Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameitaka jamii kuondoa hofu ya dhana kwamba Mahkama imefuta kesi inayowakabili watu wanaotuhumiwa kuhusika na uzembe katika ajali ya Meli ya M.V Spice Islanders iliyotokea hivi karibuni.
Balozi Seif ametoa kauli hiyo katika mfululizo wa ziara zake za kuzifariji Familia zilizopatwa na msiba kufuatia vifo vya watu waliokuwemo ndani ya Meli hiyo ikielekea Kisiwani Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa na Ujumbe mzito wa Viongozi wa ngazi ya juu ya Serikali Wakiwemo Masheikh katika ziara hiyo amesema Mahkama ilichofanya hivi sasa ni kusitisha kuendesha kesi hiyo ikitoa nafasi kwa Tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa kujua chanzo cha ajali hiyo na baadaye kutoa Ripoti kamili.
Amesema kesi hiyo itaendelea tena mara baada ya Ripoti ya Tume hiyo kwa vile shauri hilo tayari polisi wameshalifikisha mahakamani baada ya kufanya uchunguzi wa awali.
Balozi Seifa ameendelea kusisitiza kwamba Serikali itatekeleza mapendekezo yote ya Tume hiyo likiwemo lile la watakaobainika kuhusika na uzembe hatua za kuwawajibisha zitachukuliwa mara moja.
Kuhusu suala la idadi ya Watu waliokuwemo ndani ya meli hiyo Balozi Seif amesema uchunguzi huo utafanywa kwa kina ili kuhakikisha Serikali inahakiki kwa lengo la kupata idadi ya watu waliokuwemo ndani ya chombo hicho.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wafiwa wenzake Maalim Silima Hassan wanaendelea na msiba huo huku wakipata faraja kutokana na kuungwa mkono na Serikali katika kuomboleza msiba huo.
Wamesema watajitahidi kuziepuka Taarifa za Baadhi ya vyombo vya nje vinavyoripoti Taarifa zinazojaribu kuchangia cheche za kuendelezwa msiba huo kinyume na hali halisi ilivyo.
Wakati huo huo Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameendelea kupokea michango inayotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya za Kiraia kwa lengo la kuwafariji watu walipatwa na maafa kufuatia ajali ya Meli ya M.V Spice hivi karibuni.
Waliochangia Kamati hiyo ni pamoja na Ubalozi Mdogo wa Misri Uliopo Zanzibar ambao umekabidhiDawa zenye uzito wa karibu kilogram 120,nJumuiya ya Youth Self Employement, Benki ya FEMB, Ujumbe wa Mfalme wa Ras Alkheima,Kampuni inayojenga bara bara ya MECCO, Kampuni ya Mafuta ya Gapco, Kmpuni ya Mipira ya Agro Tex pamoja na Familia ya Marehemu Mzee Shaaban Khamis Mloo,
Nyengine ni Uongozi wa Shirika la ndege la Precision, Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } PAMOJA NA Mamlaka ya usafiri wa ANGA Zanzibar.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

0 comments:

 
Top