TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dalili za mafanikio ya Maendeleo ya Kiuchumi na Ustawi wa Jamii ndani ya Bara la Afrika yanaanza kuchomoza kufuatia Bara hili kuungwa mkono na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China katika miradi tofauti ya maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo kwenye Uwanja wa Michezo wa Jimbo la Sichuan Nchini China wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la 12 la Maonyesho ya Biashara na Viwanda.
Balozi Seif ambae ameiwakilisha Tanzania katika Tamasha hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano Mh. Mizengo Pinda amesema juhudi za China kuwapatia Taaluma Wasomi wa ngazi ya juu wapatao 15,000 wa Bara la Afrika ni mwanzo mzuri wa kunyanyua Ustawi wa Kiuchumi wa Mataifa ya Afrika.
Amesema hatua hiyo imekwenda sambamba na kupatiwa mafunzo Wataalamu 100 wa ngazi ya Juu katika sekta ya Kilimo, ujenzi wa Hospitali 30 za Kisasa na Ujenzi wa Skuli 100 za elimu ya juu katika maeneo ya Vijijini Barani Afrika.
“ China ni Mshirika Halisi katika juhudi za kuona umaskini Barani Afrika unapungua au kutoweka kabisa ”. Alisema Balozi Seif. Balozi Seif alifahamisha kwamba China katika kuliona Barala la Afrika linasimama imara kujitegemea Kiuchumi Nchi hiyo iliamua kusaidia kusaidia zaidi ya Yuan Bilioni elfu 2.3 fedha za China mwishoni mwa mwaka 2007.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Jmuhuri ya Watu wa China kwa uamuzi wake wa kuendelea kuunga mkono Bara la Afrika katika kujikwamua na Umaskini.
Akizungumzia Tamasha la Maonyesho ya ya 12 ya Biashara na Viwanda Balozi Seif amesema mpango huo wa Jimbo la Sichuani ni fursa adhimu kwa Wafanyabiashara wa China na Afika kshirikiana pamoja.
Blozi Seif alisema kupitiaTamasha hiloWashirika wa pande hizo mbili watapa nafasi ya kubadilishana uzoefu utakapelekea kujenga umadhubuti katika sekta za Biashara ambayo ni muhimu kwa pande hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amesisitiza kwamba Tanzania na Zanzibar kwa jumla tayari inaendelea kuimarisha miundo mbinu kwa lengo la kuvutia wawekezaji wa Nje.
Amewashauri Wawekezaji wa China kufungua zaidi milango ya uwekezaji Nchini Tanzania hasa katika Sekta za Utalii, Mawasiliano, Bahari na Madini kwa vile mazingira mazuri kwenye Sekta hizo yameshawekwa.
“ Kuna kila sababu kwa Wawekezaji wa China na Hasa Jimbo la Sichuan kuja kuwekeza Tanzania ambapo watapata tija kutokana na mazingira bora yaliyopo ya Kibiashara ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif amewahakikishia Wawekezaji wa China Kwamba utulivu wa Kisiasa uliopo hivi sasa pamoja na Sera Nzuri madhubuti zilizopo utawapa fursa nzuri ya kufanikisha miradi yao ya Uwekezaji.
Tamasha hilo la 12 La Maonyesho ya Biashara na Viwanda Jimboni Sichuan Nchini China lilijumuisha pia maonyesho ya Biashara yaliyotawaliwa zaidi na uwezo wa Kiteknolojia ya kisasa iliyofikiwa na Jimbo hilo .
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top