Akina mama nchini wametakiwa kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kimaendelo ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Mama mlezi wa kikundi cha tushikamane kina mama, Bi.Sharifa Nambaga ameeleza hayo alipokua akizungumza na hits fm radio huko Migombani Wilaya ya Mjini Unguja.Amesema endapo akina mama hao watakuwa na jitihada ya kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo kama kilimo cha mbogamboga wataweza kuepukana na hali ngumu ya maisha.
Sharifa ameongeza kuwa kutokana na juhudi wanazozichukuwa bado wanahitaji mipira ya kumwagilia maji mazao yao ili wafikie malengo waliokusudia.
Mama mlezi huyo ameiomba serikali kuwawezesha na kujenga utamaduni wa kuvitembelea vikundi vidogo vidogo ili waweze kujulikana zaidi. Kikundi cha tushikamane kina mama kinachojishughulisha na mboga mboga kimeanzishwa mwaka 2010, kina wanachama 21 ambao wanawake 19 na wanaume 2.

0 comments:

 
Top