kwa kawaida kila muamba ngoma hujivutia kwake.
hii ni methali ya kawaida kwa jamii ya waswahili na hasa ile ya pwani ya Afrika ya Mashariki na hususana watu waishio katika visiwa vya Zanzibar
suala la usafi ni kitu muhimu katika jamii na ni suala la kila mtu au awe ni mfanya kazi wa taasisi au mpita njia tu katika taasisi hiyo
si kitu cha kushangaza hata kidogo kumuona mtu mwenye athari za akili kuwa anaokota kitu jaani au katika debe la taka halafu akakila hii ni kutokana na athari aliyokuuwa nayo kutokana na kuathirika kwake kiakili na si vyenginevyo
lakini inashangaza kuona sehemu muhimu yeye watu ambao sio waathirika wa akili tena ni wafanyakazi na waalipwa msharaka katika mahospital au vituo vya afya vya kiserikali lakini cha ajabu kitu usafi kwao ni kitendawili
lakini watu hao hao wanapokwenda katika vile vihospitali vinavyoitwa vya watu binafsi huwa ni walimu wazuri wa kurekebisha tabia za wenzao utadhani wao wanatimiliza majukumu yao ipasavyo
siku ya leo niliweza kuitembelea hopitali kuu ya Mnazi Mmoja visiwani hapa, lakini kwa kweli hali ya usafi bado ipo chini sana na si ya kuridhisha hata kidogo, kiasi ambacho hata wewe uanayekwenda kumkaguwa mgonjwa unaomba mungu usishikwe na haja ili usiingie huko chaooni kwa kweli ni aibu tupu kwani harufu mbaya itokayo chooni imekuwa ni adha na kero kwa kiasi kikubwa katika baadhi ya wodi za kulazia wagonjwa
ni kweli Mnazi Mmoja ni hospital kuu lakini jee suala la usafi limepewa nafasi gani? kwamba irimradi mkono unakwenda kinywani tu inatosha? po haja kwa waliopewa dhamana na wananchi kulitambua hili ikiwezekana kufanya ziara za mara kwa mara katika hospital hii ili hata wale madaktari wa kigeni wawe na hamu ya kuja tena kutusaidia
kwa kweli ipo haja ya kubadilisha utamaduni na kuheshimu suala hili kwani usafi katika kituo cha afya peeke ni tiba seuze kumuona muuguzi
inawezekana tutimize wajibu wetu

0 comments:

 
Top