Bidhaa zinazozalishwa ndani ya Afrika Mashariki zinaweza kupata soko la uhakika iwapo wazalishaji wa bidhaa hizo watazitengeneza katika kiwango kilicho bora Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiifungua Semina kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema cha msingi kusisitizwa Wananchi ni kuwa na Ujasiri wa kutumia fursa za Umoja wa Forodha na Soko la pamoja ili kujiletea Maendeleo.
Balozi Seif alisema Wananchi walio wengi bado wana uelewa mdogo kuhusu masuala ya Mtangamano wa Afrika Mashariki hali ambayo inawatia hofu katika hatma yao ya baadaye.
“ Wananchi watatuuliza maswali mengi na tutakuwa na wajibu wa kuwajibu na kuwafahamisha mpaka waelewe kwa lengo la kuzijua haki zao za Jumuiya ya Afrika Mashariki ”. Alifafanua Balozo Seif.
Alisisitiza kwamba uelewa mkubwa wa Mtangamano huo wa Afrika Mashariki ni muhimu katika kubuni mbinu za kukabilianan na ushindani ili kuweka mazingira bora ya kuongeza tija katika uzalishaji na utoaji huduma.
Balozi Seif alieleza matumaini yake kwa Zanzibar kujenga shauku kubwa ya kushiriki kikamilifu katika Mtangamano wa Afrika Mashariki..
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Afrika Mashariki kwa kuandaa Semina hii ambayo itasaidia Wawakilishi kuwajengea uwezo wa kuwahamasisha Wananchi katika kutumia fursa zilizopo za Biashara, Uwekezaji na Ajira ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akitoa Mada ya Historia ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrka Mashariki Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dr.Abdulla Juma Abdulla alisema ushirikiano wa Jamii ya Watu wa Kanda ya Afrika Mashariki upo kwa karne kadhaa zilizopita..Dr. Abdulla alisema kilichovuruga ushirikiano huo ambao ulihusisha Damu na Biashara ulivurugwa na Watawala wa Kikoloni walioingiza ubaguzi na kusababisha matabaka Miongoni mwa Jamii hizo.
Wakichangia mada mbali mbali zilizowasilishwa katika Semina hiyo Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameiomba Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuzingatia maslahi ya Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Wamesema suala la msuko suko wa Sarafu lililoikumba Dunia kipindi kilichopita limeathiri pia Uchumi wa Zanzibar na kushindwa kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa ambao umepanda kwa kiasi kikubwa.
Wameshauri kuwepo kwa Timu ya pamoja ya Wataalamu wa kilimo wa Nchi zote Wanachama wa Kanda ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuwa na sauti moja katika Sekta hiyo muhimu kwa Wananchi walio wengi wa kanda hii ya Afrika Masharii.
Akiifunga Semina hiyo Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Mwenyekiti wa Semina hiyo Mh. Pandu Ameir Kificho alisema
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zazbar

0 comments:

 
Top