RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema suala la msaada wa
kisheria sio la Zanzibar pekee, bali ni la kimataifa, lina historia kubwa duniani.
Alisema, Zanzibar
inawajibu wa kukeleza kwa vitendo huduma za sheria kama lilivyoelezwa kwenye
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 12 pamoja na Sheria nyengine
mbalimbali zilizopo nchini.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa Sheria, yaliyofanyika ukumbi wa Idrissa Abdul wakili, Kikwajuni Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, watoaji wa msaada wa sheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa wananchi wasio na uwezo wa fedha katika msada wa sheria.
Dk. Mwinyi alieleza lengo la kilele cha maadhimisho hayo ni kuzifanya huduma za kisheria kuwa endelevu na zenye kuleta tija kwa jamii sambamba na kutatua changamoto nyengine zinazokwaza huduma za utoaji wa kisheria nchini.
Alieleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora itaendelea kushirikiana na watoa msaada wa kisheria kwa kuhakikisha wanaendelea kutwaa tunzo zaidi, pia wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Pia Dk. Mwinyi alieleza Serikali itahakikisha marekebisho ya Sera na Sheria ya Msaada wa Kisheria yanafanyika kwa ufanisi na haraka ili kukidhi matakwa yanayotakiwa.
Akizungumzia suala la upatikanaji wa vifaa na vitendelea kazi kwa wasaidizi wa wasaidizi wa kutoa msaada wa sheria, Rais Dk. Mwinyi aliwaahidi kwamba seikali inaungamkono shughuli wanazozifanya b
upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi nayo ni changamoto nyengine. Mazingira wezeshi ya utoaji huduma yanahitaji kuwa na vifaa vya kutosheleza, vikiwemo vyombo vya usafiri, vifaa vya Ofisi kama vile printa, mashine za Fotokopi, Komputa na kadhalika. Vinapokosekana vifaa hivi, ni dhahiri kuwa daraja la ufikiaji haki nalo hukosekana.
Aidha, aliwataka
watendaji mbalimbali wa Serikali na taasisi binafsi na vyombo vya kusimamia
haki, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Watoaji msaada wa kisheria ili
kuwajengea uwezo wa kufanikisha kazi zao kwa uweledi. Sambamba na kuwaunga
mkono na kupata ushirikiano wa kutosha.
Hata hivyo alitoa kwa jamii nakuwataka kutimiza wajibu wao kila mmoja kwanafasi yake ili kuwe na mazingira bora ya upatikanaji msaada wa kisheria na kuzidi kuimarisha kiwango cha utawala bora nchini na misingi ya haki za binadamu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Jaji Mstafu Robert Makaramba alisema, maadhimisho ya 2023 yamekwenda sambmba na mazingira ya uboreshaji wa mifumo, miundo, sera na sheria zinazohakikisha huduma za msaada wa sheria zinatolewa katika hadhi ya zenye lengo la kufikia uwezeshaji wa Serikali kwa kushirikiana na watoa msaada ya kisheria, wadau wa maendeleo, taasisi za kiraia, wadau wa sekta za haki wakiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Polisi, Chuo cha Mafunzo na jamii husika.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Hanifa Ramadhan Said alieleza, watoaji wa msaada wa sheria wanafanya kazi kwa kujitolea na uzalendo kwa uhakikisha wananchi wa Zanzibar wasio na uwezo wanafikiwa na huduma za kisheria kwa sehemu zote ili kutatuliwa haja zao kisheria.
Alisema, maadhimisho
hayo walishirikiana na taasisi zote zinazohusu masuala ya sheria, wakiwemo
Mahakama, jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu, Chuo cha Mafunzo na wadau wengine.
Maadhimisho hayo ya msaada wa sheria yaliyokuwa na kauli mbiu “Mazingira wezeshi kwa watoa msaada wa kisheria ni daraja la upatikanaji haki” ambayo yalianza Julai 17 na kuadhimishwa Julai 22 mwaka huu yalitanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji ikiwemo kampeni ya vyumbo vya Habari, mkutano na vyombo vya Habari, kutembelea vyombo 21 vya Habari, kufanya program ya vijana kwa Unguja na Pemba, mihadhara na jamii, kufanya usafi wa mazingira kwenye hospitali ya wagonjwa wa Akili, Kidongochekundu, kufanya bonaza na hatimae kuadhimisha kilele halisi wiki ya msaada wa kisheria.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa Sheria, yaliyofanyika ukumbi wa Idrissa Abdul wakili, Kikwajuni Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, watoaji wa msaada wa sheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa wananchi wasio na uwezo wa fedha katika msada wa sheria.
Dk. Mwinyi alieleza lengo la kilele cha maadhimisho hayo ni kuzifanya huduma za kisheria kuwa endelevu na zenye kuleta tija kwa jamii sambamba na kutatua changamoto nyengine zinazokwaza huduma za utoaji wa kisheria nchini.
Alieleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora itaendelea kushirikiana na watoa msaada wa kisheria kwa kuhakikisha wanaendelea kutwaa tunzo zaidi, pia wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Pia Dk. Mwinyi alieleza Serikali itahakikisha marekebisho ya Sera na Sheria ya Msaada wa Kisheria yanafanyika kwa ufanisi na haraka ili kukidhi matakwa yanayotakiwa.
Akizungumzia suala la upatikanaji wa vifaa na vitendelea kazi kwa wasaidizi wa wasaidizi wa kutoa msaada wa sheria, Rais Dk. Mwinyi aliwaahidi kwamba seikali inaungamkono shughuli wanazozifanya b
upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi nayo ni changamoto nyengine. Mazingira wezeshi ya utoaji huduma yanahitaji kuwa na vifaa vya kutosheleza, vikiwemo vyombo vya usafiri, vifaa vya Ofisi kama vile printa, mashine za Fotokopi, Komputa na kadhalika. Vinapokosekana vifaa hivi, ni dhahiri kuwa daraja la ufikiaji haki nalo hukosekana.
Hata hivyo alitoa kwa jamii nakuwataka kutimiza wajibu wao kila mmoja kwanafasi yake ili kuwe na mazingira bora ya upatikanaji msaada wa kisheria na kuzidi kuimarisha kiwango cha utawala bora nchini na misingi ya haki za binadamu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Jaji Mstafu Robert Makaramba alisema, maadhimisho ya 2023 yamekwenda sambmba na mazingira ya uboreshaji wa mifumo, miundo, sera na sheria zinazohakikisha huduma za msaada wa sheria zinatolewa katika hadhi ya zenye lengo la kufikia uwezeshaji wa Serikali kwa kushirikiana na watoa msaada ya kisheria, wadau wa maendeleo, taasisi za kiraia, wadau wa sekta za haki wakiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Polisi, Chuo cha Mafunzo na jamii husika.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Hanifa Ramadhan Said alieleza, watoaji wa msaada wa sheria wanafanya kazi kwa kujitolea na uzalendo kwa uhakikisha wananchi wa Zanzibar wasio na uwezo wanafikiwa na huduma za kisheria kwa sehemu zote ili kutatuliwa haja zao kisheria.
Maadhimisho hayo ya msaada wa sheria yaliyokuwa na kauli mbiu “Mazingira wezeshi kwa watoa msaada wa kisheria ni daraja la upatikanaji haki” ambayo yalianza Julai 17 na kuadhimishwa Julai 22 mwaka huu yalitanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji ikiwemo kampeni ya vyumbo vya Habari, mkutano na vyombo vya Habari, kutembelea vyombo 21 vya Habari, kufanya program ya vijana kwa Unguja na Pemba, mihadhara na jamii, kufanya usafi wa mazingira kwenye hospitali ya wagonjwa wa Akili, Kidongochekundu, kufanya bonaza na hatimae kuadhimisha kilele halisi wiki ya msaada wa kisheria.
0 comments:
Post a Comment