Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Mabalozi wapya sita walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Mabalozi hao ni Dr. Batilda Buriani anakwenda Nchini Kenya, Balozi Shamim Nyanduga anakwenda Msumbiji, Balozi Grace Majuma anaenda Zambia, Dr. Ladislaus Komba anakwenda Uganda Uganda, Dr. Deodorus Kamala anaenda Ubelgiji na Balozi Philip Marmo anaenda China.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mabalozi hao kwamba changa moto kubwa inayowakabili ni kuhakikisha wanasimamia uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Nchi wanaozozisimamia.
Aliwataka kufuatilia kwa kina makubaliano au mikataba iliyopo kati ya pande hizo mbili ambayo wataikuta haijatekelezwa.
Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na Nchi zote sita kuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kinachohitajika zaidi kwao ni ustahamilivu katika kutekeleza majukumu yao waliyopangiwa..
Akitoa shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake Balozi Grace Mujuma ambaye ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Nchini Zambia alisema hivi sasa wana deni kubwa la kwenda kutekeleza jukumu walilopangiwa na Taifa.
Balozi Grace alisisitiza kwamba wanaahidi suala la kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Nchi wanazokwenda kutekeleza kazi zao litapewa nafasi kubwa zaidi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top