Kuendelea kuwepo kwa unyanyapaa ndani ya Jamii kumeelezwa kupunguza kasi ya Taifa na Taasisi zake za kupambana na ukimwi Kitaifa na Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Kjiji cha Makombeni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba.
Balozi seif alisema licha ya utafiti wa mwaka 2010 wa kupima kiwango cha unyanyapaa na ubaguzi wa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi unaonyesha kupungua lakini bado tabia hiyo katika Jamii inayotuzunguuka.
Alisema hiyo si tabia nzuri wala ustaarabu na ni dhambi mbele ya Muumba. Hivyoamewasili wananchi kuwaona wenzao waliopata bahati mbaya ya kuambukizwa kuwa bado ni sehemua ya Jamii na wanahitaji kuheshimiwa, kulindwa na kushirikishwa katika maisha ya kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali inakusudia kupitisha sheria ya Ukimwi kwa ajili ya kuweka mazingira bora ili Watu wote wapate huduma, wajikinge na kukingwa na maambukizi ya Virusi vya ukimwi.
Alitanabahisha kwamba Mkakati wa pili wa Taifa wa Ukimwi utatekelezwa kwa kuheshimu haki za Binaadamu katika upatikanaji wa huduma kwa wote bila ya kunyanyapaliwa au kubaguliwa kutokana na sababu zozote zile.
‘‘ Moja ya changamoto ambayo inatukabili katika mapambano dhidi ya ukimwi ni kutegemea sana fedha za wahisani katka Programu nyingi. Kwa bahati mbaya fedha hizo zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na hivyo kuleta ugumu katika utekelezaji wa Programu za Ukimwi ’’. Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliipongeza Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar Zapha + kwa namna inavyoshiriki kaika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Alisema Jumuiya hiyo imefanikiwa kuwafariji na kuwaelimisha wanachama wake juu y namna bora ya kuishi na Virusi vya Ukimwi pamoja na Kuwatunza Watoto waliofiwa na Wazazi wao kutoknana na Ukimwi. {Yatima }.
Alizitaka Taasisi zinazoshughulikia na kusimamia ajira na Uwezeshaji kuhakikisha kwamba wanawake wanafaidika na Programu zilizopo kwa vile wao ndio wanaoambaukizwa zaidi ili kuwapunguzia matatizo ya kiuchumi yanayopelekea kujitumbukiza katika ajira mbaya kama uasherati.
Mapema Mwenyekiti wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Profesa Saleh Idriss Mohd amesema Zanzibar imeweza kufanikiwa kudhibiti kiwango cha maambukizi ya Virusi vya ukimwi chini ya asilimia 1%.
Profesa Saleh amesema lengo la Mkakati wa kupunguza Virusi hivyo imeelekezwa kufikia asilimia 03% katika Mkakati mpya.
Hata hivyo Profesa Saleh alisema ugumu wa Jamii kuendelea kubadilika kitabia unachangia maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na hasa kwa akina mama.
Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa inayojihusishsa na Mapambano dhidi ya Ukimwi ya UN AIDS Dr. Luc Ban ameipongeza Tanzania na Zanzibar kwa ujumla kutokana na Mikakati inayochukuliwa ya kukabiliana na janga la Ukimwi.
Dr. Ban alisema juhudi hizo zimepunguza maambukizo mapya ndani ya ukanda wa Maziwa Makuu na kuwa mfano bora wa kuigwa.
Wakitoa salamu zao Wanachama cha Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi Zanzibar Zapha + wameishauri Serikali kuanzisha Mfuko Maalum utakaosaidia huduma zao hasa wakati misaada ya wahisani inapochelewa.
Walisema changa moto inayowakabili hivi sasa ni ukosefu wa dawa zinazosaidia kupunguza maradhi nyemelezi.
Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Ftma Alhabib Fereji alisema lengo la Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Kila ifikapo Disemba Mosi ya kila mwaka ni Kutafakari hatua zinazochukuliwa katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi Duniani yaliambatana na Maandamano pamoja na Maonyesho ya Kazi za Mikono zilizoshiorikisha Wafanyakazi wa Taasisi za umma, Wafanya biashara ndogo ndogo, Wajasiri amali pamoja na Wanafunzi .
Ujumbe wa mwaka huu wa siku ya ukimwi duniani ni Zanzibar bila ya Maambukizi mapya ya ukimwi, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi inawezekana ?
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top