Kiasi ya watu 14 wamekufa katika nja katika eneo la Kaskazini Mashariki la Turkana nchini Kenya, vifo hivyo ambavyo vinahusishwa kutokana na njaa na ukame unaoendelea katika eneo la Turkana nchini kenya, imeelezwa kwamba ni tokea la  kwanza kutokea ambalo linagharimu maisha na uhai wa watu nchini Kenya.
Mbunge wa Turkana, John Munyes, alisema vifo hivyo vimetokea katika vijiji vitatu baada ya serikali kushindwa kusafirisha chakula kwa ajili ya watu walioathiriwa na ukamenchni kenya.Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya raia wa Kenya milioni nne wanatishiwa na ukosefu wa chakula katika eneo lilikumbwa na ukame mbaya katika kipindi cha miaka 60. Nchi nyingine zilizoathiriwa ni Somalia, Ethiopia na Djiblouti.
Mwandishi wa BBC Odiambo Joseph akiwa Turkana anasema ametembelea kijiji ambacho mamia ya watu wengi wao wakiwa wazee na dhaifu walikuwa kwenye mstri mrefu wa kugawiwa chakula. Watu 14 waliokufa nchini Kenya walikuwa watu wazima, lakini watoto pia wana utapiamlo mkali, mwandishi wa BBC anasema

0 comments:

 
Top