MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKISALIMIANA NA MJUMBE WA KAMATI YA SIASA NA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMINISTI CHA CHINA CCP BW, LIU YUNSHAN ANAEONGOZA UJUMBE WA WATU 21 WALIOFIKA OFISINI KWA BALOZI SEIF ILIOPO MTAA WA VUGA MJINI ZANZIBAR
Jamuhuri ya Watu wa China itaendelea kuwa Kiungo muhimu katika harakati za kusaidia Uchumi na Maendeleo ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Ujumbe wa Viongozi 21 wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Chama cha Kikoministi { CCP } wa Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa na pia Kamati Kuu ya Chama hicho Bw. Liu Yunshan hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema Tanzania na Baraza zima la Afrika Limekuwa na kasi ya maendeleo kutokana na nguvu za msukumo wa China licha ya Baadhi ya Mataifa ya Magharibi kulalamikia hatua hiyo ya china.
Alisema uwekezaji wa Makampuni ya China katika Miradi ya Kiuchumi hasa yale ya Maadini, Viwanda na Miundo mbinu ya Mawasiliano imeweza kusaidia mapato ya Taifa na kuongeza ajira kwa Wazalendo waliowengi hasa Vijana.
“ Wenzetu wa Magharibi wanalalamikia kasi ya China Kuvamia Bara la Afrika kiuchumi lakini wamesahau kwa China ni mshirika wa Bara hili tokea Nchi zetu zinadai Uhuru kutoka kwa hao wanaomlalamikia ”.
Alifafanua Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo kwamba Zanzibar bado inahitaji nguvu za Jamuhuri ya Watu wa China katika kuimarisha Uchumi wake
Balozi Seif alisema Wawekezaji na Makampuni ya China yana nafasi nzuri wa kuwekeza miradi yao Zanzibar hasa katika Sekta ya Utalii na Viwanda.
Aliipongeza China kwa Juhudi za za kutoa Taaluma kwa watendaji mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo wale wa Sekta inayonedelea kuimarishwa hivi sasa kwa ajili ya utoaji ajira ya Uvuvi.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa na pia Kamati kuu cha Chama cha Kikoministi cha China Bwana Liu Yunshan alimueleza Balozi Seif kwamba Nchi yake itaendelea kuunga mkono sekta za Uchumi na Maendeleo ya Tanzania na Zanzibar kwa jumla.
Bw. Liu alisema Makampuni mengi yameonyesha hamu ya kuendelea kuwekeza katika maeneo ya Umeme, Madini na Viwanda kufuatia rasilmali iliyopo Nchini Tanzania.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu cha CCP amesisitiza kwamba uhusiano wa mude mrefu uliopo katika ya China na Tanzania na Zanzibar unastahiki kuimarishwa zaidi.
Ujumbe huyo wa Viongozi 21 kutoka Jamuhuri ya Watu wa China upo Nchini Tanzania kwa ziara rasmi na tayari umeshakukutana kwa mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa pamoja na Kutembelea sekta za Kiuchumi.
Wakati huo huo Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Nchini Indonesia Unaoongozwa na Waziri wa Nchi anayesimamia wizara za Biashara na Viwanda na ile ya Maendeleo ya Taifa ya Indonesia Bwana Lee Shyan umeonana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar yamelenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Zanzibar na Indonesia.
Ujumbe huo umehidi kulifanyia kazi mara moja ombi la Zanzibar la upatikana na meli kubwa za kudumu zitakazosaidia usafiri wa abiria na mizigo kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba
Viongozi wa pande hizo mbili wamesisitiza haja ya kuangalia miradi ya pamoja itakayosaidia kuongeza kasi ya maendeleo na kustawisha jamii za sehemu hizo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top