katika kitabu kitakatifu cha biblia kuna maandiko yasemayo hivi "msipowashinda waandishi na mafarisayo ufalme wa mungu hamutaupata" haya ni mafundisho muhimu kwa mto mwenye akili
kwa kweli sikuwa na haja ya kuyanukuu maneno hayo, lakini imenibidi nifanye hivyo, kwani inaonekana kwa kiasi kikubwa kalam za baadhi ya waandishi wa habari zimekuwa ni silaha za maangamizi katika baadhi ya mataifa dunia kote
ingawaje kwa hapa kwetu kalam hizo huwa zinafanya kazi vizuri katika kile kipindi maalumu cha ambacho baadhi ya wanasiasa huwatumia baadhi ya waandishi kwa makusudi kwa ajili ya kuweza kuihujumu jamii
kwa kweli tatizo la matumizi hayo mabaya yanaonekana kushamiri zaidi katika bara la Afrika na hata hapa Zanzibar zipo kalamu nyingi ambazo huwa zinaandika kila wanachodhani kwao ni kizuri kwa kuanagalia upande mmoja wa shilingi
kwa mfano yapo baadhi ya matokeo ambayo yaliripotiwa vibaya katika visiwa vya Zanzibar katika miaka mitano iliyopita lakini matokeo kama hayo yalipotokea moja kati ya mikoa ya Tanzania bara yalipambwa na kwa sura na rangi nzuri kama kwamba hakutana tatizo lolote baya linalotendeka katika maaneo hayo
sina uhakika kama kufanya hivyo ni kufuata maadili ya habari au ni utashi wa kumutimia bwana pesa na kampuni yake ya tumboni
kwa kweli katika kipindi cha miezi sita kijacho waandishi wengi watajitokeza na kuja Zanzibar eti kwa ajili ya kuandika masuala ya kisiasa, sijuwi ni siasa ipo wanayuitaka kuiyandikia wao?
ni suala la kujiuliza na kutafuta ufumbuzi kwani wengi wa waandishi hao huwa hawafahamu chochote kuhusu hali halisi na hitoria ya Zanzibar, bali wanachojali wao ni kuandika tu hata kama ni uongo au uzushi
ipo haja kwa wale waandishi makini ambao kwa kiasi kikubwa wanafahamu wanalolitenda kuifanya kazi hii, ili kuepuka kuwa na wao ni miongoni mwa mafarisayo
ni vyema ifahamike kuwa kalamu ya mwandishi wa habari kama haikutumika vizuri inaweza kuwa ni bomu la maangamizi kuliko lile la atomik

0 comments:

 
Top