Wahenga walisema “mafahali wawili wakipigana ziumiazo ni nyasi” lakini pia wapo waliosema “vita vya panzi neema kwa kunguru”.
Hii  ni misemo miwili yenye maana tofauti ingawaje ukiitazama kimanti inawezekana ikiwa na maana mmoja ila sio kweli kudhania hivyo.
Sikuwa na nia ya kuanza na misemo hiyo kwa sababu waswahili huwa na maana pana pindi wakitumia methali hizo.
Ni muda sasa tangu vita kati ya Urusi na Ukraine vikiwa vinaendelea, huku maafa na majanga mbali mbali yakiwa yamekithiri ktote barani Ulaya.
Ni mara nyingi matiafa ya Ulaya yalikuwa yakizungumza wakimbizi walikuwa nazingusa nji za Afrika na Bara Arabu, lakini kwa bahati mbaya , wahenga walisema “mambo kangaja huendea yakaja” na sasa yamekuja kweli, maana kwa mara ya kwanza Ulaya imetowa wamkimbizi juu ya kwamba ustarabu na maaendeleo yapo kwako.
Inawezeka kabisa hili la ukimbizi ni jambo jipya kwa watu wa ulaya kwa sababu  wamezowea kuona wakimbizi kutoka Afrika, Bara Arabu na baadhi ya nchi za bara la Asia.
Kuendelea kwa vita hivyo kwa kiasi Fulani kumepeleka kuufanya uchumi wa dunia kuyumba na baadhi ya sarafu  kuanza kuporomoka kutoka kwenye thamani yake halisi na kuwa katika kiwango cha chini ambapo haikutarajiwa kwa jamii ya kimataifa na hasa bara ulaya.
Kwa hakika dunia imekumbwa na mfadhaiko mkubwa, kaisi ambacho mabwannyenye wa dunia ambao hujifanya vinara wa kutunza amani na kusimamia demokrasia kwa sasa wameemewa hawajuwi la kufanya.
Kwa kiasi kikubwa vita vya  Urusi na Ukraine vimeleta kizazaa kibwa na hasa katika Nyanja mbili,  usafiri na kilimo. Tunaposema kilimo tunamaananisha ukosefu wa NGANO ya kutokasha kutapelekea baadhi ya mataifa kufa njaa. Kwa sababu wakulima wawili wapo kwenye mapambano ya kutaka kutanua ardhi zao kwa ajili ya kilimo ama kisiasa Zaidi.
Na tunaposema kilimo, tukumbuke kwamba Urusi ndio msambazaji mkubwa wa mbole na huhitajika karibu mataifa yote iwe Afrika, Ulaya na hata Marekani ambao waliowengi wanaona kwamba hili ndio taifa pekee lenye nguvu duniani, kumbe sivyo ilivyo, wao  ni wasaka tonge tu.
Kwa maana hiyo, upo uwezekano mkubwa kwa sekta ya kilimo nchini, kuteterekea kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha vita, si tu Tanzania au Afrika bali kwa mataifa mengineya Ulaya na Amerika pia.
Ila kwa kuwa kila aliaye hulia mama yangu, na hakuna anayelia ambaye husema mama yetu hata kama msiba unawahusu ndugu wa ukoo mmoja, hivyo basi ipo haja kwa wizara husika kufikiria njia mdala kabla athari hajianza kuwa kubwa kwa wakulima wetu kwa ajili ya kukosa mbolea (pembejeo).
Athari nyengine, ambapo imeanza kuonekan ni mfumuko wa bei ya ngano kutoka 2,000/- bei ya awali hadi kufikia 2,600/- bei ya sasa kwa kisiangizo eti cha mapambano kati ya mafahali wawili wa ulaya.
Hatukatai kama kuna vita, bali wafanya biashara manatakiwa kuwa waadilifu, kwa sababu ngano ambayo ipo sokoni imeingizwa lini nchini? Na siitoshe hebu semeni ukweli inachukuwa siku ngapi meli kutoka Urusi na Ukraine kulete ngano Tanzania hata ngano ipande ghafla bin vuu? Au ushuru wa forodha umependa kiasi gani?
Ukosefu wa uadilifu inawezekana ndio chanzo cha mfumo wa bidhaa nchini kwa kisingizo cha vita, hii sio sahihi hata kidogo na hasa ukizngatia kwamba zimebabaki siku chache wa kuingiza mwezi Mtukufu wa Ramadhani, inawekana kabisa faida ikawa nzuri ila isio na maana mbele ya Mungu, kwa sababu ya kufanya khadaa na kusema uongo, na kwa masaba huo kama ni muumini angalia faida unayopata je ni halali yako au ni kharamu yako?
Ama kwa upande wa usafari, nako kumetetereka kwa asilimia kubwa na hasa kutokana na kutokuwepo kwa mafuta ya kutosha, ambapo Urusi pia ni muuzaji na mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani.
Kinachoshangaza ni kwamba, Urusi imewekewa vikwaza ktokana na shindikizo la Marekani, kwa madani ya ukiukwaji wa haki za Binadamu, mbona UN imeshindwa kuwawekea vikwaza Israel kwa kuwauwa Wapelestina ndani ya nchi tena ni zaidi ni mika 40 sasa? Mbona hatujasikia UN kuiwekea vikwaza Saudi Arabia kwa kuvamia Yemeni kwa zaidi ya miaka saba vita vinaendelea na watoto, wazee wangapi wanakufa hapo? Mbona hatujsaikia UN kuchukuwa hatua yoyote kwa serikali ya Mymary kwa kuwa watu wajamii ya Rohingya? Mbona hajutasiki UN kuwachukuwa hatua wale waliojifanya umoja wa kujihami NATO kwa kuwauwa maelfu ya watu ma watoto Parkisatani, Libya, Iraq?
Inawezekana kabisa hao wate hawakuwa watu ni wanyama ndio maana UN iliufanya mkia watu ni wa UKRAINE pekea yao? Hebu ufanye tathmini wa opereshini za NATO zimeuwa na kuwangamiza watu wangapi halafu tupewe na thamni halisi wa waliokufa Ukraine kwa sababu ya uvamizi wa Urusi? Alichokifanya Urusi na uvamizi wa NATO ni dhambi moja tu wote wameuwa na wanaendelea kuua bila ya sababu, ila kilichojitokeza hapo ni tofauti ya soji la punda tu, lakini punda ni yule yule.
Tunayoyaeleza sio kwamba tunashabikia vita hivyo la hasa, ila kuwepo na uhalisi na ukweli wa taarifa sio kuwepo na ubaguzi wa taarifa, kama vikwazo vya kiuchumi vilivyoweka Urusi basi vilipaswa kabisawa kuwekewe Saudi arabi, Israel pamoja na nchi zpote wanachama wa NATO, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tonny Blair alikiri hadharani kwamba walivamia Iraq kijesi bila ya hata sababu ya msingi, cha ajabu UN, Mahakama ya uhalifu wa kivita ipi, vyote vilivyamaza kimya na kuwasubiri viongozi wa Afrika akina Omar Al bashri kuwatia hatiani kwa vile wao akina NATO ni watakatifu hawana makaosa.
Bado narudia kusema tena “vita vya panzi neema kwa kunguru” ipo haja kwa nchi za Afrika hasa Tanzania, kwa vile Mungu ame;libarikia taifa hili kuwa na maliasili nyingi na za kuitosheleza, kuanza kufikiria njia mbadala ya kupata nishati hasa ya mafuta na gesi.
Kwa sababu kwa hali halis ilivyo sasa kutokana na vita na vikwaza vinavyoweke na baadhi ya mataifa vinaweza kulete madhara kwa makubwa na inawezekana kukwamisha harakati za kimaendeleo na mikakati ya taifa.
Licha ya kwamba tunaweza tukawa na gesi na mafuta yetu, suala la msingi ni je yanatosheleza? Ikiwa hayatoshelezi ipo siku sekta ya usafiri wa bahari, anga na nchi kavu vinaweza vikateterekena kuitoka na mambo kama hayo ya vita, kwa hivyo ipo haja ya kufikiria mfumo mpya ma magari ama kutumia chaji au gesi.
Mbali na mafuta na gesi, kitu cha pili ni sekta ya kilimo, vita vya Urusi na Ukraine iwe ni somo tosha kwa taifa, na mkazo sasa katika kilimo cha ngano.
Ni lazima ufanyike utafiti wa kutoka kupia wizara husika ile ya kilimo na biashara kuweza kuwa na takwimu sahihi za uangizwaji wa ngano nchini upo kwa kiasi gani na serikali ifanye nini katika kukiimarisha kilimo hicho, kwa sababu mtegemea cha ndugu hufa masikini.
Vita hivi vya kiuchumi kati ya Ulaya na Marekani, iwe ni fundisho tosha kwa mataifa ya Afrika na kunahitaka umoja thabiti wa Afrika ambao utaweza kusimamia si tu masuala ya kisiasa lakini kuwepo na mkakati maalumu wa kukusa na kusimamia sekta ya kilimo.
Wito wangu kwa Watanzani tunapaswa kujifunza nyakati badala ya kuwa washabiki wa baadhi ya mataifa kwa sababu tunayependa kulinga na wanavyoonekana kwenye maigizo ya Tv, kwa sababu kwana tofauti kubwa kati ya maisha halisi na maigizo ya kwenye Tv.

0 comments:

 
Top