Zanzibar ni miongoni  mwa mkusanyiko wa visiwa vingi vinavyopatikana katika mwambao wa bahari ya Hindi. Na kawa kuwa sasa Zanzibar inatimiza mika 59 tangu kupinduliwa serikali ya kisultan 1964.
Kwa kawaida visiwa vya Zanzibar vipo ambavyo vinaishi watu na vipo vyengine ambavyo haviishi watu bali hutumika kwa shughuli mbali mbali za kijamii kama vile  uvuvi, kilimo na  na utalii.
Licha ya kuwepo visiwa kama Tumbatu, Uzi, Pemba, Kojani, Bawe, Changuu, Unguja na  vyenginevyo ambapo kisiwa cha Unguja ndio mji mkuu wa shushuli za kibishaara na Kiserikali.
Katika kisiwa cha Unguja ndipo penye mji mkuu wa Zanzibar, tukiachilia mbali mji wa Chake chake, Mkoani na Wete kule Pemba, lakini bado harakati za kuendesha visiwa na miji na vijiji za Zanzibar zinaratibiwa na kusimamiwa na Serikali kuu ambayo ipo Unguja.
Umaarufu wa kisiwa cha Unguja kutaitwa kwa jina la Zanzibar ni kwa sababu ndipo penye serikali kuu na pia ndio sehemu ya Mji mkuu, ambao unajulikana kama “Zanzibar city” kama ilivyo kwa Kuweit City, ingawaje walio wengi unapowauliza kuhusu jina la mji mkuu wa Zanzibar walio wengi huishia kusema Mkongwe, Forodhani ama Darajani, hii ni kutoka na mambo mbali mbali ambayo ni jamii au watendaji au taasisi husika kushindwa kutofautisha baina ya ng’ambo na mji mkuu.
Inawezekana pia baadhi ya taasisi kushindwa kufahamu mipaka yake ya kiutendaji na hasa katika muda huu ambao SMZ na wananchi wa Zanzibar waamini kwamba utalii ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi, ingawaje vipo baadhi ya vitu kama vikiendelezwa vinaweza vikao ndio chanzo kikubwa cha uchumi wa Zanzibar kuliko utalii kama ambavyo walio wengi wanaamini hivyo.
Tunaposema  knna baadhi ya taasisi zinashindwa kufahamu mipaka yao ya kazi hii, ni kwa sababu ndani ya mji wa Zanzibar ambapo tunangalia Mjini na Magahari yake kumekuwa na kukinza kwa baadhi ya taasisi ambazo kwa njia moja ama nyengine imekuwa ndio chanzo cha migogoro kati ya serikali na wananchi wake.
Kwa mfano ndani ya mji au jiji la Zanzibar, kuna Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, kuna wakuu wa Wilaya  2 wa  Magharibi A na B. Kuna Meya Jiji la Zanzibar na Meya wa Mji wa Zanzibar (Manispaa), kuna Meya 2 wa Maghrib A na B.
Licha ya hayo kuna wakurugenzi watatu Baraza la Manispaa Mjini, pamoja na wakurugenzi 2 wa Maghrib A na B, ambapo jumla ya watendaji wote katika Jiji la Zanzibar ni 11 ambapo wote hao mwisho wanaripoti pengine kwenye Wizara moja na wanafanya kazi za aina moja kwa kutumia bajeti na kasma tofauti ya fedha kutoka serikalini.
Ukifuatlia kwa makini mwenendo wa kiutandaji wa mgawanyiko wa viongozi 11 waliopo kwenye jiji la Zanzibar unaweza ukaona kama ni kutengeza migogoro ya kiutendji na mzigo mkubwa kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kwa kuwa Jiji la Zanzibar ni kitovu cha biashara hivyo hakuna shaka kwamba zipo baadhi ya Wizara ambapo ndani ya hizo wizara kuna idara ambazo kwa njia moja ama nyengine zinaweza zikahusika moja kwa moja na utunzaji na uimarishaji wa Jiji la Zanzibar kwa mfano, Wizara  inayosimia Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, ambapo ndani ya Wizara hii itakuwa imekusanya, Bazara la Manispaa Mjini na Maghribi, Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya, Meya wa Jiji la Zanzibar na Meya wa Manispaa.
Kwa kupitia Wizara hii utaona kwamba umebeba vitu vingi na vizito na inawezekana kabisa hata bajeti yake pengine isiweze kuhimili ya kuendesha taasisi zote hizo na ndio maana unaweza ukaona bado mji au jiji la Zanzibar limekuwa katika khatari ya kutokujuwa nani hasa mwenye dhamana ya kuliendesha na kulitunza jiji hili na ndio maana unaweza ukaona kwamba,  Mkuu wa Nchi akilalamika usafi na uchafu wa mji atakuwa anaiguza WIZARA hii muhimu ya Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ.
Si hivyo tu, bali pia zipo na Wizara nyengine ambazo pia zinamkono na jukumu kubwa la kutunza na kulifanya Jiji au Mji wa Zanzibar kuwa katika hali nzuri na bora kwa mfano Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, kwa njia moja ama nyengine hii nayo ni Wizara muhimu kwa sababu wao ndio wanahusika na mipango miji, usimamizi na matumizi mazuri ya ardhi, na kwa kwa kupitia wizara hii nadni yake ipo Idara ya Utambuzi wa Ardhi na mipango miji, lakini pia kwa kupitia wizara hii tunaweza ku;ipata Shirika la nyumba, inangawaje ni taasisi mpya
Aidha, Wizara ya  Ujenzi na Mawasiliano hii nayo ni miongoni mwa taasisi muhimu katika kuendeleza na mifumo bora ya  mawasilino ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ujenzi mzuri na wenye tija kwa taifa ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo bora ya mawasilino, ingawaje ipo haja kwa Serikali kuangalia upya mfumo na utendaji wa wa Wizara hii kwa kuondosha neon UJENZI na kulipeleka katika Wizara ya Aridhi na kama kuna haya ya kuwepo kwa Wizara hii basi ni vyema ikabadilihswa jina na kuwa Wizara ya MAWASILINO NA TEKNOLOGIA kwa sababu inaonekana kama Wizara hii kubeba kazi za taasisi mbili ambazo ni Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi pamoja na Tume ya Utangazaji Zanzibar.
Tunaposema Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano ibadilishe au ivunje hii ni kwa sababu ya mahitaji ya hali halisi ilivyo sasa kwa sababu mbali mbali lakini muhimu hapa ni kutokana na badiliko ya sayansi na teknologia karibu dunini kote kubalia na wizara hii kwa sasa ni mzima tu kwa serikali na hasa tunapoangali kazi na utendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar kubakia ndani ya Wizara ya Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo ni kuipa Wizara hiyo mzigo mzito wa kiutendaji na ufanisi kwa sababu ndani ya wizara hii kuna taasisi kubwa muhimu ambazo ni Shirika la Magazeti la Zanzibar leo, Shirika la Utangazaji (ZBC RADIO/ TV), Idara ya habari Maelezo, Shirika la Uchapaji, Tume ya Utangazaji  n.k.
Mbali ya hiyo, kuna Wizara ya Utalii na Mambo ya kale, ambayo pia kuna mambo mengi ya kufanyiwa kazi licha ya kwamba  Wizara hii ni mpya, lakini ndani yake ndio utaweza kuona chanzo kikuu cha wizara hii ambazo ni Kamesheni ya Utalii, Mamlaka ya Uhifadhi Mji Mkongwe pmoja na Idara ya Makumbusho na Mambo ya kale ambapo hapa ndio tunapogusa hasa suala zima la uhifadhi na utunzaji wa rasilimali muhimu ambayo ni historian na mambo mengine ya asili.
Kwa ujumla unapoangalia mpangilio na mtiririko wa taasisi hizo utaweza kuona kwamba Serikali inabeba mzigo mkubwa katika kulipa posho na mishara mingi kwa watendaji, ambapo kama kuna baadhi ya vitengo au taasisi nyengine zingeweza  kufutwa au kuunganishwa na taasisi husika, kwa ajili ya ufanisi Zaidi badala ya kuwepo wingi wa taasisi ambazo zinaongeza wingi wa lawama na mzigo kwa serikali.
Si hivyo tu lakini pia kwa kuangalia Wizara inayohusika na Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ , ambayo ndio kioo cha Jiji na Mji wa Zanzibar, kwani wizara hii inamzigo na jukumu kubwa la kulinda na kuimarisha uchumi wa nchi, kwa kupitia taasisi zake muhimu,
Lakini pia wizara hii imekusanya watendaji wengi, ambapo hesabu yao wanaweza kufikia 13/15, tukianzia na Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi, Wakuu wa wilaya watu, Meya wane, wakurugenzi wanne,  waliopo katika ngazi ya serikali kuu, ikiwa kila mmoja tuseme alipwe wastani wa shilingi milioni tano (5,000,000) kwa thamni ya shilingi ya Tanzania kila mmoja inamaana serikali ya Zanzibar kwa mwenzi mmoja inatumia wastani wa shilingi milioni khamisini na tano (55,000,000), hizo ni kwa mwenzi sasa ukifanya kwa miezi kumi na mbili 12 unaweza kapata jawabu kwamba fedha nyingi zinatumika kwa posho za watendaji. 
Aidha, unaweza ukajiuliza suala moja je nani mwenye dhamana ya kusimamia, kutunza  na kuendeleza Mji au Jiji la Zanzibar? Hapa kuna kitandawili na nishia kupata mtegeguzi.
Andapo Mji au Jiji la Zanzibar litakuwa na Msimamzi mzuri miongoni wa hao watendaji hapana shaka kwamba lile neno Zanzibar ni kitovu cha biashara linaweza likafanya kazi ipasavyo.
Vi vigumu kwa sasa kuweza kumshika mchawi au mkosa ambaye anadumaza  ustawi na malengo mazuri ya SMZ hasa katika suala zima la kukuza uchumi, kwa sababu, ukiangalia kwa  ghafala unaweza kuona kama kuna mwingiliano katika taasisi muhimu za Kiserikali, licha ya kwamba taasisi hizo zipo kwa mujibu wa sheria.
 Kwa mfano, unapoangalia kazi za Meya wa Jiji na Manispaa takribani ndio hizo hizo, lakini pia Meya wa Jiji na Mkuu wa Mkoa na wasaidizi wake ambao ni  Wakuu wa wilaya. Ingawaje wote wapo kisheria ila ipo haja ya kuwangalia upya jinsi ya utendaji wao kazi kwa ajili ya kupata ufanisi na utendaji ulio bora, si vibaya viongozi kuiga vitu vizuri na vyenye tija kwa taifa, na ndio maana kupitia ziara mbali mbali za ndani na nje ya nje, ni vyema kupitia  ziara hizo kuangalia wenzetu wanafanya nini katika kuimarisha miji na majiji yao. Kwa kulingalisha na kutofautia uwepo wa Meya, Mkuu wa Mkoa pamoja na Wakuu wa wilaya, ni vyema Serikali kuweza kuliangalia vizuri suala hili.
Ushauri kama ipo haya ya kufanya mabadiliko, basi Serikali ingeweza kuangalia kwa kina kuhusu mabadiliko ya kiutendaji katika Wizara hii ya Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, ambapo kama upo uwezekano vipo baadhi ya vyeo vingesimamishwa kwa muda ili kuona kama ufanisi utapatikana kupitia mabadiliko hayo na hasa iangalie zaidi nafasi za Wakuu wa Wilaya, Wagurugenzi wa Manispaa na Halmashauri na pia kati ya Meya na Mkuu wa Mkoa.

0 comments:

 
Top