Suala la kubadili tabia kwa jamii ya Kitanzania ya sasa ni suala la lazima na sio la hiyari, ingawaje inaonekana kwamba kisingizio kikubwa ni kwamba kila mtu ana haki ya kufanya atakalo kwa mujibu wa katiba. Ingawaje uhuru huu wa mtu mmoja mmoja kwa kiasi kikubwa umekuwa ukichangia maongezeke ya virusi vya ukimwi siki hadi siku huku Zanzibar ikionekana kuwa na asilimia 0.6 ya maambikizi yaliyopo hivi sasa, ingawaje bado maambukizi yanaendelea siku hadi siku ingawaje hakuna mchanganuo wa idadi ya wanawake na wanaume wangapi.Na kwa upande wa Tanzania bara ni alisilimia 80 ya maambukizi yote.
kama hiyo haitoshi malazi yasiyofuata maadili, mila na silka za Kitanzania zimekuwa chanzo cha kuongeza mmomonyoko wa maadili katika taifa hili kwa wazee na vijana kuiga mambo ambayo yanaonekana ni ya kisasa zaidi kupitia vyomba vya habari na mitandao tofauti iliyopo nchini hivi sasa, lakini jamii inapaswa kufamu kwamba ukosefu wa wawazi katika malezi, wogo wa kuwaogopa watoto kwa kuhofiaa kwamba ukisema nae atajiuwa hiyo siyo silaha ya kutokuesema na mtoto wako na si mapenzi hata kidogo.
Kitu cha kufanya ni kupata muda wa kuweza kusema na watoto  wetu na jamii kwa ujumla hili linawezekan bila ya kuwa na mfadhili kwani mfadhili mkuu ni nafsi yako na wa pili ni mzee na si marafiki kama ilivyozoeleka hili linawezekana bila ya kutumia fedha nyingi za serikali wa wafadhili au kupitia semina elekezi 

0 comments:

 
Top