ni kitu cha busara kwa uongozi wa AZAM MARINE na FAST FERRIES MATAWI YA PEMBA, kwa kutoa tangazo hili lenye muelekeo wa kuwaheshimu abiria na mali zao pamoja na taratibu za kiusalama kwenye vyombo hivyo vya usafiri wa baharini
ingawaje sina uhakika kama walichokitangaza kama ni kweli au ni uongo hilo ni juu yao, lakini bado tunashuhudia mizigo kama hiyo ambayo imetangzwa imekuwa ikishushwa ndani ya boti hizo kila uchao, lakini hebutuwe wawazi zaidi je tangazo hili ni kwa PEMBA TU au bandari zote?
ikiwa ni kwa Pemba tu ni kwenda kinyume na haki za binadamu kwani abiri watokao Pemba, Unguja , Dar-es-salaam wote ni binadamu na ni Watanzania na kwa mujibu wa katiba zote mbili wote wanahaki iweje tangazo hili liwe kwenye Bandari ya Mkoani tu? wakati tunashuhudia mizigo kama hiyo inakwenda Dar-es-salaam kila uchao na pia inatoka Dar kuja Zanzibar (Unguja) vile vile.
najuwa kilichoangakiwa hapa ni suala la kiusalama zaidi, lakini hii ni kwa mizigo tu au hata kwa abiria kwani, tiketi za boti hizi huwa zinauzwa kiholela holela tu na muda mwengine hata abiria huwa hawana pa kukaa na kusababisha msongamamo kwenye chumba cha daraja la kwanza (first class), kwani abiria wanapozidi hutolea daraja la tatu na kupelekwa huko jee hili uongozi mmelizingati au ni vitanda tu na baiskeli ndio vinavyoosababisha ajali kwenye boti zenu?

0 comments:

 
Top