Na Haji Nassor

Wananchi wa Kisiwa cha  Pemba walijumika kwa pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik kwenye kilele cha tamasha la 100% Zanzibari lililobeba sura ya kusherehekea kutimia kwa miaka miwili tangu kufikiwa kwa maridhioano ya kisiasa ya Zanzibar na kupelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Wananchi hao ambao pamoja na mengine walishuhudia Ngoma za asili , Taarab na Maigizo kutoka kwa vikundi mbali mbali kutoka Unguja na Pemba. Maonesho hayo yalifanyika katika uwanja wa Gombani, kuanzia saa 10 jioni kwa ratiba ya awali na kuendelea kuanzia saa 2.30 usiku kwa ajili ya ratiba rasmi
Mamaia ya wananchi hao walikua hawatulia vyema kwenye viti vyao wakati wote wasanii hao wa Zanzibar walipokua wakiporomosha vimondo vyao vya hasa vilivyoendana na siku yenyewe .
Waliokuwa wamwanzo katuzihangaisha nyoyo za w ananchi wa Pemba pamoja na ugeni uliokuwepo uwanjani hapo kwa furaha ni kikundi cha taarabu cha Pemba all star walipoporomosha nyimbo zao tatu nfululizo kila moja ikimpita mwenzake kwa kuibua hamasa jana hiyo.
Wimbo unaotambulika lwa jina la ‘Maridhiano ambao uliimbwa na Wastara ndio ambao waliwanyanyua juu ya viti vyao wenyeji na hata wageni wasiojua lugha ya Kiswahili kutokana na vinanda vilivyopamgika.
Wimbo huo ambao mara baada ya kumalizika kwakwe wnanachi wakaomba urejewe uliwakuna wengi akiwemo musisis wa Mpinduzi ya mwaka 1964 Hassan Nassor Moyo ambae nae alikua mmoja kati ya waaliojumika uwanjani hapo.
Muimbaji Asha Ali nae aliibua hisia na kuwafanya baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba Juma Kassim Tindwa, Wakuu wa Wilaya za Wete na chake chake, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, mwalikishi wa Jimbo la mjini mkongwe pamoja na maafisa wadhamini kuonekana na furaha.
Wimbo uliosababisha kuvamiwa kwa stage la muimbaji huyo ni ule usemao Mambo poa ambapo ulionyesha hisia za muafka wa Zanzibara uliozaa matunda na kufikia mambo kua poa kwa wananchi wote wa Zanzibar.
Pemba Taarab All-Stars wakaishia na wimbo wake 'Napenda' alioumbia msanii Said Dokoa ambapo hapo uliwafanya hata ujumbe wa balozi kutaka kujua juu ya wimbo huo kutokana na kuona kuziteka hisia za wananchi ambapo Makamu wa Kwanza akionekana kama akimtafsiria na kisha kutabasabu.
Nayo Mkota Ngoma kutoma Wilaya ya Mkoani iliwaacha baadhi ya wananchi mara baada ya kuhitimisha usiku huo ulioitwa wa weupeni kujaa hamu na ngoma hiyo kutokana na umahiri na ushajaa wa wanakikundi hicho.
Wazee wa taarabu wa Zanzibar Culture ndio waliokuja kuzisuuza nyoyo na roho za wananchi Pemba kufuatia wimbo wao ‘Bure asikupumbaze’ ulioporomoshwa na Mtumwa Mbarouk huku wananchi wakizidi kujenga upendo ndani ya nyoyo zao
Mradi wa 100% Zanzibari umeandaliwa na taasisi ya Swahili Center na umeendeshwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway pamoja na kampuni ya mawasiliano ya Zantel

0 comments:

 
Top