Afrika Kusini imesema haijatuma ndege Libya kumsaidia kiongozi wa nchi hiyo anayepingwa Moammar Gadhafi ili kuondoka nchini.Katika taarifa yake jumatatu, Serikali ya Afrika Kusini imesema inataka kukanusha tuhuma kwamba ndege za Afrika Kusini zitamsafirisha kanali Gadhafi na familia yake kwenda sehemu isiyojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje Maite Nkoana –Mashabane alisema bwana Gadhafi hajaomba hifadhi Afrika Kusini na anauhakika kwamba hawezi kufanya hivyo. Amsema haijulikani mahali alipo kiongozi wa Libya.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliongoza juhudi za umoja wa Afrika kutatua mzozo wa Libya baina ya Serikali ya bwana Gadhafi na waasi wanoungwa mkono na magharibi.
Huku ikionekana kuwa bwana Gadhafi ataanguka, Afrika Kusini imesema jumatatu kwamba inaunga mkono utaratibu wa Umoja wa Afrika unaotaka kuwepo serikali ya mpito ya Libya, kuandika rasimu ya katiba mpya, na kuitishwa kwa uchaguzi wa kwanza kabisa wa kidemokrasia nchini humo

0 comments:

 
Top