Picha BBC News
Biashara ya utalii ni miongoni mwa vitega uchumi ambavyo kwa sasa inaonekana kunawiri katika kila pembe ya visiwa vya Zanzibar.
Kuimarika kwa SEKTA hii ya utalii kwenye visiwani vya Zanzibar inaonekana ni jambo la faraja kwani, imepelekea vijana wengi wa waishio ndani na nje ya visiwa hivi kuweza kupata ajira, ingawaje bado si ajira rasmi
Hapana shaka kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea kuimarika kwa sekta hii, ambayo nathubutu kusema kwamba ndio uti wa mgongo na tegemeo la uchumi si tu kwa wananchi bali hata kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ingawaje bado kunahitajika mipango imara ya kuendeleza sekta hii ya utalii visini Zanzibar.
Katika
mataifa mengii sekta ya utalii huwa ni moja wapo katika ya vyanzo vya kuonegeza
au kuinua uchumi wa nchi husika na hasa inatizamiwa kwa mwananchi kwani wao
ndio walengwa katika sekta hii.
Ingawaje
ni vigumu kwa nchini kama Tanzania kesema kwamba sekta imekuwa bado ni kitendawili kisicho na
mteguazi, hii ni kutokana kwamba bado faida ya utalii nchini ni ndogo
kulinganisha na mataifa mengine ulimwenguni.
Nakubaliana
na juhudi za Serikali ya Zanzibar imekuwa
ikifanya juhudi kubwa katika sekta hii na
kuleta tija kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla.
Kuimarika
kwa njia ya Nungwi kumepelekea kukuza sekta ya Utalii kwa Mkoa wa Kaskazini,
hivyo ipo haja juhudi zifanyike ili kupunguza masafa na machofu kwenye njia
inayokwenda Mkoa wa kusini Unguja.
Ifahamike
kwamba kuwepo kwa barabara zenye viwango vionavyotambulika kwa mujibu wa
Mkandarasi iwezesha watalii watembeleao Zanzibar kutokuwa na mashaka wala
wasi wasi wowote katika safari zao za kuelekea Kiwengwa ama Nungwi kwani huwa
wanafika kwa wakati unaotakiwa.
Lakini
pia kuwepo kwa barabara zilizojengwa vyema imepelekea hata wenyeji wa
maoneo ya utalii kuweza kufanya shughuli zao bila ya khofu na hasa wakati wanapopoleka mazo yao katika hoteli na
maeno mengine ya mji wa Zanzibar kwa ajili ya kutafuta soko zaidi la bidhaa zao
ambzo kuuza kwao ndio manufaa kwao na jamaa zao, lakini pia hata kuimarika kwa
kipatop cha mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.
Lakini
pia barabara zinajengwa sasa zizingatie wiwango wakimataifa, badala ya kujenga
kwa mazoweya, ulinzi na taa za barabara ni miongoni mwa mambo muhimu hata
katika nyakati za usiku.
Aidha wimbi kubwa la vijana ambao hutoka nje ya nchi hufika Zanzibar kwa ajili ya kutafuta ajira na hufakiwa kuchukuwa ajira kiulani katika sekta ya utalii, hii ni kwa sababu hapo awali vijana wengi wa Kizanzibar walikuwa hawapo tayari kuingia kwenye sekta hii ya utalii lakini kutokana na ukata wa maisha unaoikabili taifa vijana wengi waishio visiwani humu nao sasa wamekuwa mstari wa mbele katika sekta hii ya utalii.
Tatizo
kubwa ambalo linawakabili vijana wa Zanzibar ni kutokana kwamba baadhi ya
nafasi za kazi kwa upande wao zinakuwa ni ngumu kutokana mazoweya au utamadunni
uliyopo, lakini hii ilikuwa kabla na sio
muda huu tena kwani hata vijana wa Kizanzibar nao wamekuwa wahudumu wabaa hata
kama ni hoteli ya kitalii jina na matendo ni yale yale.
"Bado kuna mengi yanapaswa kufanyiwa kazi i katika sekta hii ya utalii, kwa mfano umeme umekuwa ni tatizo kwani mara kwa mara huwa unakatika pamoja na ukosefu wa maji maeneo meng, kwa hivyo kama hali hii isiporekebishwa itaathiri sana sekta ya utalii ambayo ndiyo imetupa vijana ajira na kutoa pato kubwa kwa serikali" alisema Bi.Laura Bonara meneja wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Asko.
Mbali ya kuwa, utalii ni chanzo tegemezi kwa uchumi wa Zanzibar, lakini ni ukweli usiofichika kwamba sekta hii imeathiri sana mila, tamaduni na silka za Kizanzibar, hii ni kutokana kwamba vinaja wengi wamekuwa wakiinga mambo mabaya na kuacha mazuri ya kwao kwa kudhani kwamba kufanya hivyo ndio kwenda na wakati.
Ni
dhahiri kwamba Zanzibar ya leo sio ya jana wala juzi vijana na watoto wote
wamekarambuka na kama juhudi za makausudi hazikuchukuliwa, sekta ya utalii
itakuwa ni silaha tosha ya kuangamiza na kuondosho uatamaduni wa pwani na
sitoshangaa kwamba badala yake itakuwa kama ITALIA au UFARANSA ndogo.
Biashara ya utalii ni miongoni mwa vitega uchumi ambavyo kwa sasa inaonekana kunawiri katika kila pembe ya visiwa vya Zanzibar.
Kuimarika kwa SEKTA hii ya utalii kwenye visiwani vya Zanzibar inaonekana ni jambo la faraja kwani, imepelekea vijana wengi wa waishio ndani na nje ya visiwa hivi kuweza kupata ajira, ingawaje bado si ajira rasmi
Hapana shaka kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea kuimarika kwa sekta hii, ambayo nathubutu kusema kwamba ndio uti wa mgongo na tegemeo la uchumi si tu kwa wananchi bali hata kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ingawaje bado kunahitajika mipango imara ya kuendeleza sekta hii ya utalii visini Zanzibar.
Aidha wimbi kubwa la vijana ambao hutoka nje ya nchi hufika Zanzibar kwa ajili ya kutafuta ajira na hufakiwa kuchukuwa ajira kiulani katika sekta ya utalii, hii ni kwa sababu hapo awali vijana wengi wa Kizanzibar walikuwa hawapo tayari kuingia kwenye sekta hii ya utalii lakini kutokana na ukata wa maisha unaoikabili taifa vijana wengi waishio visiwani humu nao sasa wamekuwa mstari wa mbele katika sekta hii ya utalii.
"Bado kuna mengi yanapaswa kufanyiwa kazi i katika sekta hii ya utalii, kwa mfano umeme umekuwa ni tatizo kwani mara kwa mara huwa unakatika pamoja na ukosefu wa maji maeneo meng, kwa hivyo kama hali hii isiporekebishwa itaathiri sana sekta ya utalii ambayo ndiyo imetupa vijana ajira na kutoa pato kubwa kwa serikali" alisema Bi.Laura Bonara meneja wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Asko.
Mbali ya kuwa, utalii ni chanzo tegemezi kwa uchumi wa Zanzibar, lakini ni ukweli usiofichika kwamba sekta hii imeathiri sana mila, tamaduni na silka za Kizanzibar, hii ni kutokana kwamba vinaja wengi wamekuwa wakiinga mambo mabaya na kuacha mazuri ya kwao kwa kudhani kwamba kufanya hivyo ndio kwenda na wakati.
0 comments:
Post a Comment