TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Bendera ya Tanzania itaendelea kupepea na kushamiri nje ya Mipaka iwapo watendaji wa Afisi za Kibalozi za Nchi hii watatekeleza vyema majukumu yao waliyopangiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo katika Tafrija Fupi aliyoandaliwa yeye na Ujumbe wake na Ubalozi wa Tanzania uliopo Mjini Addis ababa Nchini Ethiopia .
Balozi Seif alikuwa na mapumziko mafupi ya ziara yake Mjini Addis ababa akielekea Jamuhuri ya Watu wa china kuhudhuria Tamasha la 12 la Maonyesho ya Biashara na Viwanda katika Jimbo la Sichuaji lilioko Magharibi mwa China .
Amesema ni vyema kwa watendaji hao kuhakikisha kwamba matendo yao yanaoana na sifa ya Tanzania ambayo tayari imeshaenea katika sehemu mbali mbali Duniani.
“ Sisi tunapendwa sana na kuonewa wivu na wenzetu hasa wale majirani wetu waliotuzunguuka” Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif aliwatahadharisha watendaji hao kujiepusha na mambo yote ambayo yanapigwa Vita ya Taifa na hivi mtakuwa tayari mmeshamsaidia Balozi wenu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha wanadiplomasia hao kusaidia na kuhakikisha wanajenga mustakabala mwema wa maisha yao ya baadaye.
Amesema si vyema kwa watendaji hao kuwa wageni wanaporejea nyumbani kutakotokana na kushindwa kujiwekea hatma njema ya baadaye.
Mapema Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Bwana Joram Biswano amesema Mchango wa Balozi Seif katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa umewawezesha watendaji wengi kuwa na uwezo mkubwa kiutendaji.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi tayari ameshawasili katika Jimbo la Sichuan na anatarajiwa kufanya ziara katika Maeneo ya Kihistoria na Miradi ya kiuchumi kabla ya kuhudhuria Ufunguzi wa Tamasha la 12 la Maonyesho ya Kibiashara na Viwanda yatakayofanyika Tarehe 20/10/2001.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top