Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imetekelezwa vyema Majimboni hatua ambayo inaweka wazi ushindi wa CCM katika ngazi zote katika uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025.
Mhe. Hemed ameeleza hayo wakati akiwasalimia wanachama wa CCM Jimbo laAmani, Jimbo la Shauri moyo na Jimbo la Kwahani akiendelea na ziara ya kukagua uhai wa Chama Mkoa wa Mjini Kichama.
Amesema Miradi mbali mbali mikubwa imetekelezwa chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa lengo la kuinua hali za wananchi wa Zanzibar kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 inavyoelekeza hivyo, CCM ina kila sababu ya kuendelea kushikilia Dola.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameendelea kukemea usaliti na makundi ndani ya CCM kwani hayana tija bali yatazorotesha utekelezaji wa Ilani na mpango mkakati wa Chama Cha Mapinduzi wa kuwaletea Maendeleo wananchi wake.
Amefahamisha kuwa CCM inaendeshwa kwa kusimamia Katiba na kanuni hivyo, changamoto yoyote ndani ya Chama itatuliwe kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa ili haki na usawa utendeke kwa wanachama wote.
Aidha Mhe. Hemed amesisitiza nidhamu na uwajibikaji ndani ya Chama kwa kuwataka Viongozi kuwajibika katika kutekeleza Ilani ya CCM na kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza ahadi zao walizoziahidi wakati wanaomba ridhaa ya kukaa madarakani 2020.
Ameeleza kuwa ushirikiano na uwajibikaji ndio silaha kubwa ya kuwapigia wapinzani hivyo hakuna haja ya kuwagawa wanachama kwa maslahi binafsi na badala yake wawaunganishe wanachama kwa maslahi ya CCM na Taifa.
Sambamba na hayo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka vijana kukilinda, kukitumikia na kukitetea Chama Cha Mapinduzi ambacho kina dhamira thabiti ya kusimamia maslahi yao na kuwataka kutumia fursa mbali mbali zilizopo nchini.
Mhe. Hemed amewahakikishia kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazijenga barabara zote za ndani kwa kiwango cha lami katika Majimbo ya Amani, shaurimoyo na kwahani ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa Zanzibar.
Amesisitiza suala la kusajili wanachama wapya ndani ya CCM ni la lazima sambamba na kuwasajili vijana waweze kupatiwa kitambulisho cha Mzanzibari ili waweze kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura.
Nao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu. Ussi Salum Pondeza na Ndugu Abdallah Manzi wameeleza kuwa ziara ya Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanyika muda sahihi baada ya kuwepo kwa makundi kipindi cha Uchaguzi wa Chama mwaka 2022.
Wameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini kitasimamia umoja na mshikamano katika majimbo ili kuheshimu maono ya waasisi na viongozi wakuu wa Chama hicho.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Dogo Iddi Mabrouk ameeleza kuwa Jumuiya ya Wazazi imepewa jukumu la malezi katika Chama hivyo watahakikisha ifikapo uchaguzi wa Dola wa mwaka 2020-2025 majimbo yote yatakjuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kura nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wao viongozi wa Majimbo hayo wamemueleza Mjumbe huyo wa Kamati Kuu kuwa wataendelea kuhubiri maendeleo yanayofanywa nchini na kuahidi kuwa ushindi wa asilimia kubwa kwa CCM katika Uchaguzi wa Dola ifikapo mwaka 2025.
Viongozi hao wamemuomba Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuziangalia changamoto walizowasilisha kwake ili ziweze kupatiwa utatuzi haraka jambo ambalo litazidisha uaminifu na mapenzi kwa Chama Cha Mapinduzi.
Katika ziara yake hiyo ya kukiimarisha chama cha Mapinduzi Mhe. Hemed amefungua kisima cha maji safi na salama Kilimahewa bondeni, amekagua ujenzi wa Tawi la CCM Mgandini.
Luluwa Salum
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:
Post a Comment