujihisi kwamba tukio hilo sio lao pekee bali ni la Wananchi na Viongozi wote Hapa Nchini.
Kasa aliyesababisha vifo hivyo alivuliwa tarehe 3 Januari na baadaye kuchinjwa kwa ajli ya kitoweyo ambapo iliwachukuwa saa 3 tuu walaji kuanza kupata athari zake.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top