Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amelipongeza Shirikisho la Kimataifa la Jumuiya ya khoja Shia ithna-asheri kwa juhudi zake za kusaidia Maendeleo ya Elimu Hapa Zanzibar.
Balozi Seif alitoa pongezi hizo baada ya Kukabidhiwa Seti tatu za Kompyuta kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Duniani Dr. Ali Dinna.
Rais wa Jumuiya ya Koha Shia Ithna-sheri hapa Zanzibar Nd. Mohd Raza amekabidhi msaada huo kwa Niaba ya Rais wa Shirikisho hilo hafla iliyofanyika katika Skuli ya Kitope.
Balozi Seif ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maendeleo makubwa yamepatikana ndani ya Jimbo la Kitope kutokana na kupata nguvu za Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri.
Aliwaomba wananchi wa Majimbo mengine kuhakikisha wanachagua Viongozi wazuri watakaowaleteta maendeleo ya haraka katika Majimbo yao bila ya kuangalia ujomba au rafiki.
Mapema Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri Zanzibar Nd. Mohd Raza alisema Taasisi yao itaendelea kusaidia huduma za Kijamii, Elimu na Uchumi ili kuona ukali wa maisha unapungua miongoni mwa Wananchi.
Kompyuta hizo zenye thamani ya shilingi milioni nane ni utekelezaji wa ahadi ya Uongizi wa Shirikisho hilo waliyoitowa tarehe 30 Mei mwaka huu wakati wakikabidhi msaada wa madeski katika skuli zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope.
Wakati huo huo Balozi seif alizindua Kikundi cha Ushirika cha Ushonaji kiitwacho hatubaguani wote ni wetu cha jimbo la Kitope kinachoendelea kupata mafunzo katika ofisi ya jimbo hilo hapo kinduni.
Balozi Seif pia alikabidhi msaada wa vyarahani, mota pamoja na Vifaa mbali mbali vya kujifundishia vikiwa na thamani ya jumla ya shilingiMilioni 2,325,000/-.
Akitoa nasaha zake katika Hfla hiyo Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi amewaomba Wake wa waheshimiwa kuwasaidia Waume zao katika kufanya ziara za kujua matatizo yanayowakabili Wananchi.
Mama Asha Alisema utaratibu huo utasaidia kuibua matatizo ya msingi na kuleta upendo katika kuharakisha maendeleo ya pamoja kati ya Viongozi na wanaowaongoza.
Kikundi cha ushirika cha ushoni cha hatubaguani wote ni wetu chenye wanachama 45 kimelenga kutoa mafunzo kwa wnanchi wake kwa nia ya kusambaza ajira miongoni mwa wanawake ambao ndio walezi wa
Familia popote pale.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top