Ugonjwa au tatizo la maumivu ya nyonga yanaweza kutokea kwa mwanaume na mwanamke pia yanaweza ikatokea hali isiyo ya kawaida katika viungo vya ndani, au maumivu kutoka kwenye mifupa ya nyonga. 

Kwa wanawake, maumivu ya nyonga yanaweza kuhusishwa na mfumo wa uzazi na hasi katika kile kipindi chankuingia kwenye hedhi. 

Wapo baadhi ya wanawake ambao huingia ndani ya siku zao na kupatwa na tatizo hilo, hivyo mara nyingi matibabu yake hutegemeaana sana na chanzo cha maumivu yake.
 
Maumivu ya nyonga yanaweza kuwa ishara kwamba kunaweza kuwa kuna tatizo kati ya viungo vya uzazi ndani ya eneo la nyonga za mwanamke.

Ingawa maumivu ya nyonga mara nyingi hutokana na maumivu katika maeneo ya viungo vya ndani vya uzazi, basi maumivu ya nyonga yanaweza kuwepo wakati wa kufanya tendo la ndoa n.k.

Maumivu ya nyonga yanaweza kuwa dalili ya maambukizi au yanaweza kutokana na maumivu kwenye mifupa ya nyonga au katika viungo vya ndani visivyokuwa vya uzazi. Kwa wanawake hata hivyo, maumivu ya nyonga yanaweza kuwa ishara kabisa kwamba kunaweza kuwa na tatizo ndani katika mojawapo ya viungo vya ndani vya uzazi katika maeneo ya nyonga kama vile mfuko wa uzazi(uterus), vifuko vya mayai(ovaries), mirija ya uzazi(fallopian tubes), pamoja na uke(vaginal ).

Visababishi vya maumivu ya nyonga kwa mwanaume na mwanamke huwa ni pamoja na mambo haya yafuatayo:

👉. Matatizo ya kibofu cha mkojo
👉. Kidole tumbo
👉. Magonjwa ya zinaa
👉. Maambukizi katika figo au mawe kwenye figo
👉. Matatizo ya utumbo
👉. Matatizo ya mshipa wa ngiri
👉.Mifupa ya nyonga iliyovunjika.

Visababishi vinavyowezekana vya maumivu vya nyonga kwa wanawake tu ni pamoja na  haya yafuatayo:

👉. Ujauzito
👉. Mimba kutunga nje ya kizazi
👉. Mimba kutoka
👉. Maambukizi katika via vya uzazi au PID
👉. Yai kupevuka
👉. Maumivu wakati wa hedhi
👉. Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
👉. Uvimbe katika tumbo la uzazi(uterine fibroid)
👉. Endometriosis
👉. Saratani ya shingo ya kizazi, nk

0 comments:

 
Top