WFP yalaani taarifa ya wizi wa chakula cha msaada
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linalaani hatua zozote za kuiba chakula cha msaada kwa ajili ya mamilioni ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa. Shirika hilo limesema linachunguza madai hayo ya wizi unaodaiwa kufanyika mjini Moghadishu.WFP inasema nia yake ni kuhakikisha chakula cha msaada kinawafikia walengwa lakini haliwezi kufuta uwezekano wa wizi wa baadhi ya chakula chake cha msaada kutokana na matatizo ya kiusalama nchini Somalia
0 comments:
Post a Comment