Nchi inaweza kugeuzwa kuwa jalala la kutupia vifaa vya kizamani vya analogi iwapo itachelewa kuingia katika mfumo wa sasa wa teknolojia ya Habarai ya Digitali.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu kampeni ya elimu kwa umma kuhusu Utangazaji wa Digitali iliyofanyika hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif Alisema seti nyingi za Televisheni za analogi zimekuwa zikiingizwa kwa wingi katika Nchi ambazo hazijaanza matangazo ya digitali athari ambayo inaweza pia kuikumba Zanzibar.
Alisema Serikali imedhamiria kwenda sambamba na mageuzi ya Utangazaji yanayotokea na kuhakikisha chini ya Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC } Taifa linaingia katika Teknolojia ya Dijitali kabla ya Disemba 2012.
“ Serikali yetu inafanya mazungumzo na Benki ya Exim ya China kwa lengo la kuipatia mkopo kwa ajili ya kununua mitambo ya kurushia matangazo na kuimarisha Studio za kutangazia kuendana na mabadiliko ya Teknoliojia” Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimepanga Disemba mwaka huu kuwa tarehe ya mwisho ya Televisheni za Analogi katika kanda hii.
Alisema Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa Ujumla imelazimika kutekeleza Maamuzi ya Mkutano wa Geneva wa mwaka 2006 ya kuanza matangazo kwa mfumo wa Dijitali ambao ni wa lazima.
Balozi Seif aliipongeza Tume ya Utangazaji Zanzibar { ZBC } kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania { TCRA } kwa uamuzi wao wa kuandaa Mafunzo wakielewa kuwa mabadiliko hayo yanawagusa Wananchi.
Akitoa Mada ya utoaji wa Elimu kwa Umma kuhusu Teknolojia ya Digitali Mrajis wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Abdulla Hassan Abdulla alisema utafiti wa mdogo uliofanywa unaonyesha kamba Zanzibar ina karibu seti za Televisheni laki 300,000 za mfumo wa Analogi.
Nd. Abdulla alisema taifa linakabiliwa na changa moto kubwa ya kwenda samba mbana mfumo wa teknolijia kwa vile tayari dalili za gharama kubwa za seti zinazoingizwa nchini zimanza kuonekana.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania Bwana Ali Gunze akitoa mada ya Uhamaji wa Teknolojia ya Analogi kuelekea Digitali katika sekta ya Televisheni kwa upande wa Tanzania kwa ujumla alisema mfumo wa Digitali utawawezesha Wananchi kupata huduma nyingi na bora zenye taaluma ya kiwango cha juu.
Bwana Gunze alisema Kiwango cha chanal kiongezeke kutoka 21 hadi 69 wakati masafa yaongezeke kutoka 760 hadi 862kwa mujibu wa azimio la Tume ya Kimataifa ya Mawasiliano { ITU }.
Mwakilishiwa Tume ya Mawasiliano Tanzania Bwana Inocent Mungi akitoa Mada ya Mkakati wa Elimu kwa Umma juu ya Uhamaji wa Mfumo wa Analogi kwenda Digitali alisema Mkakati huu wa Elimu ni muhimu na wa lazima.
Bwana Innocent alisisitiza kwamba Wananchi na Jamii kwa ujumla ni vyema ikafurahia huduma za Digitali.
Akiifunga Semina hiyo Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Mwenyekiti wa Semina hiyo Mh. Pandu Ameir Kificho ameiomba Serikali kuchukuwa hatua za haraka kupiga vita marufuku uingizwaji wa vifaa vifaa vya analogi.
“Uingiaji wa Vifaa vya analogi hapa Zanzibar Hivi sasa umeongezeka kwa vile ni kituo kikuu cha kupokea na baadaye kusifirisha katika Mwambao wa Afrika Mashariki ”. Alisisitiza Spika Kificho.
Mh. Kificho alisema kuendelea kupokea vifaa hivyo kwa sasa ni kuwatia hasara Wananchi pamoja na kuchafua mazingira kwa vile ni miezi michache tu Taifa linakaribia kuingia katika mfumo huo wa Digital.
Semina hiyo ya siku moja imeandaliwa kwa pamoja kati ya Tume ya Utangazaji Zanzibar { ZBC } kwa kushirikiana na Tume ya Mawasiliano ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania { TCRA }.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top