Kasri ya Kibweni au Ikulu ya Kibweni, imejengwa mwaka 1915 chini ya usimamizi wa Seyyid Khalifa bin Haroub bin Thuwein, ambaye  aliitawala Zanzibar ktoka mwaka 1911 hadi 1960.
Kasiri hili,  lipo nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambapo kwa miaka hiyo ilikuwa shamba lakini kwa sasa kasri hili lipo chini ya serikali ya mkoa wa mjini Magharibi.
Kwa wakati huo jengo hili likijulikana kwa jina la “Kasrusaada”, ikiwa na maana “Nyumba ya Starehe”. Msanifu wa majengo wa Serikali maarufu kwa wakati huoB w. John H. Sinclair ndiye aliesarifu ujenzi wa jengo hili katika mtindo wa Kiislam.
Nyumba hii ilikuwa inapendeza mno kwa kusheheni mapambo ya aina kwa aina pamoja na vitu vya thamani vya watawala waliofuta baada ya mwaka 1960, ndani ya kasri hii kulikuwapo na  magudulia makubwa ya thamani kutoka China,  ambayo yalipambwa kwa nakshi za kipekee na zakuvutia pamoja na  sahani za shaba ambazo kilikuwa ni kivutiao kikubwa cha wageni waliohudhuria maghali mbali mbali katika kasri hii ya kibweni.
Mbali na hayo,  kasha la zamani kutoka Arabuni, nyaraka mbalimbali, picha mbili kubwa za zilizochorwa na msanii maarufu, Bw. Shariff Al – Mansoor, ni miongoni mwa vitu vya kuvutia vilivyokuwemo ndani ya ukumbi wa kasiri  la Kibweni
Kwa upande wa nje, kasri  hili lilikuwa limeipambwa kwa bustani nzuri ya kuvutia kwa wakati huo,  ikiwa na aina mbalimbali za miti ya matunda na maua kama vile muembe wa Alfonso (mbichi tamu), mifurusadi, mikiluwa, miembesakua (embe ng`ongo) na mengineyo, ambapo badhi ya miti hiyo kwa sasa imepotea na ni michache ndio iliyobakia katika kasri hili.
Kupote kwa miti hiyo, kwa kiasi kikubwa imechangia kupotea kwa  baadhi ya ndege maarufu visiwani Zanzibar kama vile dhwarde, mnana, chozi na wengine wengi, Wakati wa utawala wa mfalme kasri hili lilipambwa na kuvutia kutokana na uwepo wa ndege kama njiwa, tausi   pamoja na wanyama kama vile farasi n.k.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964,  jengo hili lilikuwa chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kujuilikana kama Ikulu ya Kibweni.  Jengo hili lilitumika kama sehemu ya mapumziko kwa Maraisi wa awamu tofauti pamoja na kufanyia mikutano ya kiserikali. Kwa sasa ndani ya jengo hili kuna maonesho ya Mabadiliko ya Zanzibar Karne ya 19 na pia maisha na matumizi ya jengo tokea wakati huo lilipojengwa mpaka sasa.
kasri la Kibweni au Ikuli ya Kibweni imegawika katika sehemu kuu tatu, ambapo kuna sehemu ya , ambayo ilitumika kama makaazi ya ndugu wa karibu wa Sultani, ambapo katika sehemu hii kuwelikuwepo na eneo maamu  la mazungumzo ya faragha.
seheumu hii ilitengwa maalumu kwa ajili ya wageni walikwenda kuonana na Sultani , ambapo ndani yake kulikuweko  chumba maalumu cha walinzi wanaume wa Kasri, mabanda ya tausi, njiwa na farasi.
Eneo hili pia lilikuwa likitumika kama makaazi ya watumishi wa kike na watoto wao. Na sehemu iliyobakia kulikuwa na jiko kwa ajili ya kupikia chakula cha Sultani na wageni wake maalumu waliofika hapo kwa mwaliko. Kwa sasa eneo hili la chini limetengwa kwa ajili ya maoenesho na hasa kuhusiana na historia  ya Zanzibar katika karne ya kumi na tisa katika kipindi ambapo Zanzibar ilikuwa kitovu kikuu cha biashara na mahusino ya Kidiplomasia kwa eneo lote la Mwambao wa Mashariki ya Afrika.
Eneo jengine la kasiri ni ile sehemu ya  juu ambayo nayo iligawanywa katika sehemu kuu mbili  ambazo ni Ukumbi wa mikutano aliokuwa akiiutumia  Sultani kukaa na wageni wake maalumu na ulikuwa na samani nyingi kama vile makabati ambayo yaliyowekwa nyaraka mbalimbali.
Baada ya Mapinduzi ya 1964 ukumbi huu uliendelea kutumiwa kwa shughuli za mikutano katika awamu mbalimbali za Marais walioingoza Zanzibar.
sehemu ya pili ilikuwa ni chumba cha Seyyida Salme kimepambwa kwa picha  na samani mbali mbali zenye ukumbusho wa bint Mfalme huyo. Awali chumba hicho kikitumika kama ukumbi wa chakula ambao ulikuwa ukichukua watu wasiozidi kumi na sita (16), pia palikuwa na mafeni ambayo yalipepea kwa kutumia mikono. Ukumbi huu ulitumika kwa ajili ya chakula cha mchana tu.
Eneo la mwisho katika kasri hili ni ghora ya pili, ambapo  lilitumika kwa matumizi binafsi ya Sultani na lilikuwa na vyumba vya kulala, ukumbi mdogo wa kupumzikia, choo na sehemu ya kubadilishia nguo, pamoja na veranda ya kupumzikia na kupitishia hewa. Matumizi haya yaliendelea hata baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 katika awamu za Marais mbali mbali.
Mbali na mtumizi yote hayo, ambayo yaliyokwisha fanyika awali, kwa muda huu serikali ya Dk.Hussein Ali Mwinyi, imeamuwa kulifanya kasri hili kuwa ni miongoni mwa makumbusho, kwa ajili ya kuhifadhi na kutunza mali na historia ya Zanzibar.
Uamuzi huu wa Serikali ya Zanzibar imekuja kutoka na khitilafu zilizojitokeza katika Kasri la Forodhani (Jumba la Wananchi la Forodhani) ambapo kwa sasa kasri hili lipo katika hali mbaya na linahitaji kufanyiwa matengezo makubwa..
Katika kuhakisha kwamba mali na saamni zilizomo ndani ya makasri haya, ndipo juhudi za makusudi zimechukuliwa kwa kuzihamishia Kibweni ambapo wananchi na watalii watapata fura nzuri ya kuweza kutembele kwenye kasri la kibweni kwa ajili ya kuona na kujifunza histori ya Zanzibar kutoka karne ya 19 hadi sasa.
kitu cha msingi kwa jamii ni kwenda kutembelea ndani ya kasri hilo la Kibweni kwa ajili ya kupata taaluma zaidi, hii ni kwa sababu makumbusho ni yao sio ya wageni.
lakini  ipo haja kwa Idara husika kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kufanya ziara za mara kwa mara kwenye sehemu za kihistoria ili kijifunza na kupata elimu zaidi ya mambo ya kale, inawezekan timiza wajibu wako.

0 comments:

 
Top