Afisi yaUmoja wa Mataifa  inayojishughulisha na masuala ya haki za binadamu, imeelezea hofu yake dhidi ya uharibifu uliofanywa kwenye jengo la taasisi ya amani na demokrasia mjini Baku Azerbaijan Agosti 11. Uharibifu huo umehusisha ofisi zingine mbili zisizo za kiserikali, katika kampeni ya kupinga mabomu ya kutegwa ardhini na kituo cha wanawake, ambacho kilikwa kituo pekee cha kusaidia wanawake wenye matatizo, wakiwemo waliofanyiwa ukatili nchini Azerbaijan.Afisi ya haki za binadamu inasema mabulidoza yaliyoamriwa na meya wa Baku bila kutoa taarifa yamekwenda na kubomoa jengo la afisi hizo. Mkuu wa haki za binadamu ametoa wito wa kufanyika uchunguzi na ikiwezekana kuwalipa fidia wahusika

0 comments:

 
Top