Wapiganaji wa Libya wadai kuingia katika mji wa Zawiya na inasemekana kwamba wapiganaji hao waliingia katika mji huo jana, wakati huo huo wakuu wa Tripoli wamedai kuwa bado wanaudhibiti mji huo wa Zawiya. Endapo wapiganaji wa Libya watafanikiwa kuuteka mji wa Zawiya kwao utakuwa ni ushindi mnono na ni pigo kwa kiongozi wa Libya. Mji huo ni jirani na mji mkuu, na uko kwenye barabara inayotoka Tunisia, njia muhimu kwa Kanali Gaddafi. Ni wazi kuwa wapiganaji wameweza kuingia mjini humo jana, ingawa walipigwa mizinga na risasi. Ripoti moja kutoka Zawiya kwenyewe, ilisema wapiganaji walikaribishwa na mamia ya wenyeji. Wapiganaji wanadai kuwa usiku ulipoingia, walikuwa wameshaudhibiti mji.Wakuu mjini Tripoli wamesema shambulio la wapiganaji lilikuwa dogo tu na kudai kuwa bado wanaudhibiti mji wa Zawiya

0 comments:

 
Top