Bunge la Uingereza linatarajiwa kukutana kwa ajili ya kujadili machafuko yaliyotoke hivi karibuni nchini Uingereza.Waziri Mkuu David Cameron ambaye alikatisha likizo yake ameliruhusu jeshi lapolisi ya nchi hiyo kutumia  magari yenye maji ya kuwasha kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji waliojazana mitaani katika miji ya Tottenham na Manchester.
Wabunge wa nchini hiyo wanatarajiwakukutana kwaenye kikao cha  dharura ili kuweza kupata muda wa kujadili kwa kina  hali ya machafuko yaliyojitokeza hivi karibuni mara baada ya vijana kufanya vuguru za kupinga kuuliwa kwa kupigwa risasi Mark Duggan kutokana na kukaidi amri halali ya polisi.
Waziri Mkuu Cameron amewahakikishia wananchi kuwa polisi wataendelea kupambana n waandamanaji hao na kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini humo kama ilivyokuwa awali.
Waziri Mkuu ameeleza kwamba hatua zilizochukuliwa hivi sasa na jeshi la polisi ni kuhakikisha kwamba wanadhibiti kwa kiasi kikubwa hali ya ghasi  ghasia zinazoendelea nchini humo na kuahidi kuongeza idadi ya  polisi katika kila mtaa wenye machafuko na vitendo vya uhalifu.

0 comments:

 
Top